Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF;

Nimerejea baada ya safari ya takribani wiki mbili ili na mimi niweze kutumia vema haki yangu ya kupiga kura. Nikishapiga kura naondoka tena nikaendelee na harakati za maisha.

Nimesikia kutoka ITV kuwa watatuletea matangazo LIVE ya mchakato wote wa upigaji wa kura kutoka Studio zao mpya walizoziita Studio One (Masako na Nyangasa) na Studio Two (Gondwe). Nimeona mwonekano wa studio hizi umeboreshwa kama zile za watani wetu wa jadi. Bila ya shaka TBC1 na TV zingine nao watakuwa hewani.

Nami bila hiana nimeamua kwa hiari yangu kesho niwe mtumishi wenu. Nitaamka saa 10.30 alfajiri ili niwahi foleni ya kupiga kura na baada ya hapo nirejee kwenye laptop yangu kwa ajili ya kuwaletea kinachojiri toka nitakaporejea.

Najua wengi mtapata fursa ya kusikia matangazo, kwa hiyo tutasaidiana kuposti.

Natoa wito wote tuhamasishane kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi ambao watatutumikia katika kipindi cha miaka 5 ijayo.

Stay tuned!
 
Asante superman, nikumbushe vituo vinafunguliwa saa ngapi? nataka mikawe wa Kwanza Kesho
 
Asante superman, nikumbushe vituo vinafunguliwa saa ngapi? nataka mikawe wa Kwanza Kesho

Haaa haaa Mkuu nadhani ni saa 12. Ila nimesikia wengi mtaani kwetu watajidamka mapema ili wawahi. Biashara asubuhi Mkuu.

Tuko pamoja mkuu.
 
Haaa haaa Mkuu nadhani ni saa 12. Ila nimesikia wengi mtaani kwetu watajidamka mapema ili wawahi. Biashara asubuhi Mkuu.

Tuko pamoja mkuu.

Ngoja nikalale Mkuu ili kesho niwahi kuamka maana Kesho nina hati hati kama nitalala
 
Angalia pia kama Kadi ya Camera ina nafasi maana hizo Memory zisije zikajaa baada ya picha chache.

Kama unatumia Mkanda, basi nina imani umeshanunua. Kila la kheri na tunakusubiri kesho.
Tuko pamoja Mkuu. Umenikumbusha ngoja nicharge betri yake kabisa nitafute na stand yake nilipoihifadhi.
 
Angalia pia kama Kadi ya Camera ina nafasi maana hizo Memory zisije zikajaa baada ya picha chache.

Kama unatumia Mkanda, basi nina imani umeshanunua. Kila la kheri na tunakusubiri kesho.

Du! Kweli Mkuu. Ngoja nitoe picha zote ili iwe blank.

Bahati nimekuta shemeji yenu Generator kishaijaza mafuta. So JF kesho tuko vizuri kuleta yote yanayojiri bila kuchakachua.
 
Sasa Wakuu, ngoja mimi nipumzike halafu niwahi kufanya kazi kesho.

Hakuna jiwe litasilia juu ya jiwe. mambo yote hadharani. Nimemtahadharisha Shemeji yenu kuwa Breakfast, Lunch, Dinner vyote hapa. Hakuna wageni wanaruhusiwa. Watanzania wanatoa ajira kesho.

Usiku mwema.
 
Naam; hatimaye kumekucha!

Nimechelewa kidogo, lakini Mamaa ananihimiza tuwahi kupiga kura.

Niko na Camera mkononi, ndo tunaelekea. Nikirudi tutapashana yalijyojiri!
 
Sabalkheri wana jf wenzangu. Mwenzenu tayari niko mstarini nikisubiri kwenda kufanya kweli. Kuna nyomi la kufa mtu huku. Im super dupa excited
 
Naam; hatimaye kumekucha!

Nimechelewa kidogo, lakini Mamaa ananihimiza tuwahi kupiga kura.

Niko na Camera mkononi, ndo tunaelekea. Nikirudi tutapashana yalijyojiri!

Asante kwa kujitolea kuwa nasi nasubiria matukio muhimu
 
Sabalkheri wana jf wenzangu. Mwenzenu tayari niko mstarini nikisubiri kwenda kufanya kweli. Kuna nyomi la kufa mtu huku. Im super dupa excited

wats up dude.........kumbe ndio maana ulipotea namna hiyo..........show dem da real substance of life............
 
Sabalkheri wana jf wenzangu. Mwenzenu tayari niko mstarini nikisubiri kwenda kufanya kweli. Kuna nyomi la kufa mtu huku. Im super dupa excited

Na mimi ndiyo nimemaliza kunywa chai na sasa naelekea kupiga kura yangu. Toka nyumba yetu tuko watu watano na wote tunampigia Dr Slaa na wagombea ubunge/udiwani wa chadema. God Bless you Dr Slaa and all the best.
 
wats up dude.........kumbe ndio maana ulipotea namna hiyo..........show dem da real substance of life............

worry not my friend. Though the sky is a little overcast, this outstanding nyani son of ngabu is ready to mete out some raw justice in the form of takbiru ala walibalu
 
Naam wana JF nimesharejea.

Tuliondoka kama saa 11.45 asubuhi na tumerudi saa 1.45 asubuhi. Imetuchukua takribani masaa 2. Kituo chet hakika hakiko mbali na tunapoishi.

Nimepiga kura yangu kwa ajili ya kuwachagua madiwani, mabunge na Rais.

Nina mengi ya kuwaeleza, ungana nami katika posti zinazofuata.
 
37117_445360416155_687191155_6101302_6888355_n.jpg

Wanasubiri kutekeleza wajibu wao..
 
Back
Top Bottom