Lisu awataka waliotuhumiwa kwa ufisadi wajibu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Lisu awataka waliotuhumiwa kwa ufisadi wajibu

na Joseph Malembeka, Morogoro
Tanzania daima

MWANASHERIA ambaye ni mkurugenzi wa sheria, katiba na haki za binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lisu, amewataka mwenyekiti wa Chama Cha Mpinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete na katibu mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba, kukanusha kinagaubaga tuhuma dhidi ya viongozi na chama hicho, badala ya kutishana kwa nguvu ya dola.
Alisema Watanzania wamesikia hoja za wapinzani juu ya tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali ya CCM, na kilichobaki ni kusikia tuhuma hizo zinajibiwa moja kwa moja na watuhumiwa na Makamba kujibu kwa niaba ya chama chake, badala ya kutishana kwenye vyombo vya habari.

Akihutubia mkutano wa hadhara mjini hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita, Lisu alisema kuwa CCM haina viongozi wa kuwasaidia kwa kuwa asilimia kubwa wananuka rushwa.

Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kama sehemu ya kujiimarisha.

“Anayebishia hilo ajitokeze hadharani akanushe, kumbukeni kuwa si jmbo rahisi kumtuhumu mtu hadharani, kama kweli sisi ni wazushi, tunataka kuchafua majina yao, waje hadharani wakanushe haya,” alisema.

Lisu, ambaye muda wote alikuwa akiutaka umati huo kumsikiliza kwa makini na kutomshangilia kwa kuwa anayozungumza ni ya hatari, alisema nchi inakabiliwa na matatizo makubwa sana kutokana na kutawaliwa na viongozi wabovu, na kwamba hali hiyo imewarahisishia kazi wapinzani.

Alisema kuwa waliotuhumiwa wametajwa kwa majina, ni vema iwapo wakajitokeza hadharani na kujitetea kila mmoja kutokana na tuhuma zinazomkabili, kuliko kutoa kauli za jumla kuhusu tuhuma za ufisadi.

Lisu alisema kushindwa kwa utawala kufahamu kiini cha matatizo yanayolikabili taifa, kumesababisha nchi kuingia katika matatizo mazito yakiwemo ya uchumi na hali hiyo inahatarisha kupoteza mwelekeo wa siasa.

Alisema inashangaza kuona kuwa wafanyabishara hao ni sehemu ya mamilioni ya Watanzania ambao waliipigia kura CCM lakini ilipoingia madarakani imewageuka na kuwaona takataka.

Alisema kutokana na uongozi huo, leo Mtanzania anaweza kusingiziwa kesi kubwa na hakuna wa kumtetea kwa kuwa hana fedha za kuwahonga polisi, mahakimu na maofisa magereza.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Haki na Mahusino ya Umma wa CUF, Mbaralah Maharagande pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa vilivyo katika ushirikiano.
 
Basi nimeelewa kwanini Tundu Lissu ameupokea uchifu kwa mikono miwili
[HASHTAG]#HapyAnniversaryToMeInJF[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom