Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 27,340
- 65,830
LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.
Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.
Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.
Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.
Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu
Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.
Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.
Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.
Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.
Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.
LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam