Live on Star TV: Tutanufaikaje na Uchimbaji wa Gesi, Urani na Mafuta?

In order to move ahead and succeed do what the rich are/have doing/done (legally, that is). There is a need to learn from whoever has done it well and has made oil & gas work for their countries. Case in point: the Emirates. We should learn to avoid the so called "Dutch disease" plaguing other Afrikan countries e.g. Equatorial Guinea, Nigeria, etc.

In minerals we should learn from South and Latin American countries and even Botswana where the royalties are as high as 18% on total revenues and not on profits that we have here in Tanzania!
 
Swali kwa mhe Kabwe.tueleze kwa uwazi Tanzania inapata asilimia ngapi? Ya kodi kutoka migodini? Na je? Migodi yetu inachimba madini kiasi gani?. Kwa mwezi
 
Swali kwa Zitto:

Kwa kuwa kwenye m4c ya CHADEMA hajashiriki na sababu za kutoshiriki hajatuambia na kwa vile ametangaza kugombea urais kupitia chadema na maneno yamekuwa mengi atolee ufafanuzi haya.

1. Kwa vile wao CHADEMA ni wachache bungeni na sauti zao zinasikika sana nje kuliko ndani ya bunge haoni kuwa ni muda muafaka kuweka nguvu zaidi nje ya bunge?
2. Kwa kuwa wote mnakubaliana kuwa rasilimali za taifa ni lazima zimnufaishe kwanza mtanzania huoni ni muda muafaka mkashauriana ndani ya chadema na kuachana na wimbo wa mafisadi kwani umekuwa wa kawaida masikioni mwa wananchi?
3. Huoni ni muda muafaka wa kuachana na M4C na kuja na 'Operesheni okoa mali za taifa' na wewe kuiongoza nchi nzima na kuwafungua wananchi masikio?
 
Last edited by a moderator:
Mh. Zitto

Unadhani sera,mipango na mikakati gani inaweza kunufaisha sehemu husika yenye madini au gesi .... je mgawanyo wa mapato yatokanayo na uchimbwaji wa rasilimali madini ni sahihi kuwa sawa sawa na sehemu zisizo na madini lakini labda zina zalisha mazao ambayo directly yanawanufaisha walio maeneo hayo ?
 
Star tv Mbeya haipo hewani. Ni mara nyingi inakatika Inakera sisi wana Mbeya kukosa vipindi muhimu kwa taifa kama hivi!
 
Mhe Kabwe, muda wa kulalamika umekwisha tufanye kazi sasa, madini tumeibiwa sana sasa gas na mafuta wanataka waanze kuiba.

Tuamke na kufanya maamuzi mazito,mhe Zitto wewe una uwezo mkubwa wa kuongoza na kujenga hoja na kuelewa mambo hata urais unaweza japo nina shaka na uaminifu kwenye pesa, lakini bado we ni mtu muhimu sana plz anzisha chama chenye mtazamo na sura ya kitaifa ambacho kitalenga kuweka viongizi wazalendo madarakani.

Kaka sajili chama kwa uwazi weka katiba makini si ku-paste za CCM na CHADEMA na sisi vijana wazalendo tutakuunga mkono ila take from ndani ya chama chako hakuna ukombozi wa dhati, tunaibiwa sana hiyo gas na mafuta yetu.
 
Swali kwa mhe Kabwe:

Tueleze kwa uwazi Tanzania inapata asilimia ngapi ya kodi kutoka migodini? Na je? Migodi yetu inachimba madini kiasi gani?
 
Swali kwa mh Zitto
Kama hakuna sera za gesi, kwa nini tuna kimbilia kwenye uchimbaji? Kutokuwa na sera hauwezi kuwa mwanya wa ufisadi kwenye rasilimsli hii?
 
Mkuu yahya,
mwambieni zito akome kutamka "wananchi wetu"
yeye au wao hawana wananchi, wao ni wananchi wenzetu.
 
Kunufaika na gesi ni ndoto za mchana kwani si wananchi wala viongozi wanaojua ni jinsi gani ya kufanya hiyo biashara. Zaidi ni kuingia mikataba aliyoandaa mwekezaji kuna kutoka hapo? Tumelizwa kwenye madini hapo itashindikana nini.
 
Yahya, mizunguko ni mirefu sana,
hili jambo la maliasili hasa zilizo tangible, zinapaswa kuwekwa kwenye formula.
Iwe ni lazima, kwa mali tutakayomshirikisha mbia thamani yake iwe 75% na mbia apate 25% hii ndiyo iwe muhimili wa mikataba. Na ijiweke wazi kuwa ikibainika mkataba umesainiwa bila kuzingatia asilimia hizo hapo juu, atakayepata hasara kwa matokeo ya kuvunja mkataba awe muwekezaji, hatuko tayari kuibiwa.
 
Back
Top Bottom