Live Coverage..........KumeKucha DODOMA

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Jul 27, 2007
452
7
Haya kumekucha jamani,baada ya jana pirika za kuipitia ripoti ya RICH-MONDULIS leo ni siku nyengine ya kuijadili.

Mliopo DODOMA tuleteeni DATA kunani HUKO?

Mheshimiwa Spika, kutokana na madai hayo ambayo hayakuwa na uthibitisho, Kamati ya Wataalamu ikaipendekeza Richmond Development Company LLC kuingia kwenye majadiliano ya mkataba na Serikali. Katika kuhalalisha ushindi huo wa Richmond Development Company LLC wajumbe wote wa Kamati hiyo ya wataalamu, Waziri wa Nishati na Madini aliyetangulia Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb), Waziri wa sasa wa Wizara hiyo, Mhe. Nazir Karamagi (Mb), Katibu Mkuu wake, Ndugu Arthur Mwakapugi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Johnson Mwanyika, (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ndugu Gray Mgonja na maafisa wote waandamizi wa Serikali na TANESCO waliotoa ushahidi mbele ya Kamati Teule, walitoa kauli zilizofanana mithili ya wimbo maarufu kuhusu sifa za Richmond Development Company LLC zilizoifanya ishinde, kuwa.....Mheshimiwa Spika, ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura, si lazima uwe ushahidi wa kwamba kiongozi huyo wa kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa staili yake ya kawaida kabisa ya uongozi katika kufuatilia masuala yote ya kitaifa kwa karibu sana tukizingatia kwamba nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme. Watu pekee waliokuwa wanaujua ukweli wenyewe, ukweli ambao ungeipa Kamati Teule msingi wa kumhoji Waziri Mkuu kwa kiapo, walikuwa watatu: Waziri Dk. Msabaha (Mb), Katibu Mkuu Mwakapugi na Mwenyekiti wa Bodi Balozi Kazaura.

Mheshimiwa Spika, Kamati Teule ikawaita kwa mara ya pili Dk. Msabaha (Mb) na Ndugu Mwakapugi kwa mahojiano zaidi. Wote wawili, wakiwa ndani ya kiapo, walikataa katakata kupokea maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu ya kuipa Richmond upendeleo. Lakini Mhe. Dk. Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaiuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo. Maelezo hayo ya ziada nje ya kiapo ya Mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa “si yeye ila mkuu wake wa kazi”, yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007. Mara baada ya kumaliza mahojiano kwa kiapo na Kamati Teule, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa “Bwana Mkubwa” na “mshiriki wake mkubwa kibiashara”, akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).
Mheshimiwa Spika, tumelazimika kueleza hata mambo tuliyoelezwa kwa siri kiungwana (in confidence) kutokana na uzito wa suala lenyewe na dhamana kubwa tuliyopewa na Bunge ya kuelezea kilichotokea kwa uwazi na ukweli. Lakini ushahidi huu wa ziada na nje ya kiapo wa viongozi hawa wawili, haukutoa msaada stahili kwa Kamati Teule kwa kuwa msingi wa maamuzi yote ya Bunge si minong’ono au tetesi, bali taarifa zenye uthibitisho halisi. Ni dhahiri kuwa, kwa watumishi hao “waaminifu” wa Serikali, isingelikuwa rahisi kumtaja Waziri Mkuu chini ya kiapo. Hatua hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu.Lunyungu,Halisi,Invisible mpira upo kwenu huo.

hili neno BANGUSILO maana yake nini?kama kuna wazaramo humu JF hebu watupe maana yake.
 
Hii ripoti ya Mwakyembe ina mapungufu, kwanini hawakumhoji Lowassa wakati kwenye hitimisho wanadai ushahidi wa maandishi, kauli na mazingira una mhusisha kwa namna moja au nyingine?

Hii habari ya kumpa waziri mkuu nafasi ya kupima mwenyewe uzito wa madai yaliyopo mbele yake na afanye uamuzi ni kumpa blank cheque na escaping route, kama ushahidi upo japo by implication kwanini wasishauri waziri mkuu nae awajibishwe?

Huu ukweli kuwa TAKUKURU waliisafisha Richmond ni ushahidi tosha kuwa waziri mkuu Lowasa ndie alieshinikiza hilo lifanyike haiingii akili cabinet member Msabaha au Karamagi aweze kuwa ushawishi huo.

Je vp kuhusu uhusika wa Rostam Aziz na Waziri Yona na kiburi chao cha kukataa kuhojiwa kwanini nao wasipendekezwe kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwani hiyo ni contempt to Parliament ya hali ya juu kwani kamati ilikuwa inafanyakazi kwa kufuata hadidu za rejea walizopewa na Spika hivyo ni sehemu ya Bunge.

How comes watu kama Mgonja wameachwa bila ya kutolewa mapendekezo yeyote ya kuwajibishwa?


Maswali ni mengi nakubaliana na Msabaha hapa pana BANGUSILO tu....
 
Nillifikiria hilo kwa kina...Jibu ..it wouldnt have made any change...Kwani kwa wale waliohojiwa na vidhibitisho vilivyokuwa vimepatika na kuhakikiwa..vinatosha kabisa kutoa..conclusion iliyofikwa..hakuna tatizo. simply..EL is guilty..!!!
 
Hii ripoti ya Mwakyembe ina mapungufu, kwanini hawakumhoji Lowassa wakati kwenye hitimisho wanadai ushahidi wa maandishi, kauli na mazingira una mhusisha kwa namna moja au nyingine?

Nilivyosoma hiyo report jana nimeona kulikuwa na barua toka kwa Private Secretary wa Lowasa kwenda kwa Msabaha, huo ni ushaidi wa maandishi, kule kuumwa sikio kwa kamati na Msabaha na Kazaura ni ushaidi wa Kauli, Ule ufuatiliaji wa karibu na Vishawishi walivyotaka kuwapa wanakamati ili wasi andike report mbaya ni ushaidi wa kimazingira. Apart from kauli zake Bungeni kwamba Wao walifanya huo Mkataba kwa nia nzuri, na kwamba Mawaziri wengine wawaelemishe Wabunge. Kilicho kuwa kina muwasha ni nini? kama sio Guilty Conscious.
Hata Hatua ya TAKUKURU kuwa safisha ina maanisha kulikuwa na Jambo
 
Nillifikiria hilo kwa kina...Jibu ..it wouldnt have made any change...Kwani kwa wale waliohojiwa na vidhibitisho vilivyokuwa vimepatika na kuhakikiwa..vinatosha kabisa kutoa..conclusion iliyofikwa..hakuna tatizo. simply..EL is guilty..!!!

Azimio,

It would make big impact, taarifa za jana usiku ni kuwa Lowasa kakataa kujiuzuru kwa kuwa kamati haiku muona anahusika moja kwa moja, hivyo huu upenyo walimpa nae anautumia kujitoa kimasomaso.

Kamati imefanya kazi nuzri lakini imejiuma uma sana kwenye ku deal na Lowassa yaani wamekula ng'ombe mzima wameacha mkia tu...
 
........nasikia mzee wa BANGUSILO amekubali KAMA NOMA NA IWE NOMA atabwaga manyanga na kurudi kwao KIBAHA.
 
Nilivyosoma hiyo report jana nimeona kulikuwa na barua toka kwa Private Secretary wa Lowasa kwenda kwa Msabaha, huo ni ushaidi wa maandishi, kule kuumwa sikio kwa kamati na Msabaha na Kazaura ni ushaidi wa Kauli, Ule ufuatiliaji wa karibu na Vishawishi walivyotaka kuwapa wanakamati ili wasi andike report mbaya ni ushaidi wa kimazingira. Apart from kauli zake Bungeni kwamba Wao walifanya huo Mkataba kwa nia nzuri, na kwamba Mawaziri wengine wawaelemishe Wabunge. Kilicho kuwa kina muwasha ni nini? kama sio Guilty Conscious.
Hata Hatua ya TAKUKURU kuwa safisha ina maanisha kulikuwa na Jambo

August exactly! u got it perfectly right! Tatizo langu ni kuwa pamoja na overwhelmingly evidence ya kuhusika kwa Lowasa bado kamati teule inampa khiari ya "kupima uzito wa madai mwenyewe" Mimi naona pamoja na kazi nzuri ya kamati hapo wame fall short tena big time!
 
Azimio,

It would make big impact, taarifa za jana usiku ni kuwa Lowasa kakataa kujiuzuru kwa kuwa kamati haiku muona anahusika moja kwa moja, hivyo huu upenyo walimpa nae anautumia kujitoa kimasomaso.

Kamati imefanya kazi nuzri lakini imejiuma uma sana kwenye ku deal na Lowassa yaani wamekula ng'ombe mzima wameacha mkia tu...

Ile kukata kujiuzulu ni hasira ya papo kwa papo kusemwa kadamnasi, he is still digesting the report na Mai Waifu wake. Na Watoto na Ndugu na Marafiki na wapambe.
Anatafakari Maisha ya Baadae yatakuwaje.
 
kamati haijampa upenyo, ila imemtega kama mjanja atakuwa kauona mtego na suluhisho ni kuachia ngazi tu.


waarabu wanamsemo:
mwenye akili hufahamu kwa ishara
 
Mhe. Mwakyembe ametupa hali halisi ya mambo, sidhani kama kuna haja ya bunge au Mhe. Rais kufanya mabadiliko kwa ajili ya watanzania, NI SISI WATANZANIA, MIMI NA WEWE NA YULE TUNATAKIWA KUFANYA CHANGE, NA WALA SIYO KUWA READY FOR CHANGE, LET US CHANGE THIS, sisi kama watanzania wa kweli tunatakiwa kuonyesha kuwa tunataka mabadiliko ya kweli, sidhani kama kumsubilia Mhe. Kikwete afenye mabadiliko ni jambo nzuri, tunatakiwa sisi kuingia barabarani na kutaka mabadiliko hayo soon and very soon.Mimi binafsi nimechoshwa na Serikali ya Mhe. Kikwete kwani ina mapungufu mengi hata kama kuna watu safi ndani yake ni wachache sana.

LET US BE THE CHANGE AND NOT READY FOR CHANGE, THEY WONT'T DO THAT FOR US, ESP, DURING THIS TIME OF CRISIS.
 
Hivi ni lazima yeye ajiuzulu...Dr Mwakyembe ameliweka Bunge mtegoni na pia amemuweka JK mtegoni. Hayo yote ni iwapo EL ataukwepa mtego wake.
 
It is time now Wabunge wahoji sababu za Wabunge kukataa kuitikia mwito wa Kamati ya Bunge .Nadhani ilikuwepo kwa mujibu wa sheria na wao kama watuhumiw wenye ushahidi ambao ungaliweza kusaidia sana wakawa wamekataa kuitwa mbele ya kamati .
 
hapa tumeliwa heading inashawishi kuwa mambo yamo humu, ila kumbe inatafuta habari.

sawa mkuu lunyungu ushafika hapo bungeni?


jee usiku uliishia vp?

na vp shuh\ghuli za bunge ambalo sasa linaanza kuota meno zishaanza?


tupashe yanayojiri na yaliojiri na wengine wanaoweza kutusaidia kupata news maaana wengi tumekuwa kama watenda mimba tena mwezi wa mwisho kwa hiyo si wakitako si wa kulala si wa kusimama tuna haha kutaka kujua kulikoni
 
Haya mambo yako wazi na kama inavyoonekana huyu EL kapewa options mbili tu!
Ibara ya 52 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Kamati Teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mhe. Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond Development Company LLC. Hata hivyo Kamati Teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu Tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mhe. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, 1. ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge. 2. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.
Mimi naona anasubiri hili bunge litumie uwezo wake kikatiba!!

He is caught at a junction waiting for some miracles to happen ila the truth of the matter asipoachia ngazi still ataachishwa tu...
 
Maulid Ahmed, Dodoma
Daily News; Wednesday,February 06, 2008 @20:01


KAMATI ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura ya Kampuni ya Richmond imekabidhi ripoti yake bungeni na kuwataja viongozi kadhaa wa serikali kwamba walihusika kuibeba kampuni hiyo hewa na kuisababishia nchi hasara ya mabilioni.

Waliotajwa kwenye ripoti hiyo kwa madai ya kuhusika kuibeba kampuni hiyo isiyokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme ni pamoja na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, anayedaiwa kuwa na uhusiano na kampuni hiyo.

Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko na viongozi wa Tanesco.

Richmond, ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme huo wa dharura ilichelewa kuleta mitambo katika kipindi ambacho nchi ilikuwa ikikabiliwa na mgawo. Hata hivyo, kwa mujibu wa mkataba kwa sasa inalipwa Sh milioni 152 kwa siku hata kama haizalishi.

Mara baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa, wabunge walitangaziwa kwamba itajadiliwa kwa siku mbili, leo na kesho. Waziri Mkuu Lowassa na wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo walikuwamo bungeni wakati ikisomwa isipokuwa Mbunge Rostam.

Katika ripoti yake hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kulikuwa na majaribio kadhaa ya kuwazuia wasifanye kazi yao ipasavyo na hata ya kuwahonga. “Tulichukua kila tahadhari tusibanwe na mgongano wowote wa kimaslahi… hatukupokea senti tano ya mtu wala baiskeli yake.

Mwenye ushahidi tofauti, basi alithibitishie Bunge hili tukufu,” alisema. Alisema wamebaini kwamba viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waliutumia uhuru walionao katika kuhakikisha Richmond inapewa zabuni ya umeme wa dharura.

“Kutotimiza masharti ya Bodi za Makandarasi na Wahandisi na Wizara ya Nishati na Madini kuikingia kifua kampuni hiyo isichukuliwe hatua za kisheria; uteuzi wa mwisho wa Richmond kuwa mkandarasi kufanywa na Waziri Mkuu mwenyewe Juni 21 2006, ” ilisema taarifa.

Walizitaja kasoro nyingine kuwa ni uamuzi wa kuiteua Richmond kuwa mkandarasi kusafishwa na Takuru (sasa Takukuru) kuwa ulikuwa wa wazi na wa haki; uamuzi wa Serikali kuizuia Tanesco isivunje mkataba na kampuni hiyo, licha ya sababu zote kisheria kuwapo, kuwa ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyo juu.

“Kamati Teule kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa mdomo, inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu,” taarifa iliyowasilishwa bungeni imesema. “Ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge,” ripoti ya kamati imesema.

Iliendelea kusema; “Waziri Msabaha na Mwakapugi walisema walikataa kupokea maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu na kuipa Richmond upendeleo, lakini baada ya mahojiano chini ya kiapo, Dk. Msabaha akaiuma sikio Kamati Teule kuwa suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu kwa maneno yake mwenyewe alisema “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo”.

Balozi Fulgence Kazaura (alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco,) nje ya kiapo Novemba 30 mwaka jana alisema Richmond ulikuwa mradi wa ‘Bwana mkubwa’ na ‘mshirika wake mkubwa kibiashara’, akimaanisha Waziri Mkuu na Rostam Aziz…,” alisema.

Katika ripoti hiyo yenye kurasa 165 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mbunge wa Kyela, kwa saa 1:30, ilionyesha jinsi kampuni ya Richmond Development LLC ilivyokosa sifa za kushinda zabuni ya kuzalisha umeme, lakini baadaye “ikabebwa.”

Katika ripoti hiyo, kamati hiyo imependekeza Waziri Karamagi, awajibishwe kutokana na kushabikia sana uhalalishaji wa Mkataba wa Richmond kwa kampuni ya Dowans Holdings S.A. Imependekeza pia Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha na Katibu Mkuu Arthur Mwakapugi, wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa madai ya kuliingiza Taifa kwenye mkataba na Richmond.

Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko, naye imependekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond ambao inaelezwa ulijulikana tangu mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta.

Kwa upande wa Mbunge Rostam, Mwakyembe alisema kuwa mashahidi zaidi ya watano waliohojiwa ambao walimtaja kuwa na uhusiano na kampuni za Richmond na Dowans iliyokuja baadaye kuchukua kazi za Richmond. Kuhusu Mwanasheria Mkuu, kamati ilipendekeza mamlaka ya juu ya nchi imwajibishe na wasaidizi wake kwa kuiingiza nchi katika mkataba iliyousema kuwa ni wa “aibu.”

Awali kabla ya Mwakyembe kuwasilisha taarifa hiyo, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alisimama kuomba muongozo wa Spika akisema katika kikao chao cha Januari 28 cha wabunge walielezwa shughuli za Bunge na miswada itakayowasilishwa ambapo shughuli za serikali zinapewa kipaumbele hivyo miswada ilikuwa haijakamilika kupisha kupokelewa kwa taarifa hiyo.

Hata hivyo, Spika alisema kamati ya uongozi yenye mwakilishi kutoka serikalini iliamua kuwasilishwa kwa ripoti hiyo ya Richmond jana na kuongeza, “nami nimeona busara kwa sababu hisia za wabunge katika semina ya Jumapili (iliyotaka ripoti hiyo kabla kujadiliwa miswada ya mafuta na umeme) zinanielekeza hivi ni sahihi.”
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom