Live on STAR TV: tuongee asubuhi mada, jicho letu ndani ya habari.

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,739
744
Wadau habari za asubuhi:
Kipindi cha tuongee asubuhi kipo hewani sasa, mada jicho letu ndani ya habari.
Wanajadili namna vyombo vya habari vilivyo report vulugu za mbagala na Zanzibar. Je vyombo vya habari vimekidhi haja na kiu ya wasomaji na wasikilizaji na weledi wa uandishi wa habari.
Dotto Bulendu hajatushirikisha jukwa la wenye akili anawashirikisha fb.
Hatunyimwi kujadili kwa faida yetu.
 
Limezungumziwa suala la kuwepo kwa redio za Kikristu kuushambulia uisilamu, na pia redio ya kiisilamu kuishambuliwa Ukristu. Kazinja amesema kuwa watendaji walio chini ya Rais wanasubiri nini kuchukua hatua badala ya kusubiri tamko la rais? Jibu ni kwamba, huenda walio chini ya Rais (Waziri wa Habari, TCRA) wanaweza kuwa wanataka wachukue uamuzi lakini wanaogopa kwa kuwa huenda dini inayochukuliwa hatua ni ya bosi wao (rais), na wanaogopa kugusa maslahi yake!
 
Wa MAFIATI MBEYA.NDIYO NI KWELI KABISA KUNA RADIO NA TV ZIMEJIACHIA KUTANGAZA UDINI KILA KUKICHA NA SERIKALI KUTO CHUKUA HATUA YOYOTE INA MAANA KWAMBA SERIKALI INAKUBALIANA NA KITAKACHO TOKEA BAADAYE."DALILI YA MVUA NI MAWINGU" MOLA TUNUSURU NA CHUKI ZA KIDINI.ASANTE 'STARTV' MUNGU AWAONGOZE KATIKA KUTUELIMISHA KILA IITWAPO LEO.
 
Kweli udhaifu ni kitu kibaya sana. Kwa nini inashindwa kutolewa order ya dini moja kutokashifu dini nyingine?? Mfano hai ni kijiwe kilichopo pale Manzese n.k. Tunayoyaona yoote ni matokeo ya kufumbia haya.
 
jaribuni kutumia wachambuzi mbali mbali kila siku ni hao hao mwishowake tutatafsiri kuwa ni propaganda ya chombo chenu
 
Naona Dar es slaam James Range amefeli, ameshindwa kabisa kubalance mjadala, Propaganda zaid hakuna michango ya maana

hasa Falajala anapotosha na kugeuka msemaji na mtetezi wa serikali.

Bulendu amejitahidi kubalance mjadala Big up.
 
Back
Top Bottom