LIVE:Nape na Kinana wavamia Geita,wanaunguruma uwanja wa Kalangalala

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
1,195
Wakuu wa JF:

Katibu Mkuu wa CCM Abdulhaman Kinana na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nauye hivi sasa wako kwenye uwanja wa Kalangalala mjini Geita wakiwahutubia wananchi wa wilaya ya Geita na Mkoa mzima kwa ujumla,wamingia asubuhi kwa ndege na dhumuni la ziara yao ni kuhakikisha kwamba wanaimarisha mashina ya chama hicho.

Nitaendelea kuwajuza kwa sababu baada ya dakika chache wataanza kupikezana kwenye jukwaa.

UPDATES:

KINANA:-CCM ya sasa imezaliwa upya na inarudi kwenye enzi zake wakati wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere,
:-Ni lazima CCM ihakikishe kwamba inawasimamia watendaji wa serikali ili kuhakikisha kwamba ahadi zilizoahidiwa na chama,
hicho zinatekelezeka ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maendeleo.
:-Watendaji wanaofuja fedha za serikali kukiona na kuanzia sasa mtumishi yeyote atakayebainika kula fedha za maendeleo,
ya wananchi hatahamishiwa mahali pengine atashughulikiwa na kuachwa hapohapo.

NAPE:Wanaodhani kwamba hizi ni nguvu za soda wasubiri tutakutana hukohuko na wajaribu waone,
:Haiwezekani chama kikatukanwa kwa sababu tu ya wajanja wachache ambao wanafanya kazi kwa utashi wao,
:Tuko kikazi zaidi na wanaodhani kwamba CCM haina meno sasa wajiandae kung'atwa na CCM.
 

Wingu

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,321
1,225
Hakika mwanzo mbaya wa Chadema kuelekea 2015.Kinana kazi yako wataipata tu.Hata Kibanda Ana kujua
 

SoNotorious

JF-Expert Member
Sep 11, 2011
2,420
1,195
huko geita najua tembo hakuna nawaomba kitu kimoja pana fisi wanakula watu huko na hivi karibuni kasi yao imezidi, muombeni kinana mbinu anazotumia kukamata na kuua tembo wetu azitumie kukamata na kuua hao fisi, msikubali aondoke bila kuwafanyia hilo, mchizi ana ability na potential hiyo komaeni nae hawezi kuwaangusha kabisha, mtaishi kwa amani ndo utakuwa mwisho wa fisi wala watu huko geita.
 

Prince Hope

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
2,160
1,225
ziara yenyewe haina jina wala agenda. acha wale hela za maboya.
Wakuu wa JF: Katibu Mkuu wa CCM Abdulhaman Kinana na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nauye hivi sasa wako kwenye uwanja wa Kalangalala mjini Geita wakiwahutubia wananchi wa wilaya ya Geita na Mkoa mzima kwa ujumla,wamingia asubuhi kwa ndege na dhumuni la ziara yao ni kuhakikisha kwamba wanaimarisha mashina ya chama hicho. Nitaendelea kuwajuza kwa sababu baada ya dakika chache wataanza kupikezana kwenye jukwaa.
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,606
0
Mkuu mbona unapotosha kwa makusudi dhumuni la ziara ya Kinana.
Madhumuni ya Ziara ya Kinana huko Geita ni kuonana na wananchi ili kutatua matatizo katika uchimbaji wa madini na wala sio kuimarisha mashina ya chama.
 

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Mbona hatupewi update tena,amesema nini? Au wananchi wamemfukuza wakidhani akikosa nyara za serikali atavamia nyara za wananchi kama mbuzi na kondoo?
 
Top Bottom