Live Coverage..........KumeKucha DODOMA

Mimi napenda kupingana kidogo na baadhi ya wana JF walio changia thread hii kuwa, ripoti ya Mwakyembe haijasema wazi kuwa bwana EL awajibishwe!! Hebu someni vizuri pendekezo namba (16)ya kamati teule

''(16) Uhuru mkubwa ambao viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia bila wasiwasi katika kuhakikisha kwamba kampuni waliyoitaka, Richmond Development Company LLC, inapewa zabuni ya umeme wa dharura; maelekezo ya mara kwa mara ya Waziri Mkuu kwa Wizara katika kila hatua ya mchakato huo; upendeleo wa dhahiri ambao Richmond Development Company LLC iliupata kutoka taasisi mbalimbali za Serikali k.m Kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho kilifikia hatua ya kufumbia macho baadhi ya taratibu zake za msingi ili kuipa kampuni tanzu ya Richmond Development Company LLC cheti cha uwekezaji haraka iwezekanavyo; kutotimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria; uteuzi wa mwisho wa Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kufanywa na Waziri Mkuu mwenyewe tarehe 21 Juni 2006; uamuzi wa kuiteua Richmond Development Company LLC kuwa mkandarasi kusafishwa na TAKURU ( sasa TAKUKURU) kuwa ulikuwa wa wazi na wa haki; uamuzi wa Serikali kuizuia TANESCO isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote kisheria kuwepo, ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu ya Wizara ya Nishati na Madini kutumika katika suala hili na Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu.

Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge''

Mistari ya mwishono mwa hilo pendekezo linasema kwa maneno mengine, kutokana na kwamba PM ameshindwa kutekeleza majukumuu yake kama ilivyoainishwa katika ibara ya 52 ya katiba ya Jamhuri ya Tz ya 1977 basi AJIUZULU! Ripoti kwa meneno mengine inasema, kama atashindwa kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe na kwa faida ya taifa, basi Bunge ambalo kwa mujibu wa ibara ya 51 inayolitaka bunge kuthibitisha uteuzi wake, basi bunge hilo LIMUTHIBITISHE VINGINEVYO kwamba HAFAI!! Kwa maoni yangu ripoti imeonyesha wazi kabisa mapendekezo yake kiasi kwamba hata mtoto wa darasa la tano anajua what is supposed to be happening next regarding our EL na washirika wake.

Sisi tusubirie bunge linachukua hatua zipi na hao wote waliotajwa huko ndani wanafanya nini! Then, sisi wananchi tukiwa na umoja wa kweli tunaweza tukaamua kwa pamoja kama tunataka kundelea kuwa na hawa mafisadi au laa iwe leo au kesho!! Kwa sababu ninacho kiona mimi ni ''days are numbered''wamelihujumu sana taifa hili,watafanya kila aina ya ufisadi na udhalimu lakini nchi hii itabikia kuwa ya watanzania, kama ALAMA HIZI ZA NYAKATI ZINAVYO JIONYESHA....mafisadi wanafichuliwa, viongozi feki or mitumba wanajulikana na mambo mengi mengi tu......!!!

festog
 
Ngoma ya jana imeanza sasa. Sitta aja na sababu juu ya watoa hoja .Waziri Mkuu amesimama sasa kujibu hoja .
 
Lowasa asema Natural Justice haikufanya lolote na yeye amelalamika kwamba hakuitwa na yeye hakuitwa .So anadai hakutendewa haki na anasikitika sana mbele ya Bunge kwamba karukwa .Lowasa anasema hili ni jungu na anauliza kwa nini hakuitwa kuulizwa ? Lowasa anaanza kupangua ngoma .Duh kweli Tanzania usanii .
 
Ni kweli sasa nimeamini kwamba Lowasa ni msanii na kweli wamesha jiandaa vya kutosha hapa ngoma imelala hakuna wa kujiuzuru.Wamesha jipanga vya kutosha .
 
Masatu said:
Hii ripoti ya Mwakyembe ina mapungufu, kwanini hawakumhoji Lowassa wakati kwenye hitimisho wanadai ushahidi wa maandishi, kauli na mazingira una mhusisha kwa namna moja au nyingine?

..hivi itakuwaje kwa hawa watumishi wa serikali ambao walikuwa wanafuata maagizo/amri za wanasiasa?

..nimeona Dr.Mwakyembe amependekeza PS na Commisioner wizara ya Nishati wajiuzulu.

..Dr.Mwakyembe anamtuhumu Commisioner kwa kutokumshauri PS kuhusu uwezo wa Kifedha wa Richmond.

..Ukisoma ripori unaona kwamba Commisioner aliandika barua ya kuvunja mkataba wa Richmond wa kujenga bomba la mafuta. Commisioner aliandika barua hiyo kwa niaba ya PS.

..hivi inawezekana Commisioner akaandika barua kwa niaba ya PS bila kufanya mashauriano naye kwanza?

..Sasa inakuwaje PS asifahamu uwezo mdogo wa kifedha wa Richmond wakati wa mchakato wa tenda ya majenereta?

..vilevile Dr.Msabaha lazima alikuwa na taarifa za ukata waliokuwa nao Richmond. Yeye alikuwa Naibu waziri wakati Richmond waliposaini mkataba wa kujenga bomba la mafuta Dar-Mwanza.

..Kitu cha ajabu vilevile ni kitendo cha Mwanasheria Mkuu kutohudhuria vikao hivi. What was going on? Je, ilikuwa ni uvivu tu, au alikuwa hataki kuitwa ushahidi katika mradi huu?

..Nasubiri kwa hamu kubwa maelezo ya kina ya watuhumiwa wote.
 
kujiuluzi uwaziri haitoshi, wajiuzulu ubunge na uanasiasa, hawa wataendelea kuiba tuu mpaka lini?, masatu umeongea kweli, lakini waliambiwa wenye ushahidi waende mbona hakwenda?
 
Mbunge Ndesamburo alikuwa anasema Mafisadi wanastahili kunyongwa...naona TVT wametoa matangazo ya Bunge hewani..au ni Jumptv inaleta ujinga...
 
Back
Top Bottom