Wakuu habari zenu,
R.I.P jemedali na mbabe wa vita JPM.
Kumekuwa na habari zikizunguka mtandaoni siku nyingi kabla hata ya Rais kutangazwa kifo, kwamba huko benki Kuu yetu ya Taifa kuna watu wamekwapua pesa na madini.
Hiki kilikuwa kipindi ambacho tetesi zimezagaa kwamba Rais anaumwa na baadae zikaenea kwamba ameaga dunia kabla mamlaka husika ya serikali kuthibisha.
Hatimaye, Serikali ikathibitisha Rais ameaga dunia, na tayari tumezika cha kushangaza leo CAG na TAKUKURU wametoa ripoti zao mbele ya Rais mpya mama Samia....Na mama ameagiza uchunguzi ufanyike BOT kuanzia january mpaka march 2021.
Je, mama kanusa harufu ya hatari kama taarifa zinavyosambaa mtandaoni kwa mda mrefu sasa?
Na kwanini iwe january mpaka march? Hapa ndio napata ukakasi zaidi..maana kipindi hiki ndio hali ya Rais JPM ilianza kuteteleka na hatimaye uvumi wa kupora pesa BOT kwa kufoji sign yake ukazagaa...
Kama ni kweli, awamu iliyopita inaweza kuwa na madudu mengi zaidi..
Tusubiri muda haujawahi kuongopa.