Live on Star TV: Mkuu Maxence Melo wa JF, yuko live ndani ya Jicho Letu Ndani ya Habari, JF ikiwa ndie mtoaji mkuu wa habari Tanzania

May 30, 2020
JAMIIFORUM HAITUKANI MTU INAFUATA SERA YAKE KIKAMILIFU - MAXENCE MELO.
Mkurugenzi JamiiForums akimjibu Paschal Mayalla kuhusu baadhi ya wadau kudai watu / viongozi wanatukanwa JF - JamiiForums vigezo, masharti , sera zake (policy) na maudhui ya mtandaoni hufuatwa na ndiyo mtandao unaojaribu kufuata kwa kiasi kikubwa taratibu zilizowekwa.


Viongozi wakubali maoni toka kila pande bila kujali maoni hayo hawayapendi, kukubali kukosolewa na siyo kutaka kusifiwa huku wamekosea.
Source : Startv Habari
 
Pasco ametangaza rasmi kupitia kampuni yake kuwa yeye anamuunga mkono Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi wa 2020.

Hivyo wadau msishangae hoja za Pascal kuelekea 2020, msiseme amenunuliwa Ila mjue ndio msimamo wake.

2015 alikuwa na Lowasa, 2020 anaenda na Magufuli...

Tunashukuru kwa kuliweka wazi hili, nadhani zile kauli za kusema umenunuliwa sio tu zitakoma bali zitaisha kabisa...

Zile ofisi zako pale Posta nadhani utawezeshwa na utalipia pango, zile tenda za serikali zilizokata bila shaka sasa zitamiminika.

Hongera umeona mbali, njaa haina baunsa.
Mayalla amefanya vyema kujiongeza maana zile tenda zilikuwa zinampatia mamilioni ya kutosha.

Hongera Mayalla..👏👏👏
 
May 30, 2020
MAMBO AMBAYO WAANDISHI & VYOMBO VYA HABARI WANAPASWA KUZINGATIA KUANZIA SASA KUELEKEA UCHAGUZI 2020.


Source: StarTV Habari
Dotto Burendu ndiyo anaibeba hiyo tv, vinginevyo ingesha fungasha virago
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom