Lita Tengeru: Uongozi wa chuo wazuia utumiaji wa maji kwa wakazi wake

Panthera 1

Member
Dec 30, 2014
50
9
jana nilikuja na uzi unaozungumzia hatari iliyopo kwa wanachuo wa chuo cha mifugo Tengeru pamoja na wakazi wake kutokuwa na huduma ya maji kwa kipindi karinu miezi mitatu licha ya kuwa kila kaya inechangishwa shilingi za kitanzania 30,000 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya kuvutia maji ambayo hadi sasa haijulikani ni lini itanunuliwa na haijulikani ipi hatima ya pesa zilokusanywa.

ndani ya chuo hiki cha mifugo Tengeru kuna kampuni ya ulinzi iitwayo STEMO ambayo inashughulika na ulinzi ndani ya chuo ambapo moja ya kazi zao ni kulinda mali za chuo lakini leo kwa ghafla wamekuwa walinzi wa maji ambayo yanapatikana ktk kapori kadogo ndani ya eneo la chuo na chemchem hiyo ipo karibu na banda la mbuzi wa chuo.

majira ya saa sita siku ya jana walinzi hao wakiwa na bunduki waliwakamata watoto walokuwa wakichota mahi na kuwaweja chini ya ulinzi na kutoa taarifa ya kwamba yeyote atakaechota maji eneo hilo atapigwa faini ya shilingi elfu hamsini.

yote hayo yanafanyika uongozi wa chuo ukifahamu na wao ndio wanaowatuma walinzi hao kufanya hivyo.

yapo maswali ambayo wakazi na wafanya kazi tunajiuliza,maswali hayo ni :

1)NI AMRI KUTOKA KATIKA SERIKALI IPI ILIOTUMWA KWA VIONGOZI WA CHUO CHA MIFUGO TENGERU YA KUZUIA UTUMIAJI WA MAJI HAYO AMBAYO YAMEANZA KUTUMIKA BAADA YA CHUO KUSHINDWA KUTOA MAJI KTK ZIWA DULUTI ?

2)NI LINI SERIKALI YA TANZANIA IMEANZA KUWAZUIA WANANCHI WAKE KUTUMIA MAJI ?

3)KAMA MAJI HAYO HAYAFAI KUTUMIWA NA WATU,JE WATU WAKATUMIE MAJI WAPI ?
Bado inakuwa ajabu na inashangaza kuona mtu akizuia matumizi ya maji.

yani leo inafikia hatua mtu anamnyina binadamu maji Au ndio ndip utaratibu wa mama Masam(mkuu wa chuo) aliojiwekea kwa kuzuia watu kutumia maji tena akitumia walinzi binafsi.

MIFUGO YA SASA,SIYO MIFUGO YA ZAMANI.

Maji ni kwa ajili ya watanzania.

SERIKALI KARIBUNI CHUO CHA MIFUGO TENGERU.
 
Last edited by a moderator:
Serikali itimize wajibu wake wa kuwapatia wananchi huduma ya maji.

Kuingia ndani ya eneo la mtu bila ridhaa yake kwa kisingizio cha majo sio sahihi (ni kweli wana shida ila wengibe wataona ni fursa wanaweza kuingia kufanya yao huku wakisingizia kuchota maji)

Maisha yamebadilika unashangaa kunyimwa.maji????
 
Back
Top Bottom