Live: Baadhi ya mambo muhimu yaliyomo ndani ya rasimu ya katiba mpya

May 24, 2012
54
10
Kati ya mambo mengi yaliyoelezwa ni pamoja na 1. IDADI YA MAWAZIRI WASIOZIDI 15. 2. TANZANIA BARA KUWA NAMAJIMBO YA UCHAGUZI 25 TU kila JIMBO WABUNGE (2)WAWLI. 3. BUNGE LA MUUNGANO LIWE NA WABUNGE 75 (Toka Zanzibar 20, bara 50, na wawakilishi wa makundi maalum watano )
 
Hii nimeipenda sana,italeta maendeleo na kupunguza gharama,mawaziri 15 saizi kabisa maana wengi tulionao kwa sasa wanaongeza idadi tu lakini hawana jipya,waziri kama magufuli hata umpe wizara 3 ataziweza,cha msingi ni ku-merge na kuwa na wizara chache sana na kuwa na mawaziri ambao ni so compitent kuendesha wizara hizo,majimbo ya uchaguzi 25 ni burudani tosha,wabunge wengi ni mzigo tu,wengi wanaenda kujaza bunge tu na kusinzia na kuishia kugonga meza kusapoti kila hoja inayotolewa,wengi wamechoka kimwili na kifikra na uwezo wa kufikiri umefikia kikomo,tukipata wabunge 25 mfano kama Tundu Lisu regardless wametoka chama gani wanatosha sana kujenga hoja na nchi ikasonga mbele.KAMA NI KWELI HONGERA SANA TUME YA WARIOBA KWA KUTOA MAPENDEKEZO CONSTRUCTIVELLY japo najua fika yatakutana na pingamizi kubwa toka kwa wabunge na mawaziri kwani hawataruhusu ulaji uondoke kirahisi.Pia nadhani wakuu wa mikoa na madiwani wangeondolewa kabisa,hawana umuhimu kwa dunia ya leo,wachaguliwe viongozi kwa kura na sifa maalumu academic ili wawe viongozi wa mikoa na wawajibike kwa wananchi
 
Kwanza kabisa naunga mkono mapendekezo hao maana yanampunguzia mzigo mlipa kodi.
Mapendekezo yangu ingefaa kabisa kuanzia Rais,Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa Wilaya na wengine wote waliopo kwenye kada ya Uongozi iwe ni MARUFUKU kupata huduma hizi kwenye sekta Binafsi kwa wao wenyewe pamoja na familia zao;- Elimu na Afya,
 
Wakuu wa Mikoa na Wilaya hakuna wanachokifanya inastahili kabisa katiba isiwatambue
 
Ni mapema mno,ngoja tutafakari nyuma ya pazia (if any), maana hakuna jambo limo ndani ya rasmu halina maslahi ya CCM, maslahi ya kitaifa tutayatafakari kwanza....ogopa kitu inaitwa ccm....ogopa!...everything is made more political than the betterment of the nation at large..
 
Wakurungezi pamoja na Makatibu wakuu wapigiwe kura na wananchi
 
Bonge ya rasimu ....vp kuhusu wakuu wa mikoa na walaya ? Watabakia na kama ndio watapatikanae ? Manake hawa nao ni mzigo tosha

Ndugu
 
Kati ya mambo mengi yaliyoelezwa ni pamoja na 1. IDADI YA MAWAZIRI WASIOZIDI 15. 2. TANZANIA BARA KUWA NAMAJIMBO YA UCHAGUZI 25 TU kila JIMBO WABUNGE (2)WAWLI. 3. BUNGE LA MUUNGANO LIWE NA WABUNGE 75 (Toka Zanzibar 20, bara 50, na wawakilishi wa makundi maalum watano )

HONGERENI CHADEMA kwa kuwa, wanatekeleza japo si kwa usahihi yale mliokuwa mnapigania. Kwa vile wanafuata maono yenu hawatakuwa na implementation strategy za kwenu, watavurunda vurunda kwa maana ni kitu walichokuwa wanakipinga na wanafanya kwa shingo upande kwa sababu ya nguvu ya umma ilivyo sasa.

Peoples power inaonyesha matunda.
 
Back
Top Bottom