Live ITV kutoka UDSM: Kongamano la Tafakuri baada ya Uchaguzi Mkuu 2015

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Usikose kufuatilia Kongamano la tafakuri baada ya Uchaguzi Mkuu wa October 2015 kupitia ITV, CAPITAL TV watakuwepo Jaji Joseph Warioba na Prof. Issa Shivji itimiapo hapo saana nane kamili leo.

============

Updates:1500hrs

Kongamano linaendelea sasa, Wanazungumzia uchaguzi mkuu uliofanyika Tanzania 2015.
Ni kwa kiasi gani Uchaguzi huo umeacha misingi ya Utaifa, mshikamano, usawa na utu.

Vilevile wanaangaazia Ugharamiaji, Rushwa na Migawanyiko.
 
Linaendelea sasa hivi kwenye ukumbi wa blue pearl hotel Ubungo.
Nawaona mzee Warioba, profesa Palamagamba Kabudi na watu wengine maarufu.
=======

Kongamano linaongozwa na Issa Shivji na jaji Joseph Warioba
 
Ha ha haaaaa! hii kali yani wameamua hivyo baada ya kusikia kuna lingine Ubungo plaza ambalo litahusu mtazamo wa kisheria uchaguzi wa zanzibar ambao Fatma Karume atakuwa mmoja wa wazungumzaji
 
Mambo makuu ya ajabu yaliyojitokeza katika uchaguzi na kampeni zake 2015 ni pamoja na:-

1. Jaji Warioba kupanda jukwaani kuwapigia debe CCM

2. CDM kumpokea EL, mtu tunayejua kuwa ni fisadi kwa kipindi kirefu; ajenda kuu ya ufisadi ikapotezwa

3. Dr Slaa kuondoka kwenye chama chake pendwa, kuitwa msaliti baada ya kukataa nafasi yake ya kugombea urais kuchukuliwa na EL

4. Zitto Kabwe kuacha kumwachia Mama Mgwira madaraka ya Kiongozi Mkuu wa Chama kama alivyoahidi awali kwamba yeyeote atakayekuwa anagombea urais ndiye atakuwa Kiongozi Mkuu

5. Mgombea urais kupiga pushap jukwaani

6. Kuruhusu kura zibandikwe vituoni ila unazuia kuzijumlisha

Hayo ni baadhi ya mambo yamesababisha nione siasa zetu ni za mazingaombwe.
 
Linaendelea sasa hivi kwenye ukumbi wa blue pearl hotel Ubungo.
Nawaona mzee Warioba, profesa Palamagamba Kabudi na watu wengine maarufu.
=======

Kongamano linaongozwa na Issa Shivji na jaji Joseph Warioba




Chini ya uratibu wa hao uliowataja,sidhani kama kongamano hilo litakuwa na maana.Hao wote ni wachumia tumbo waliotelekeza Taaluma zao na kutumika kutetea udharimu.
 
S

Sasa nisikilize nini wakati najua yeye yupo na anapigia debe upande gani!Si alikuwa anampigia debe magufuli juzi tu hapa,nitegemee aongee nini labda?kuwa uchaguzi ulikuwa sio wa haki?Maalim seif apewe haki yake atangazwe?
Poa kama umegoma hamna noma
 
Nimependa mada ya Prof. Ayub Rioba kuhusu kazi nzuri ya vyombo vya habari na haswa wale waandishi mamluki, ambao ni mabingwa wa kutunga uongo na kuuandika vizuri na kwa umahiri zaidi hadi ukaonekana kama ni ukweli.

Pasco
 
Huyu Mzee Warioba alishapoteza haiba yake kisiasa ni bora angeungana na wenzie kina Six na wengine wafananao na yeye haaminiki tena huyu Mzee.
 
Huyu Mzee Warioba alishapoteza haiba yake kisiasa ni bora angeungana na wenzie kina Six na wengine wafananao na yeye haaminiki tena huyu Mzee.

Hata mimi siwezi kuwasha tv yangu na kuwaangalia hao watu. Kwangu mimi mtu kama mzee Warioba na wenzake akina Polepole walishanikatisha kabisa tamaa pale tu waliposhindwa kuipigania Katiba ya wananchi walio wengi badala yake wakakubali watemi wachache waifanye walivyotaka.
Hapa ni mwendo wa kuwasusia tu.
 
Back
Top Bottom