Live On Star TV: Kipindi maalum na TRA kuhusu mauzo na utoaji risiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Live On Star TV: Kipindi maalum na TRA kuhusu mauzo na utoaji risiti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Star TV, Jun 26, 2012.

 1. Star TV

  Star TV Verified User

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wana JF,

  Tunapenda kuwatangazia kwamba, usiku huu, kuanzia saa tatu na nusu mpaka saa nne na nusu (21:30 - 22:30 EAT) tutakuwa na kipindi cha moja kwa moja (LIVE) kwenye station yetu ya Star TV.

  Wageni wetu watakuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Tunapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wale wote wenye maswali ambayo yanahusiana na kodi na utoaji stakabadhi za mauzo (risiti) wayaandike kwenye uzi huu ili mtangazaji wetu apate kutuwakilishia pale itakapofaa ndani ya kipindi hiki.

  Aksanteni.
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Asanteni kwa taarifa
   
 3. Star TV

  Star TV Verified User

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muda si mrefu tutakuwa hewani na wageni wetu.
   
 4. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  MASWALI KUHUSU STAKABADHI ZA VAT.

  1. Kuna tofauti gani kati ya VAT on invoice na VAT on Receipts?
  2. Kuna baadhi ya makampuni wanatoa Invoice zisizo na VAT codes wasema wanatoa VAT receipt baada ya kupokea malipo Je hii ni sahihi?
  3. Kwa mfanya biashara ambae hajafanya mauzo yoyote kwa Mwezi mzima kwa mfumo huu wa VAT machine bado anahitajika kupeleka NIL report?
   
 5. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Mimi mfanyabiashara niliesajiliwa VAT ninayetumia mita za umeme na Maji zilizosalijiliwa kwa jina la Mwenye Jengo la biashara ninawezaje kudai makato ya VAT nilizolipa kwa huduma hizi?
   
 6. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  VAT sio kodi kwa mfanya biashara, Je mfanyabiashara ana kodi zipi moja kwa moja TRA na analipa kwa utaratibu na vigezo gani?
   
 7. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Star TV vipi!? kipindi hakipo tena?
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Star TV kipindi kipo au hakipo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Swali kwanini gharama za ukokotoaji zilizo wekwa kwenye website yao zinakuwa tofauti na gharama ambazo unakuja kutozwa baada ya kuagiza gari toka nje ambapo unajikuta wakutoza zaidi tofauti na gharamaulizozipata kwenye website zao.

  Swali la pili kila mtanzania anaponunua kitu chochote analipia na vat ya 18% ikiwa nusu tu ya wa tanzania wakifanya manunuzi ya shs 5000 kwa mwezi walipa vat ya sh 900 ambapo ni zaidi ya trilion moja kwa mwezi hizo hela zingine zinaensa wapi? au kunaudhaifu wa ukusanyaji wa kodi?
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Vipi kama biashara na malipo yanafanyika kwa simu tu (mpesa,tigopesa etc) suala la invoice au receipt linakuwaje? Mfano nanunua LUKU kwa mpesa nawezaje kupata receipt?
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Umuhimu wa stakabadhi kwenye maduka yetu ya mitaani ambao hawamo kwenye VAT; ni bidhaa gani ambazo zinahitaji stakabadhi na zipi hazihitaji stakabadhi?
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hili swali mi sijalielewa mkuu. Wanasoma maswali live?
   
 13. mwenyenguvu

  mwenyenguvu Senior Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  tunaambiwa kuwa TIN ni bure,mbana inakuwa shida sana kupata tin haswa zile tin za makampuni?
   
 14. Star TV

  Star TV Verified User

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wana JF, tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Tunapenda kuwaarifu kuwa kipindi hiki kitamalizika saa nne na dk 50 (22:50 EAT) badala ya 22:30 kama tulivyopanga awali kutokana na kipindi kuanza nje ya muda tuliokusudia awali.

  Aksanteni.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mkuu namaanisha kwenye maduka yetu ya mitaani ambayo hawajasajiliwa kwenye VAT tunanunua Mkate, Maziwa, Maji ya kunywa, Soda, Sigara, nako tunaitaji kuomba Stakabadhi.
   
 16. P

  Professa Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TRA inafanya juhudi gani kukabiliana na wafanyabiashara wenye vitabu viwili viwili? Pia inakuwaje wafanyabiashara wanakuwa na uwezo wa kukuuzia risiti peke yake (mfano ukiwa unataka uprove ofisini kuwa ulinunua kitu fulani unaweza tu ukaenda kwa mfanyabiashara na akakuuzia risiti empty yenye tin number) ?
   
 17. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  wanasoma live mkuu. Just tune star tv.
  CPA(T)
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Stakabadhi nyingi wanazotoa kwenye Bereau de Change zinakuwa hazieleweki tufahamisheni ni stakabadhi zipi ni sahihi.
   
 19. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Super market Nyingi na maduka mbalimbali wanatumia cash pay machine kutoa receipts, je na zenyewe zimeunganishwa kwenye mfumo VAT?
   
 20. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ngoja nikujibu:

  Invoice vat na receipt vat tofauti inakuja ktk utengenezaji, invoice mara nyingi ni computer made ambayo inapita kwenye esd, Receipt vat yenyewe ni receipt inayo toka kwenye etr so invoice ina detail nyingi kuliko receipt.

  - Kutoa invoice ambayo haijapita kwenye machine ni makosa, unapaswa ulipe then upewe fischalized invoice. sema tatizo lipo mfano upewe invoice ambayo imepita kwenye esd alafu usilipe wakati invoice ishaenda tra hilo tatizo ndio watu hawataki ndio maana wanafanya hayo makosa.

  - mwisho kama hakuna mauzo yoyote itabidi utume report yenye zero wao wanataka report kila siku.
   
Loading...