Live kutoka SAUT Mwanza mkitano wa hadhara wa kamanda Mbowe!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Messages
3,120
Points
2,000

mpk

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2012
3,120 2,000
Kulikuwa na mvua ndo imekatika, sasa kila kichochoro kinatema watu hapa uwanjani. Daladala pia zinashusha kutoka kila kona ya jiji hili.

Update kila baada ya muda mfupi!
Kuna nyimbo za kisukuma zinahamasisha sana, watu wamechangamka sana!

Updates: Sasa viongozi mbali mbali wa mkoa na madiwani wa jiji wanatoa nasaha zao.

Updates: Anaongea na mdogo wake Heche anaitwa Enock anasema akitoka Zitto wataingia makamanda 1000.

Amepanda kijana anaitwa Khalid anasema Ccm waache kuwafundisha waislamu kuitumia Qouran maana haikuwa na tofauti na azimio la Arusha, maana inasisitiza kuwajali wanyonge

Updatess: Pikipiki zaidi ya 100 na bendera za chama zinapita eneo la mkutano kuashiria kamanda anakaribia kuingia.

Updates: Anapanda kaka ya Charlse Tizeba (waziri) anasema yeye ni tofauti na Tizeba jambazi ambaye yuko chama cha majambazi!

Updates: Ameingia Kigaila wakati kuna Katibu wa Nyamagana anasema Ccm wanasema wana mwaziri mizigo na bado watanzania wanakubali kuongozwa na mizigo na siyo wao kuongoza mizigo

Updates: Amepanda Kamanda Mawazo anasema kama wahuni kama wa Kigoma wangetokea Mwanza wangepewa noma na kama wapo wajaribu. Anasema maskini wa Afrika kusini wanalilia mkombozi wao aliyewapa ardhi Tanzania wanaua wanyang'anyi wa ardhi.

Anasema hakuna atakayesaliti Chadema akapona hata Mbowe na Slaa

Anasema Kikwete atalaaniwa kwa kuhudhuria msiba wa mtu aliyepigania ardhi ya watu wake wakati yeye anauza ardhi kwa wazungu

Anasema Kapuya kumbaka mtoto siyo kesi lakini yeye akitongoza anakwenda magereza!

Updates: Ameingia Wenje akiongozana n Mh Mbasa wimbo wa kisukuma wa kuhamasisha unapigwa watu wanashangilia sana!

Updates: Wenje anasema kilichotokea kwa Mabina ni kuthibitisha kuwa maskini wakikosa chakula watakula matajiri na kuwa ilo liwe funzo kwa Meya feki Matata.

Anasema Yesu alikuwa na wanafunzi 12 lakini mmoja alimsaliti sembuse Chadema yenye wanachama mamilioni.

Anasema Zitto wakati wa kampeini alikataa kumpigia kampein akiwa Mwz na akasema Masha ni rafiki yake.

Anasema Zitto amewaambia mara nyingi kuwa Kikwete amemuokoa kwa kuwashawishi wabunge wa Ccm wampigie kura kwenye uenyekiti wa kamati.

Watu wanaimba Chadema inawezekana bila Zitto unaoongozwa na Mawzo!

Updates: Kamanda anaingia na msafara wa pikipiki zaidi ya 300 na magari mengi sana!

Amepanda jukwaani na kusema amechelewa kwa sababu amelazimika kukimbia Kilimanjaro kufanya kazi ya chama!

Anasema Ccm hawawezi kufanya mkutano kama huu kazi yao ni propaganda na kuchonganisha uongozi wa chama!

Anasema boti iko safarini anayejaribu kuutoboa atashugulikiwa, anawauliza wangapi wanataka awe legelege ili chama kife? Wananchi wanakataa

Anasema yeye au Slaa akihujumu chama atashughulikiwa na kamati kuu!

Wananchi wanasema Zitto asikanyage Mwz lakini mwenyekiti anakataa. Anasema wameanza udini, ukabira umeshindikana sasa ni kutuchonganisha!

Anasema C cm hawawezi kutununua kwa sababu Mbowe hana fedha lakini hana njaa na hivo hivo Dr Slaa na viongozi wengine waaminifu!

Anasema watu wamekufa mikononi mwake watu wanaleta za kuletwa tutaona kamasi!

Anauliza anayesema Mbowe ameharibu chama anyooshe mkono. Hakuna aliyenyoosha!

Anasema gazeti la Jambo leo ni gazeti la Riidhiwani lakini wanapeana matumaini ya upepo na waliofukuzwa kwenye chama. Amemaliza
 

KOMBAJR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Messages
5,833
Points
1,195

KOMBAJR

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2011
5,833 1,195
Kulikuwa na mvua ndo imekatika, sasa kila kichochoro kinatema watu hapa uwanjani. Daladala pia zinashusha kutoka kila kona ya jiji hili.

Update kila baada ya muda mfupi!
mkuu picha ndo sumu ya lumumba fc hata usipoweka maneno picha zinaongea
 

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Messages
3,396
Points
1,195

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2011
3,396 1,195
ZeMarcopolo; Bila shaka na ile sera ya Kuwadhibiti mafisadi na majangili wa tembo itaundwa bila kuisahau ile kampuni ya Kinana iliyosafirisha meno ya tembo kwenda nje ya nchi.
 

ambagae

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2009
Messages
1,652
Points
1,195

ambagae

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2009
1,652 1,195
Kulikuwa na mvua ndo imekatika, sasa kila kichochoro kinatema watu hapa uwanjani. Daladala pia zinashusha kutoka kila kona ya jiji hili.

Update kila baada ya muda mfupi!
Kuna nyimbo za kisukuma zinahamasisha sana, watu wamechangamka sana!
Mwongo wewe Mimi niko hapa mbona sioni unayodanganya Watu. Sema ukweli.
 

Apolinary

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Messages
4,436
Points
1,250

Apolinary

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2011
4,436 1,250
Kulikuwa na mvua ndo imekatika, sasa kila kichochoro kinatema watu hapa uwanjani. Daladala pia zinashusha kutoka kila kona ya jiji hili.

Update kila baada ya muda mfupi!
Kuna nyimbo za kisukuma zinahamasisha sana, watu wamechangamka sana!
kwa maana hio mkutano ulivunjika baada ya mvua kunyesha au?
 

Forum statistics

Threads 1,391,008
Members 528,343
Posts 34,070,032
Top