List ya Vyama 21 vya Siasa na Viongozi Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

List ya Vyama 21 vya Siasa na Viongozi Wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sanctus Mtsimbe, Jan 10, 2009.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Jan 10, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160

  VYAMA VYENYE USAJILI WA KUDUMU

  1. No.0000001
  Chama cha Mapinduzi(CCM)
  1st July 1992
  Jakaya Mrisho Kikwete -Chairman.
  Yusuph Makamba -Secretary General
  Kuu Street Dodoma
  Tel No. 026-22821-8
  P.O.Box 50 Dodoma
  Also Lumumba Street, P.O.Box 9151 Dar es Salaam.
  Tel No.2322727

  2. No.0000002
  The Civic United Front (CUF) 21st January 1993
  Prof. Ibrahim Lipumba-Chairman.
  Seif Shariff Hamad- Secretary General
  Mtendeni Street at Malindi, P.O.Box 3637 Zanzibar
  Tel. No 024-2237446
  Fax No 024-2237446
  Also Pot No.98 Blck A Buguruni Padya
  P.O.Box 10979 Dar es Salaam

  3. No.0000003
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 21stJanuary 1993
  Freeman Mbowe-Chairman.
  Dr.Willbroad Slaa- Secreatary General
  House No. 170 Uipa Street Kinondoni, P.O.Box 31191 Dar es Salaam
  T :0744-263200,0744-366995
  Tel:2668866, 0748-6669995

  4. No. 0000004
  Union Multiparty Democracy (UMD) 21stJanuary 1993
  Salum S. Alli-Chairman
  Ali Mshangama Abdallah- Secretary General
  House No.84 plot No. 630 Block No. 5 Kagera Street Magomeni P.O.Box 2985 Dar es Salaam. Tel: 0744-478153

  5. No.0000005
  National Convention for Construction and Reform (NCCR- Mageuzi) 21st January 1993
  James F Mbatia-Chairman
  Mwaiseje Polisya-Secretary General
  Plot No 2 Kilosa Street Ilala
  P.O.Box 72474 Dar es Salaam.
  Tel:0744-318812
  0744-276467/286536

  6. No.0000006
  National League for Democracy(NLD)21stJanuary 1993
  Dr. Emanuel Makaidi- Chairman
  Vacant…-Secretary General
  Plot No D/73 Sinza, P.O.Box 352 Dar es Salaam
  Tel:0741-259442

  7. No.0000008
  No.0000008
  United People’s Democratic Party(UPDP)4th February 1993
  Fahmi N. Dovutwa-Chairman
  Abdallah Nassor Ally-Secretary General

  8. No.0000009
  National Reconstruction Alliance (NRA)
  8th February 1993
  Rashidi Mtuta-Chairman
  Massoud Rattul-Secretary General
  Bububu Street Tandika Kilimahew
  P.O.Box 100125 Dar es Salaam
  Tel:0744-496724

  9. No.00000011
  Tanzania Democratic Alliance(TADEA)5 April 1993
  John Lifa Chipaka-Chairman
  Charles Dotto Lubala-Secretary General
  Buguruni Malapa
  P.O.Box 482 Dar es Salaam,
  Tel: 0744-980272
  0744-288996

  10. No.00000012
  Tanzania Labour Party (TLP) 24th
  November 1993
  Augustino L.Mrema Chairman
  Rajabu Tao-Secretary General
  Usalama Magomeni,
  P.O.Box 7273 Dar es salaam.
  Tel:2443237,0744-325648,0744-927362

  11. No.00000013
  United Democratic Party(UDP) 24th 1994
  John Momose Cheyo-Chairman….Vacant-Secretary General
  Mbezi Juu,
  P.O.Box 5918 DSM.
  Tel:0748-613723,0741-265404

  12. No.00000053
  Demokrasia Makini (MAKINI)
  15th November 2001
  Prof. Leornad Shayo-Chairman
  Dominick Lyamchai-Secretary General
  Mbezi Beach Makonde, Near Nguruko International Schoool
  P.O.Box 75636
  Dar es salaam
  Tel:0744-288179,0744-295670
  Zanzibar-P.O.Box 2872 ZNZ Tel: 0747-860512
  Taveta Meli Nne

  13. No.00000054
  The Forum for Restoration of Democracy (FORD) 18thJanuary 2002
  Ramadhani Mzee-Chairman
  Said Kondo Ramadhani-Ag.Secretary General
  Kibambawe Street No.13 Kariakoo,P.O.Box 15587 DSM Tel 0744-478116

  E-mail : tz2004@yahoo.comThis e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it

  14. No.00000056
  Chama cha haki na ustawi (CHAUSTA) 15th November 2001
  James Mapalala-Chairman
  Joseph D.Mkomagu-Secretary General
  Drive in Oysterbay P.O.Box 5450 Dar es salaam Tel:0744-990228

  15. No.00000057
  Democratic Part (DP) 7th June 2002
  Rev.Christopher Mtikila-Chairman
  Stephen Mhina Mbwana-Secretary General
  Mchikichini Ilala
  P.O.Box 63102 Dar es salaam
  Tel: 0741-430516, 0741-625349

  16. No.00000058
  Progressive Party of Tanzania(PPT-Maendeleo) 4th
  March 2003
  Peter Kuga Mziray-chairman
  Ahmed Hamad-Secretary General
  Plot No.11 Kawawa Road Morocco.P.O.Box 31932 DSM.
  Tel:0744-300302

  17. No.00000065
  Jahazi asilia-17th
  November 2004
  Kasimu Bakari Ally-Chairman
  Haji Mussa Kitole-Secretary General
  Saateni JKU Road,
  P.O.Box 761 Zanzibar, Tel: 0747-428593
  0744-937065
  0744-016589,0748-509176
  E-mail –jahazi Asilia@yahoo.comThis e-mail address is being protected from spam bots, you need JavaScript enabled to view it

  18. No.00000066
  Sauti ya UMMA(SAU) 17th February 2005
  Paul Herny Kyara-Chairman
  Jacob Nkomola-Secretary General
  Plot No.231 Block F Shekilango Road,Kinondoni Districh,P.O.Box 5480 Dar es salaam
  Tel:0745-870601
  0748-840087

  VYAMA VYENYE USAJILI WA MUDA

  19. National Democratic Union of Tanzania(NDUTA)
  1. Michael T. Makoba
  2. Fabian J. Midede
  19/10/2001

  20. Chama cha Ukombozi wa Demokrasia (CHUDEWAMA)
  1. Juma Wahi
  2.Ramadhani Hamisi
  5/7/2004

  21. National Democratic Part for Rehabilitation (NDPR-MAREJESO)
  1. Mustafa Sapi Mkwawa
  2. Zahoro Daudi Mbalinga
  15/7/2004

  22. National Patriotic Front(NPF)
  1 . Ascetic Malagila
  2. Naftari Nyango 25/8/2004

  Kazi kweli kweli . . . . I wish vingekuwa viwili au vitatu . . .
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Asante kwa list hii.
  List inaonyesha kuwa mtandao wa Voda ndio unaopendelewa zaidi na vyama vingi vya siasa, je hii inaweza kuwa na sababu yoyote maalum?wana JF naombeni maoni yenu.
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Jan 10, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,812
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  ZeMarcopolo

  Nadhani baadhi ya records hazijawa updated huenda kukawa na mabadiliko kwa sasa. Naangalia hata suscribers code za simu bado ni za zamani. Ni dhahiri namba hizi waliziandika wakati wa kuwakilisha makabrasha kwa msajili i.e. kabla ya 2005. Kipindi hicho Vodacom inaweza kuwa ilikuwa na market share kubwa.

  Unasemaje kuhusu utitiri wa vyama?
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Vyama ni vingi, ila vyenye nguvu ni vichache. Hiyo list ni ya zamani, manake majina mengi hayajabadilishwa mfano, katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi ni Sam Ruhuza, pia katibu wa TLP ni John Komba kama sikosei. Hata chama cha demokrasia makini, Mwenyekiti hayupo.
   
 5. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  asante kwa orodha hii.
  naona ni vyama vichache vimebadili
  viongozi kwa kufanya chaguzi.
  vingi bado vinaongozwa na viongozi waanzilishi
  kwa kutofanya chaguzi na vingine mabadiliko ya uongozi
  yametokana na "mapinduzi" ya ndani au viongozi
  kutangulia mbele ya haki.
  au nimekosea?
   
 6. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Japo ni vyama vingi lakini ni vingi mno.Matokeo yake ni kuwa mapandikizi ya ccm,kuzorotesha ushindani na chaguzi zikija ni kugawana kura kiduchu na kuiacha CCM ikishinda kwa tsunami.Cha ajabu hapo kuna vyama usikute havina hata diwani lakini 2010 ikifika nao wanasimamisha mgombea wa urais.vurugu tupu!
  Halafu huyu Makaidi ni daktari kweli au ndiyo yaleyale Nchimbi style?Naona chama cha hayati Malima Prof Kighoma bigwa wa uchumi bado kinadunda.Sijui angekuwa hai kingekuwaje sasa?RIP mzee.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Na mimi naenda ku-register changu... Jumanne... kwa hiyo ongeza kwenye list!!!

  Hii Tanzania bwana!!! Sheria imetoa mwanya kwa kuweka wanachama wachache sana wanaoruhusiwa kuanzisha chama... kwa hiyo huenda vikawa hata 80... Nadhani Kenya wanavyo zaidi ya 100....
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Orodha hii inahitaji kuhuishwa
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Utitiri wa vyama unadhihirisha jinsi uelewa wa wanasiasa juu ya demokrasia ya vyama vingi ulivyo na mapengo. Nimesoma katiba ya vyama vitatu tena vikubwa, pamoja na ilani zao za uchaguzi. Zaidi ya wazo la CHADEMA la kuanzisha majimbo, ambalo haliko practicle, sijaona tofauti ya ilani za vyama hivyo kifalsafa. Vyama vyote vina falsafa moja, sasa kuna haja gani ya kuwa na utitiri wa vyama vilivyojengwa kwa misingi inayofanana kifikra!!!
  Hata hivyo kwa vile mpaka sasa hakuna chama kilichojitokeza kuonyesha upinzani maridhawa, basi ni muhimu viendelee kushindana mpaka atakapopatikana mpinzani au wapinzani wawili wakubwa then vingine tunaweza kuvisahau, vikabaki kwenye makaburasha tu, kama wanavyofanya watu wa Marekani.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Kama kuna mwenye data za kiasi cha ruzuku kwa vyama hivyo tungeomba aweke hapa,ccm,cuf,chadema tuviweke pembeni kwanza...Tuanze na hivyo 18 vilivyobaki halafu tuone ni kiasi gani cha pesa za walipa kodi zinatumika kwenye utitiri huu wa vyama maslahi.....Vingine hata havijisumbui kuwa na makatibu,before nilisikia kuwa chama chenye kupewa ruzuku ni lazima kiwe na mbunge...Sasa hivi vinajiendesha vipi,na vina wanachama wangapi? Seriously vama 21 ni vingi mno hata nchi zenye ukomavu wa demokrasia hazina utititri wa vyama ili kuonyesha umakini ama uzingatiaji wa demokrasia na haki za wananchi.
   
 11. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nawashangaa sana kushtuka kwamba eti vyama 21 ni utitiri.

  Labda ni kwa kuwa wengi hamjui kuwa kwenye siasa kuna vyama makini, vyama vya usajili, vyama vifuasi, vyama vya mfukoni na vyama majina.

  Kila kundi hapo ni muhimu kwa ajili ya matumizi ya kisiasa kwa political strategists. Vile vile ni muhimu ujue kuwa si lazima chama kisajiliwe kwa ajili ya kutekeleza majukumu yaliyoorodheshwa kwenye objectives zake za kuombea usajili.

  Ninachojua mimi ni kuwa kufuatia mabadiliko ya nyakati vipo vy ama vitajichuja vife, vipo vitakavyoungana cha ukweli kabisa na kupoteza usajili wao wa awali, vipo vitakavyokufa kifo cha kawaida kabisa na kubakia tu historia na mwisho vipo vitakavyopanda juu na kuzidi kukua kuelekea kwenye lengo lake kwa mafanikio kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya, Kasi Mpya na HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.

  Msiogopee wingi wa vyama kwa sasa.
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sanctus,

  Hiyo ndio demokrasia yenyewe. Hata sisi tusajili cha kwetu kwi kwi kwi!!!

  Kinachonisikitisha mimi hapo ni kwamba tunawachangia pesa CCM, CHADEMA, CUF, UDP na TLP kupitia ruzuku. Vyama vyote vingenyimwa ruzuku na badala yake viendeshwe na wanachama wake wenye moyo.

  Pia mivyama yote imejaza wanaume tu, ndio maana maugomvi kila siku. Naona wenyeviti na makatibu wakuu wote wanaume.

  Inabidi vyama vingine vyenye kutetea baadhi ya mambo navyo vianzishwe kama vile green, JF, Machangudoa, chama cha Mibaba, chama cha warembo, wakulima nk.

  Demokrasia ya kweli TZ huenda inaenda chini ukilinganisha na mwaka 1995. Hii ni dalili tosha kwamba tunachohitaji Tanzania ni quality, vyama vilivyo bora na vyenye sera vichache na wala sio utitiri wa vyama kama ilivyo sasa.
   
 13. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  nadhani ruzuku inatolewa tu kwa vyama ambavyo
  vina wabunge. aidha kiasi cha ruzuku kwa kila chama
  inategemea idadi ya wabunge kutoka chama husika.
  hivyo basi utaona kiasi wanachopata ccm ni kikubwa
  zaidi ya kiasi ambacho wanapewa vyama vya upinzani
  vinayowakilishwa bungeni km cuf na chadema
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Jan 11, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280

  There you are mkuu!

  nilianzisha thread ya kuhusu vyama vingi na ruzuku, inabdi tuwe waangalifu, katika vita hii ya kuleta maendelea nchini, lazima tuhakikisha tuna majeshi mazuri, yenye umoja , na yanayopata haki stahiki.

  niliandika hivi:
  Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe TZ!

  --------------------------------------------------------------------------------

  Ndugu wana JF,

  wakati tunaangalia kulia na kushoto ili kuifanya nchi yetu ipate viongozi yule ambaye kila mtu anamtaka , naona bado natatizwa na hiki kitu kinachoitwa ruzuku!
  Ni kweli ruzuku itolewayo na serikali kwa vyama vya upinzani inaweza ikawa ni chachu ya mabadiliko nchini, lakini pia inaonekana kama ni chanzo cha matapeli wachache kuitumia vibaya, wengine kwa uroho tu, wengine wamekosa ajira na sababu nyingi zifananazo na hizo.

  Napendekeza :
  1.Ruzuku itolewe mwaka mmoja tu kwa vyama vinavyoanza;na kuwe na ufuatiliaji wa hali ya juu , juu ya matumizi ya hizo fedha au
  2.Isitolewe kabisa, kwa sababu:
  (a) Kila chama kizuri chenye sera nzuri kitakachowavutia wananchi ni dhahiri kitapata wanachama wazuri watakaohakikisha wanakitunza chenyewe na watu wake.
  Hali ya sasa hivi hata kama tutasema tunataka demokrasia ni dhahiri utitiri wa vyama hivi, unaleta
  1.Uadui kati ya wenyewe kwa wenyewe!
  2.Wengine kuona basi CCM iendelee tu maana vyama vingi vimeshajizolea umaarufu, aidha wataleta fujo na mara nyingi wanapigana kwa sababu ya fedha. N hii imeongeza hofu ya watu wengi kuwapigia kura hawa wapinzani.

  Kudhihirisha kuwa vyama vingi vinataka fedha tu, utavisikia wakati tunakaribia uchaguzi!!

  Tukiwa na vyama ambavyo wananchi ndio wanaokiendesha , tutapata viongozi wanaowajali zaidi wananchi. Tutapata viongozi amabo hatima ya maamuzi yao ni kwa manufaa ya wananchi.

  Kwa jinsi hii tutatengeneza akinaTsavangirai wetu akina Riala Odinga n.k

  Viongozi wengi wa siasa hasa wapinzani , wawajabike wasiwajibike mwisho wa mwezi hela watapata tu.
  Ni heri kupunguza vyama viwe vichache vya kiwananchi zaidi kuliko hali ya sasa. Afadhali hizo hela ziende mahospitalini n.k

  Tukiangalia kwa undani sasa , hali hii ya kupewa ruzuku haitapelea vyama vya upinzani kushinda, sana sana tumeona migogoro ya ruzuku kila siku na watu kufanya ofisi za vyama kama vijiwe.

  Pia kwa vyama vya siasa vikongwe, sijajua wana miradi gani, na wamewaza nini ili kupata income zao!
  Naamini ubunifu wa kuoata hela kwa njia ya halali , ndio ubunifu huo utahitajika pindi watakaposhika nchi.
  Naomba chama, haswa kile kinachoona kiko tayari kujiendesha kwa nguvu ya umma, kiwe cha kwanza kusema hatutaki ruzuku , hizo fedha ziende hospitalini!

  Vyama vikishuka chini, vikawa havina hela na viongozi wake waanze kuishi maisha ya kulingana na fedha za wanachama, wala yasiyo ya kifahari .Hawa vingozi watakuwa viongozi wa kweli
  .  Mhe. Zito akapinga kabisa swala la kuondolewa ruzuku, kwa kisingizio cha kuwa hata mataifa mengine wanafanya hivyo hivyo!

  Mimi sikubaliani kabisa na ruzuku ya aina yeyote, inayoenda kwa chama chochote.Vyama vinatakiwa kujiuza ka sera. Na ndiyo hii OBAMA nasema watu maskini walitoa mpaka dola 10, mifukoni mwao ili kuchangia democrat kupiga kampeni, na vijana walitoa fedha za kujirusha ili wachangie chama, well hata kama hii haina ukweli wa moja kwa moja, lakini picha inaonekana hapa ni kuwa VYAMA VYA SIASA INABIDI VIWE VYA WATU, kwa namna hii tutapata kiongozi ambaye yuko tayari kulala na njaa! NDIYO SI UMECHAGUA SIASA NA SISI TUKO NYUMA YAKO??

  Hatutaendelea ng'o na ninaamini hata vyama vingi vya siasa vinajua hilo, kuna fungu wanafaidi, nikikosa ajira ni kuanzisha chama!

  Kwa sababu ya hela, wengi ni ndumila kuwili, wanahamahama hovyo, wengi wana sera za kudesa

  Hii in apply hata makanisani, mchungaji mzuri ni yule atakayesema sitaki fungu la kumi! kama kweli anaamini Mungu atamlisha na yeye afanye kazi, bila hivyo nako tuna imani nyingi potofu kila kukicha kwa sababu fedha zimetawala.

  Hivyo CHADEMA, NADHANI KWA SASA PIGANIENI HILO , KUWA HAMUHITAJI RUZUKU, WALA CHAMA CHOCHOTE KISIPATE RUZUKU, NYIE MNAJIUZA NA NIMEWATAJA NYIE simply kwa sababu MKO JUU! MKIFANYA HIVYO MATATIZO YA MAMLUKI NA WANASIASA NDUMILA KUWILI YATAISHA naam bila hivyo forget, mtashika nchi miaka 100 ijayo! ( huu ni ukweli).

  Uzubavu huu ndiyo Mramba anapokewa kwa zuri jekundu, chenge na Lowassa tumeona, no one to see opportunity, hakuna wa kuwaelewesha hawa wananchi husika hayupo! na kama mkienda too late, kwani mna shida gani ruzuku si zipo??

  Tunataka viongozi walio tayari kukaa jela, siku 2 wakishikilia misimamo yao kama akina Morgan, watu waliojitoa hata kufa, wasio na mawazo ya fedha za ruzuku. Watu wa aiba ya Mandela, Nyerere, Tsvangrai,

  Sisemi kuwazima Moyo, lakini nisiposema hapa nachelea nakala zetu na post zetu zitaishia kama kupiga ngumi ukutani!


  waberoya
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Tanzania vyama 21 wananchi millioni 40 tu, USA vyama vitatu tu wananchi millioni 300, no wonder CCM itatawala milele!
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2014
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,843
  Likes Received: 2,316
  Trophy Points: 280
  Katika pita pita yangu nimekuta na hii list ya utitiri wa vyama -- na bado vingine vinaanzishwa, Hapa wamenikumbusha swali la SECTION B "SIASA" Mwaka 1992 kidato cha Sita lilisema hivi:-

  Demokrasia maana yake vyama vingi? Jadili - 20mks
   
 17. D

  Don FREDO New Member

  #17
  Nov 17, 2014
  Joined: Mar 21, 2014
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WADAU NAOMBA KUPATA LIST YA VYAMA VYA SIASA PAMOJA NA BENDERA ZAO,NAONA NIKIINGIA nec.go.tz, sipati taarifa, ile page haifunguki, au kama kuna site ambayo ina hizo taarifa naomba mnijuze wataalamu.
   
 18. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2014
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,692
  Likes Received: 13,632
  Trophy Points: 280
  Vyama vya Siasa vilivyopata Usajili kamili hadi Oktoba 2010


  1.Chama Cha Mapinduzi (CCM)
  2.Civic United Front (CUF)
  3Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
  4.The Union for Multiparty Democracy (UMD) of Tanzania
  5.NCCR – Mageuzi
  6.National League for Democracy (NLD)
  7.Demokrasia Makini (MAKINI)
  8.United People’s Democratic Party (UPDP)
  9.National Reconstruction Alliance (NRA)
  10.Democratic Party (DP)
  11.Tanzania Democratic Alliance (TADEA)
  12.Tanzania Labour Party (TLP)
  13.The United Democratic Party (UDP)
  14.Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA)
  15.Progressive Party of Tanzania (PPT- MAENDELEO)
  16.Sauti ya Umma (SAU)
  17.Jahazi Asilia (JAHAZI ASILIA)
  18.Alliance for Tanzanian Farmers Party (AFP)


  Hapo utaongezea vyama vilivyoanza baada ya 2010 ambavyo ni ACT, ADC, (CCJ na CCK) kama bado vipo hai.mhayo ya Bendera na Nembo utaendelea kutafuta mwenyewe
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Nov 17, 2014
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Nenda Kwenye wavuti ya msajili wa vyama. Google
   
 20. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2015
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  mbona act hakipo??
   
Loading...