Live Bungeni: Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini

mimi nimesikia hivi
kuunganisha umeme wa single face kwa umbali wa nguzo moja ni 337000 kwa vijijini na 454000 kwa mijini
kwa umbali wa nguzo 2 kwa single face vijijini ni 515000 na mijini 696000
bei hizi zitaanza january 2013 bila ubishi wowote.

Gharama ya kuunganishiwa umeme yashuka... vijijini imeshuka kwa asilimia 60 na mjini imeshuka kwa >20%!

Sasa ni 177000 kwa vijijini na 340000+ kwa mijini..

Source: waziri mhongo bungeni live now
 
Wabunge muulizeni mrahaba 4% nani wameshiriki kukubaliana na upuuzi huo!!!!
Tunahitaji 55% ya raslimali yetu iingie direct kwenye mzunguko wa uchumi wetu.
Katika hili hatuhitaji comparison ya failiers (states)

obviously Ngeleja
 
idadi ya wachangiaji itakuwa 32 tu kati ya waombaji wa kuchangia zaidi ya 100. Kazi ipo yaani yaonekana kila mmoja alikuwa ana nia ya kutoa madukuduku
 
Pan African Energy - ni wanyonyaji na wezi tu. Walitakiwa kulipa kodi kwa kudai kuwa wanaweza kuharibu miundombinu ya usambazji wa gesi katika maeneo wanayoyasimamia. Yaani mali asili zetu wenyewe na kodi wakatae kutulipa kodi
 
Waziri wa nishati na madini anasema 4% zitafanya taifa kupata pato la shs bill30...what a shame,,

Ndio maana Mnyika kwenye hotuba yake amejata neno serikali dhaifu takribani mara tano!!!

Swali je serikali hii dhaifu inaongozwa na nani? Tafakari..
 
Wakuu mnaosikiliza live tupeni updete, vp upande wa kumiliki hisa ktk migodi muwekezaji anatakiwa asizidi 60% au yalikuwa ni maneno ya kwenye magazeti tu?
 
upatikanaji wa madini ya uranium: Namtumbo na manyoni ndo maeneo yaliyothibitishwa kuwa na kiasi kinachoweza kuchimbwa kati ya maeneo mengi yalotajwa. Eneo la mradi wa namtumbo liko katika hifadhi ya selous na serikali imeiomba UNESCO kuongeza eneo la mradi na wamekubaliwa

Naomba nipewe kibali cha kuwinda wanyama wote kwenye eneo la mradi wasije uliwa kwa baruti.
 
madam speaker kishaanza kuweka liukuta kuzuia makombora kwa serikali. Mchangiaji anasema kuna siasa chafu - CCM kudai CUF na CHADEMA ni vyama vya kidini na ukabila. Madam anadai jamaa anakwenda nje ya hoja na wabunge wanasikika wakizomea
 
Mchangiaji amewaonya watawala kwamba hapatakalika kama wananchi wa mikoa ya kusini inapopatikana gesi hawataelezwa watanufaikaje?
 
Sikuelewa kwa nini wabunge wa CCM walikuwa wanampigia Mh Mnyika Makofi akiwakilisha hotuba ya upinzani,. inaonekana swala la Nishati halina chama, na nashawishika kusema mengi ya yaliyozungumwa kwenye hotuba ya upinzani yamepelekwa na serikali maana haiwezi kujikosoa yenyewe kwenye hotuba zake itakuwa kichekesho. Dah, kumekucha naona mpaka Sasa woote wamekuwa wakali hebu tuone linavyoendelea
 
Sikuelewa kwa nini wabunge wa CCM walikuwa wanampigia Mh Mnyika Makofi akiwakilisha hotuba ya upinzani,. inaonekana swala la Nishati halina chama, na nashawishika kusema mengi ya yaliyozungumwa kwenye hotuba ya upinzani yamepelekwa na serikali maana haiwezi kujikosoa yenyewe kwenye hotuba zake itakuwa kichekesho. Dah, kumekucha naona mpaka Sasa woote wamekuwa wakali hebu tuone linavyoendelea

wameshajipanga hao mkuu. wanataka kumtoa mtu sadaka na ndo maana wanashangilia hayo mawe toka upinzani
 
mheshimiwa mashishanga anadai kuwa wazungu wanachimba madini yetu na wanaenda kuyapanda huko kwao na yanaota!!!!!!
 
Hii imenishitua kwa kweli yaani hata nguzo za umeme twaagiza nje wakati mgororo miti ya nguzo kibao!!!!
 
Back
Top Bottom