Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,446
- 16,301
Nakumbuka kipindi hiko tukiwa wadogo redio ndo zilikuwa njia kuu ya kupata taarifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa, kulikuw hamna runinga wala mitandao ya kijamii. Taarifa ya habari yenyew ni kwamba mnaisubiri kwa interval ya masaa kadhaa kwa siku, asubuhi mchana na usiku.
Baadae tukahama kutoka redio tukaenda kweny runinga, lakini nazo ni yaleyale tuu ya kusubiri taarifa za habari muda fulani na fulani. Runinga za wenzetu nchi za nje hawana mambo ya kulundika taarifa hizi eti waje wazisome baadae, wako online masaa yote na tukio likitokea linaripotiwa palepale kutoka scene ilipo.
Muda si muda tukaingia kwenye simu janja na kuna social medias za kumwaga. Sasa hapa ndipo penye ukakasi, kwa sasa watu wenye simu janja hawaoni umuhimu tena wa vipindi vya habari kwa kuwa matukio yoote ya siku nzima wanayapata pale yanapotokea tuu na sio kusubiri waje waangalie yalorekodiwa kwenye runinga.
Runinga kubwa kubwa kama CNN, AL-JAZEERA,SKY NEWS, BBC, AFP na hata media za majirani zetu Kenya hapo tuu wanafanya live coverage ya news. Hamna mambo ya kurekodi na kusubiri usiku mzioneshe.
Kwa hali hii vituo vyetu vya runinga vitaweza kushindana na kasi ya maendeleo ya teknolojia ya habari ambapo kila mtu anapata habari kiganjani?