M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
alipoulizwa kwamba kwa nini hakujiunga Chadema ambacho arguably ndicho chenye nguvu na kingefanya apate umaarufu zaidi akajibu "ni kweli Chadema ni chama imara na viongozi imara lakini si busara kuweka mayai yote kwenye kapu moja".Karibu!
Stay tuned!
Maalim Seif anasema uamuzi wa kuhamia ACT wazalendo haukuja ghafla bali ulikuwa ni mchakato.
Anasema walifanya mazungumzo na vyama vyote vya UKAWA ikiwemo Chadema na Nccr na kwote walikaribishwa ila ACT wazalendo walipata scores nyingi.
Kitu kikubwa kilichowavutia kwa ACT wazalendo ni uthabiti wa viongozi wao, malengo na dhamira zao pia rika la viongozi wao kwani ni vijana wenye nguvu.
Maalim Seif amesema wameenda ACT wazalendo kuimarisha nguvu ya upinzani na kamwe si kutafuta madaraka.
Maalim anasema watakusanya kadi zao zote za Cuf bendera pamoja na sare na watampa KC Zitto ili akamkabidhi Msajili wa vyama ambaye atajua pa kuzipeleka.
Cuf ina majengo matatu tu mengine yote ni mali za wanachama hivyo wana hiyari ya kubadili matumizi.
Lengo la ACT ni kushika dola hivyo amevitaka vyama vya upinzani kuungana ili kuitoa CCM madarakani.
Maalim Seif amemalizia kwa kusema lengo la msajili na serikali ilikuwa ni kummaliza kisiasa wakiamini wakishamnyang'anya Cuf basi atakimbilia Chadema ndio sababu walipigwa na butwaa waliposikia amejiunga na ACT wazalendo.
Ahsanteni
Maendeleo hayana vyama!
tafsiri rahisi ya hili jibu la Maalim ni kuwa anaichukulia kambi ya upinzani (ukiondoa kina Lyatonga, Lipumba, Cheyo, nk) kama ni umoja wenye maslahi yanayofanana.