Elections 2010 LIVE ON TV: Kikwete ashinda kuwa rais kwa 61.17%

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,695
Tayari Wagombea wote akiwepo JK wameshawasili.

Dr. Wibroad Slaa bado hajawasili:

==================

UPDATES:


MATOKEO YAANZA KUTANGAZWA KAMA IFUATAVYO:

WALIOJIANDIKISHA: 20,137,303

Waliopiga kura 8,626,283 = 42.84%

Kura zilizoharibika 227,889 = 2.64%

Mgawanyo wa kura ni hivi:

APPT: 96,933 = 1.12%
CCM: 5,276,827 = 61.17%
CHADEMA: 2,271,941 = 26.34%
CUF: 695,667 = 8.06%
NCCR: 26,388 = 0.31%
TLP: 17,482 = 0.20%
UPDP: 13,176 = 0.15%

PICHA ZA MATUKIO:
Kikwete_Makame.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame amkikabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Kikwete_Certified.jpg

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha cheti cha ushindi katika mbio za urais mwaka 2010 muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010
Kikwete_Mkapa_Warioba.jpg

Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kutmangaza Rais Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo mchana
Kikwete_Lipumba.jpg

Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza Dr.Jakaya Kikwete kuwa mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010
 
afadhali asiende, watu watakatana mapanga mwaka huu......Mwanakijiji, quote me again.
 
Slaa hana haja ya kwenda hapo. Akienda ataonekana msanii. Safi sana , message sent...
 
Ridhiwani Kikwete kapiga kaznzu yake safi kabisa. JK kapiga green. Lipumba shati ya kitenge. Alivaa siku ya kupiga kura kama sikosei.
 
Yeah SLAA asiende hapo awaache hivyo hivyo then hapo sasa ndio mambo yanaanza
 
Kiravu anaongea sasa na anawashukuru waliohudhuria. Anamkaribisha Judge Lewis Makame.
 
Lewis anaanza kuwashukuru wote. Anasoma. Aanarefer katiba na sheria ya uchaguzi kuhusiana na zoezi zima
 
J Je in Busara kwa Dr Slaa kutohudhuria hafla ya kukamilisha kutangazwa kwa matokeo ya mwisho na mshindi wa mbio za kumtafuta Rais wa TZ 2010?????
 
Anasema kwa kuzingatia sheria majibu ya Ubunge na udiwani yameshatangazwa ila Urais
 
Ridhiwani Kikwete kapiga kaznzu yake safi kabisa. JK kapiga green. Lipumba shati ya kitenge. Alivaa siku ya kupiga kura kama sikosei.

Lipumba na Seif ni matawi la CCM. CUF bado hawajashtuka.
 
Kipenzi cha wengi, Dr Slaa hajatokea kwenye tafrija ya kutangaza matokeo ya urais.
 
Naona pia mabalozi wamealikwa. Kijani kibao. Makamba ndani ya nyumba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom