Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

Status
Not open for further replies.
Hebu tupe ushahidi.

attachment.php
 
Nikombali na tv ivyo ningependa coverage yako, lakini sikuamini kutokakana na michango yako hapa jf. You are not neutral.

mkuu pole sana na samahani kwa kukukwaza... Mimi huwa niko objective, nina tabia ya kuusema ukweli hata kama ni mchungu.. Simuogopi mtu wala siogopi kuusema ukweli hata kama unauma..nakushauri tuungane katika kuijenga nchi yetu kwa misingi ya umoja, mshikamano na upendo daima..pale ulipokwazka na michango yangu ni kwa sababu ya ukweli wangu..
 
Nilifikiri alikuwa hayaoni wala kusikia haya yahusuyo dini kumbe alikuwa anayajua haswa.

Alivyokuwa ananyamaza muda wote mpal uharibu wa mali, vurugu, watu kuuawa alikuwa anamaanisha nini? Au alikuwa anataka kuona mtu akiuwawa inakuwaje?
Anaacha kushughulikia serious matter anabaki kufanya Propaganda za kina Mwigulu + kuuza nchi kwa watu wa nje(Asia, Ulaya, Amerika).
Nchi imemshinda akae pembeni.
 
Hongera JK umewafahamisha hawa watu ambao hawaitakii mema nchi yetu.
 
Nilitarajia kama rais mwenye maamuzi ya mwisho pamoja na maelezo ya utangulizi kwa kila jambo angehitisha namna hii.

1. Tatizo la kuchinja kuanzia leo uchinjaji ni ........... na atakaye kwenda kinyume na hivyo ata.......

2. Tatizo la uchochezi hasa wa kidin kuanzia leo ..........atakayepatika anahubili kwa misingi ya ........ achukuliwe hatua .....atakaekamatwa na kanda, dvd, cd, vcd nk za uchochezi mara moja a.........atakayebainika kutengeza na kusabaza vitu hivi mara moja ......

3. Kuhusu uchomaji wa makanisa kuanzia leo mkowa au eneo uhalifu huu ukitokea ndani ya muda flani wahalifu wawe wamepatikana bila hivyo mkuu wa mkowa, Rpc na afisa upelelezi mkowa waachie ngazi mara moja kwa uzembe.

4. tatizo la kushuka kwa elimu pamoja na ............ mwisho wahusika wajitathimi kama wanafaa kuendelea kubakia wizarani .......maana taifa lolote linasimama kupitia elimu.

5. Kuhusu vyombo vya habari na wamiliki wake...........



Cha ajabu kikwete ameporomoa story kama muuza kahawa asiye na maamuzi wala mamlaka ilimradi anawaburudisha wateja wake kahawa yake iendelee kunyweka.

Nasikitika upuuzi wa uchochezi, upuuzi wa kogombea kuchinja, nk vitaendelea maadamu mwenye nyumba bado amelala fofofo na hana cha kumua na hatua za kudhibiti ujinga huu.
 
Mpumbavu tu ndiye atakayekataa serikali ya CCM chini ya Kikwete inahusiska moja kwa moja na haya yanayoendelea nchini

wewe kifua chako kimejaa chuki na husuda uliyopandikizwa na wajinga wenzako huko ndio mana unaendekeza mambo ya kijinga..hili taifa linakutegemea na linategemea mchango wako.. Amani ya tanzania inategemewa kuwepo kwa mchango wako lakini kwa jinsi unavyoonekana, wewe ni adui wa tanzania
 
nmeisilkiliza hii hotuba jk ametumia muda wote kulalamika na kujisafisha tu.
 
Mkuu alianza na ziara ya raisi wa CHINA, akaja na JENGO kuanguka and then Ishu ya UDINI. Mimi nimeona kaongea vizuri sana kwenye hoja ya UDINI na hasa ya kuchinja. Amefanya analysis moja nzuri sana, kwamba hivi tukiruhusu kuwa kuwe na mabucha ya wakristo na waislamu itakuwaje kwenye Restaurant? Hotel? Mama/Baba Ntilie nk. Je itakuwaje kwenye Harusi, Misiba nk? Nadhani inapaswa kufikiri kwa kina kwenye hili. Moja ya vitu vinavyokwenda kuangamiza taifa letu si mfumo UKRISTO wala UISLAMU nchini. Hili la kuchinja ndio linakwenda kutugawa kabisa na kutumaliza.

Hoja ya ziara ya raisi wa CHINA ameshindwa kutueleza faida za maana sana tunazokwenda kuzipata, na ishu ya majengo namuomba akajipange sana, maana hakuna shaka kuna uzembe na kulea uzembe kwenye halmashauri zetu. Haiwezekani jengo linanyanyuka bila wahusika kufahamu.
 
wewe kifua chako kimejaa chuki na husuda uliyopandikizwa na wajinga wenzako huko ndio mana unaendekeza mambo ya kijinga..hili taifa linakutegemea na linategemea mchango wako.. Amani ya tanzania inategemewa kuwepo kwa mchango wako lakini kwa jinsi unavyoonekana, wewe ni adui wa tanzania

tena adui namba 1 ukiachilia ujinga.
 
Ndugu wanajamii katika hotuba yake ya Mwisho wa mwezi akiongelea juu ya mgogoro wa udini na zaidi akielezea juu ya mgogoro wa uchichaji mh. rais ahoji mbona kuna mabucha ya nguruwe watu hawapigani.?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom