Live on Star TV: Mkuu Maxence Melo wa JF, yuko live ndani ya Jicho Letu Ndani ya Habari, JF ikiwa ndie mtoaji mkuu wa habari Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi



Tuko Live on Star TV, Mkuu Maxcence Mello wa JF, Yuko Live Ndani ya Jicho Letu Ndani ya Habari, JF Ikiwa Ndie Mtoaji Mkuu wa Habari Tanzania, Msikilize Max

May 30, 2020
MAMBO AMBAYO WAANDISHI & VYOMBO VYA HABARI WANAPASWA KUZINGATIA KUANZIA SASA KUELEKEA UCHAGUZI 2020.


Source: StarTV Habari

May 30, 2020
JAMIIFORUM HAITUKANI MTU INAFUATA SERA YAKE KIKAMILIFU - MAXENCE MELO.
Mkurugenzi JamiiForums akimjibu Paschal Mayalla kuhusu baadhi ya wadau kudai watu / viongozi wanatukanwa JF - JamiiForums vigezo, masharti , sera zake (policy) na maudhui ya mtandaoni hufuatwa na ndiyo mtandao unaojaribu kufuata kwa kiasi kikubwa taratibu zilizowekwa.


Viongozi wakubali maoni toka kila pande bila kujali maoni hayo hawayapendi, kukubali kukosolewa na siyo kutaka kusifiwa huku wamekosea.
Source : Startv Habari


Paskali
 
Pasco ametangaza rasmi kupitia kampuni yake kuwa yeye anamuunga mkono Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi wa 2020.

Hivyo wadau msishangae hoja za Pascal kuelekea 2020, msiseme amenunuliwa Ila mjue ndio msimamo wake.

2015 alikuwa na Lowasa, 2020 anaenda na Magufuli...

Tunashukuru kwa kuliweka wazi hili, nadhani zile kauli za kusema umenunuliwa sio tu zitakoma bali zitaisha kabisa...

Zile ofisi zako pale Posta nadhani utawezeshwa na utalipia pango, zile tenda za serikali zilizokata bila shaka sasa zitamiminika.

Hongera umeona mbali, njaa haina baunsa.
 
Wanabodi



Tuko Live on Star TV, Mkuu Maxcence Mello wa JF, Yuko Live Ndani ya Jicho Letu Ndani ya Habari, JF Ikiwa Ndie Mtoaji Mkuu wa Habari Tanzania, Msikilize Max

Paskali

asante mkuu.

mkuu @Maxcence Mello, nimebarikiwa sana na nondo zako. it just goes on to prove that JF is a top top top forum never seen on this continent before.
 
@Maxcence Melo hili jambo la media kutokutegemea ufadhili au upendeleo, kwa sasa naona ni jamiiforum pekee ndio tunayoiamini.

Vyombo vingi vimeshazimwa na sasa imebaki watu kuangalia upepo unaendaje.
Na kama alovyosema pasco waandishi pekee ndio wakulisemea hili sasa je ni akina nani wenye ujasiri huo kwa sasa?.

Kwa asilimia kubwa tunaona ni jamiiforum na yule jamaa wa twitter anajipatia umaarufu zaidi hasa uelekeo wa uchaguzi huu utampaisha zaidi.

pasco umeweka wazi uchaguzi huu unamuunga nani na hapo nyuma uliitwa kwenye kamati ya maadili kule bungeni mara baada ya kutoka kule ulipunguza sana ujasiri wako japo huwa umebaki kuuweka ujasiri huo kwa "code".

Je tunawaandishi wanaweza kuwa majasiri kama Mohamed Ally wa jicho pevu hapo Kenya wa citizen kama sikosei ( kama sio sahihi mtanirekebisha hapo).

Mimi naona kwa kiasi fulani media nyingi "malaika" mzima switch alishaweka kidole chake na anafanya lolote atakalo na wale waendesha vipindi wamebaki kusifia kila pambio ila kuna mengine watu hawataki kuyafanyia kazi kama nilivyosema hapo juu investigation journalism hatuna nchi hii na tumebaki na JF ndio inaweza kutoa hayo kwa watu wachache wenye ujasiri.

Tunaomba sana na uchaguzi huu @Maxcence Melo yasijirudie yale ya 2015 JF kuwa down.
 
Wanabodi



Tuko Live on Star TV, Mkuu Maxcence Mello wa JF, Yuko Live Ndani ya Jicho Letu Ndani ya Habari, JF Ikiwa Ndie Mtoaji Mkuu wa Habari Tanzania, Msikilize Max

Paskali
Tunapenda sana kumsikiliza lkn tatizo kwetu ni hicho kituo na waandaaji ukiwemo wewe
 
Back
Top Bottom