Live on STAR TV, jicho letu katika habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Live on STAR TV, jicho letu katika habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mupirocin, Aug 11, 2012.

 1. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dr Charles Kitima: kizazi chote kilichosoma bure ambacho kilionja neema ya baba wa Taifa akiwa na lengo kuu kuwa kije kuliendeleza hili Taifa sasa ndo wezi wakuu wa hili taifa. Malengo yao ni kuongeza ujinga katika taifa, kuendelea kuongoza wajinga kupitia mfumo mbovu wa elimu.

  My take:

  Dr Kitima i salute you ni kweli kabisa sisi tulionja kidogo harufu ya baba wa Taifa ndo sasa tumo humu Jf na ndio tunaolalamika sasa hiki kizazi ambacho hata Nyerere hakimjui ndo kwishnei. Pole taifa langu Tanzania. We are talking quantity rather than quality.

  Walimu ni wale waliofeli form 4 na 6 ili hawa wazalishe engineers na Drs hizi ni ndoto. Huyu mtu yeye mwenyewe alishindwa mitihani atawezaje kumfundisha ili apate division 1 wakati yeye alipata 4.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,946
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  CCM ni adui namba moja!
   
 3. mujungu

  mujungu Senior Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Doctor jibu swali la kizazi hicho kilichosoma enzi za mwalimu ni wezi.
   
 4. Pangaea

  Pangaea JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  La kuhusu walimu na jinsi taaluma yenyewe ilivyochakachuliwa sijui ni nani mwenye div.I,II atapenda kuwa mwalimu.Lakini tusisahau hao hao waliopata div. I, II ndio waliopo katika nafasi za maamuzi na ndio wanaopeleka div IV na III ualimu.

  Mwisho tusisahau zipo sababu nyingi zinazosababisha wanafunzi wasipate div I,II [rejea changamoto za elimu] hivyo kupata div IV au III hainamaana moja kwa moja kuwa mtu huyo hana uwezo kiakili tatizo ni fursa katika mfumo wetu wa elimu.
   
 5. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hakuna kitu kibaya kwa nchi yenye raslimali nyingi kama Tanzania kukaliwa na Watu ambao hawana elimu.
  Katika Mazingira ya kawaida ilitegemewa Tanzania ndiyo iwe mfano wa kila kitu katika eneo zima la Afrika Mashariki lakini badala yake ni kinyume chake.

  Nadhani huko mbeleni Taifa hili litaingia matatani kutoka na Mataifa mengine kutamani Raslimali za Taifa ambazo zitakuwa zinamilikiwa na watu wasio na uwezo wa kuziendeleza hata kuangalia hali ilivyo sasa hivi dalili hizo zi wazi.

  Tumewashuhudia baadhi ya viongozi wetu wakishirikiana na Wajanja wa nje wakianza kupora Mali za Taifa hili kama inavyojidhihirisha katika kashifa ya Rada,Meremeta,EPA,Richmond n.k.
   
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Kuongozwa na mtu mjinga by itself ni hatari mbaya.Achilia mbali Ukubwa wa Jamii husika.Mtu mjinga aiyeona hatari ya mambo kabla ya kutokea, akiongezewa na kiburi na misimambo ni hatari.

  -Hujawahi shangaa polisi wakipiga watu virungu nya kichwa?Hujaona polisi wakidhalilisha wanasiasa wa upinzani bila kujijua kuwa wanaweza ingia madarakani siku yoyote?

  -Hujawahi jiuliza na kuona hatari ya viongozi kuwahi wauzia wageni rasilimali zetu kwa bei chee huku wakiwapa mikataba mirefu?Mbaya ni kwambta maeneo mengine wanayowapa yana rasilimali nyingine zilizopaswa kuwa na mikataba tofauti , au hata kuwa na uangalifu wa hali ya juu kuligusa.Mfano wanampa mtu kitalu ch akuwinda bila kujua kuna Uranium ya kumwaga matokokeo yake jamaa naye anatengenza mamilioni ya hela kwa kumptaia mtu mwingine.Na yote haya yanafanyika kimagendo na kuhatarisha dunia pamoja na mahusiano yetu na jumuia ya kimataifa inayotihatarishwa na uuzaji wa sialha haramu.

  Hujawahi jiuliza uzembe na ujinga wa manesi hospital, na mahusiano mabovu kati yao na madaktari katika kufanya maamuzi na hatari iliyopo kwa uahai wa raia na uchumi wa nchi.?

  Hayo ni baadhi ya mamabo yanayofanya wataalamu waone kuwa binadamua mjinga ni hatari sana kuliko kitu chochote.Na mbaya zaidi akipata mamlaka na akipata jamii ya wajinga ndio mbaya kabisa.
   
Loading...