Live: DDC MLIMANI

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
156
nini lengo la upinzani na sera ya kukamata mtaji wa wanafunzi wa vyuo?
 
PROF Baregu anaelezea suala la utandawizi,ufisadi wa mwafrika,utandawizi maana yake ni
kupora mali za mwafrika
 
tundu LISSU ndio anaanza kumkoma nyani giladi asubuhi..
cha kushangaza hakuna waandishi wa habari..
mie natoka hapa,naenda kumfuata kada pale bungu plaza
 
nipo hapa ubungo plaza,mzee msekwa anaongea..vijana wa chama wanakula A/C tu,
nimeona utofauti mkubwa ..hapa wanafunzi ni mara mbili au tatu
 
mzee msekwa anaongelea dira ya chama,amekumbusha malengo aliyoyaweka mwalimu..
chama cha watu,chama cha wakulima na wafanyakazi..lazima kijali maisha na maslahi ya watu..
mzee msekwa ana busara,hapa kuna waandishi wa magazeti na TV
 
anakumbushia miiko ya uongozi iliyowekwa kipindi cha TANU,ambayo haikuruhusu kiongozi yeyote kuwa mkurugenzi wa kampuni yoyote,kuwa na hisa katika kampuni yoyote,kuwa na nyumba ya kupangisha..
 
Msekwa amekiri uchaguzi wa chama umeingiliwa na RUSHWA,ila amesema wao hawaikumbatii bali wanaipiga vita RUSHWA,amesema ni moja ya mipango yake..anarejea suala la sera ya TANU ambayo ilikuwa inakataza kiongozi yeyote kupatikana kwa hila,RUSHWA wala ujanja wowote..
 
kwi kwi kwi,
mie narudi kijini kwangu nikatazame watoto wangu..
 
mh Sikujua kama Zitto ni mpenda sifa...na JK naye kwa nini ateue wapenda sifa badala ya wachapa kazi wenye uchungu kweli na nchi hii? au ni Zitto mwingine anaongelewa hapa?
 
Katika Muda niliokuwa Tanzania, ni Politician mmoja tu niliyepata wassa wa kuzungumza naye 1o1. NI huyu Mzee Msekwa, na mengi niliweza kuzungumza naye kwa kina kiasi kwamba hata baadhi ndugu zangu walishangaa kwani haikuwa kawaida yake kabisa na wengine walinambia U are wasting your time - He is no body!. Yet, sikupuuza kulikuwa na kitu kilichonivuta kuendeleza mazungumzo.
Nilizungumza kero zangu na kwa kiasi fulani naona hizo kero zimechukua nafasi kubwa ya mwelekeo wake ktk kuijenga CCM.
Tatizo la Tanzania siku zote ni Utekelezaji - Mikutano inaweza fanyika kila siku na agenda nzito nzito lakini inapofikia Utekelezaji wake hapo ndipo ngoma kubwa...
 
Mkombozi ,acha uongo hukuwepo eneo la tukio.

Nitaweka ushahidi.

Engineer acha uongo ,zitto hakuvaa suti leo, ila shati jeusi na suruali ya khaki.

Ubungo hakukuwa na watu na hilo unaweza kuliulizia kwa waandishi wa tv waliokuwepo maeneo yote mawili.

Waandishi walikuwepo DDC na mkutano umekuwa wa kihistoria .

Ubungo nilikuwepo na hapa ndio naanda story ya kesho ,ngoja wakishachagua picha ya gazeti nyingine nitaiweka hapa.
 
Leo kama mnavyofahamu kulikuwa na makongamano ya wanafunzi jijini Dar-es-Salaam. Moja lilifanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuhutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Pius Msekwa na lile jingine lililofanyika Ukumbi wa DDC na kuhutubiwa na wasomi mbalimbali na viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo Mhe. Zitto Kabwe. Nilipata nafasi ya kutuma salamu za mshikamano kwa kongamano la DDC baada ya kuombwa kutuma ujumbe huko. Walioko nyumbani waliupata kwa njia ya maandishi, lakini hapa unaweza kuupata kwa kusikia.

Ujumbe wangu unaitwa: "Wasomi waongoze mapambano ya Kifikra".

M. M.

http://www.mwanakijiji.podomatic.com
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom