LIVE UPADTES: M4C DAR - Lengo ni Kukusanya Bilioni 5 CHANGIA MABADILIKO

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
M4C.jpg

Kampeni ya Kuchangia harakati za Mabadiliko M4C Nchini zitaonyeshwa Live kupitia Kituo cha Luninga cha Star TV kuanzia saa 2 na Nusu Usiku na lengo ni kukusanya shilingi Bilioni Tano.


Mratibu wa Fund rising hiyo Mh. Kamanda Godbless Lema amesema fedha hizo zitatumika kununulia magari yatakayowezesha kufika kila maeneo nchini na kuhamasisha mabadiliko pamoja na kugharamia kampeni zote za ukombozi kamili wa Mtanzania.


Kila mpenda mabadiliko anatakiwa kuweka kiasi cha fedha katika simu yake kuanzia shilingi 1000 - 1000000 na kuendelea na zitatangazwa namba za MPESA ambazo zitatumika kufanikisha azma hiyo kwa malengo ya Muda Mrefu.

JINSI YA KUCHANGIA: Updated

Kwa watumiaji wa VODACOM: Watumiaji wa Mitandao mingine vuteni subira kidogo kama nilivyobainisha hapo chini:


Bonyeza *150# baada ya hapo bonyeza 4, kisha weka nambari ya kampuni ni 111333. Halafu unaweka namba ya kumbukumbu ya malipo ambayo ni namba yako mtuma fedha, halafu unaweka kiasi unachochangia , kisha nambari yako ya siri na unathibitisha mualamala kwa kubonyeza 1.

MITANDAO MINGINE
Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 kila ujumbe ni shilingi 500 tuma ujumbe nyingi uwezavyo kwa kadiri ya kiasi cha fedha ulichokusidia kuchangia M4C


CHANGIA MOVEMENT FOR CHANGE

KUTOKA ENEO LA TUKIO:


Timu ya Star TV ishafika na vifaa vyao, wanafunga Dish la kurusha matangazo na kutandaza Nyaya hapa SERENA HOTEL


Keep hooked for more UPDATES

UPDATES:
Namba za Kuchangia zitatangazwa moja kwa moja wakati wa kurushwa Matangazo hayo. Watanzania wapenda mabadiliko mtaarifiwa namna ya kufanya ili kuhakikisha mnaeza kuchangia kwa kiasi chochote kuanzia shilingi mia tano hadi ukomo wa nafasi yako katika kuunga mkono kampeni hizi.

Namba za kutuma Pesa Kupitia Simu ya Kiganjani
Taratibu zinawekwa sawa kuhakikisha hakuna hujuma yoyote na zitatolewa kunako majira ya saa moja jioni ya leo. Vuteni subira na msikose kutazama Star TV na pia thread hii kwa UPDATES

Tahadhari:
VODACOM msifanye yale yaliyojitokeza Arusha kwa kuzifanya namba hizi kuwa busy na huduma ya MPESA kushindikana kwa wakati huo.

ADIOS
 
Mkuu tupiea basi link kwa ambao tuko mbali na Star TV. M4C for life.......
 
Duuh mimi binafsi nilikuwa namkubali sana ZITTO ila siku hizi imani yangu kwake inazidi kupungua tu yaani sijui hata kwa nini.......
 
tumesikia ccm wanafanya hujuma ili makampuni ya simu yasiweze kufanikisha,mwisho wenu upo karibu kuliko mnavyofikiri
 
Mwaka huu magamba mavi yanagonga chupi'yanarudi tena ndani....yanagonga tena'yanarudi. mtaisoma mwaka huu
 
Peoples.........................................!
Power...........................................!
 
Mkutano unaanza saa ngapi na kila mtu anaruhusiwa kuja au inakuwaje ndugu, tuambieni jamani sisi tunataka kuja hivyo tujue mapema

Unaanza saa tatu, ninavyo jua huwa na kiingilio ambacho ndicho mchango wako kwa Arusha ilikuwa 200,000...
 
Huo ni mradi uliasisiwa ili kumuwezesha Lema aishi mjini.
 
Mbona nilisikia kwamba zile Posho zinachukuliwa na viongozi ili kuiwezesha M4C... Hivi wabunge wetu wanazitumia vipi fedha zao ya posho za kukaa (sitting allowance) ambazo hawakutaka kuzichukua..
 
Bar na guest house zitaongezeka kama uyoga zikipatikana hizo hela maana jamaa zetu wa mlimani ndio biashara zao kubwa.
 
Mbona nilisikia kwamba zile Posho zinachukuliwa na viongozi ili kuiwezesha M4C... Hivi wabunge wetu wanazitumia vipi fedha zao ya posho za kukaa (sitting allowance) ambazo hawakutaka kuzichukua..

Utaratibu wakuhudhuria unakwenda vipi
 
Back
Top Bottom