Elections 2010 List ya viti maalumu yatoka

Paulo

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
350
66
AMANI NA IWE KWENU WANA GREAT THINKERS!
KWA MUJIBU WA TBC TAIFA, JUMLA YA NAFASI 88 YA VITI MAALUMU IMETOKA NA WENGINE WATAONGEZWA BAADAE. KTK LIST HIYO CCM NI VITI 65 NA CHADEMA NI 23. MENGINE TUTAWAJUZA KADRI TUPATAPO MORE INFO.
:israel::israel:
 
cuf wapo kumi.ccm wapo simba,mlaki,anna abdallah na daftari wengine tutawajuza...............chadema wapo abwao,komu na lucy owen..............m
 
rose kamili, owenya, komu, leticia nyerere, chiku abwao, ni baadhi tu ya waliotajwa. More is to come.............
 
cuf wapo kumi.ccm wapo simba,mlaki,anna abdallah na daftari wengine tutawajuza...............chadema wapo abwao,komu na lucy owen..............m

Hope zile nyumba ndogo za mafisadi wa CCM (Burian na Mbega) watapewa huko pia.
 
AMANI NA IWE KWENU WANA GREAT THINKERS!
KWA MUJIBU WA TBC TAIFA, JUMLA YA NAFASI 88 YA VITI MAALUMU IMETOKA NA WENGINE WATAONGEZWA BAADAE. KTK LIST HIYO CCM NI VITI 65 NA CHADEMA NI 23. MENGINE TUTAWAJUZA KADRI TUPATAPO MORE INFO.
:israel::israel:
Asante lakini habari hii si kamili bali nusu nusu. Anyway tutakutana nayo magazetini.
 
Kama hizo namba ni sahihi basi kura za wabunge CHADEMA imepata chache kulinganisha na asilimia alizopata rais wao. Upande wa CCM inaelekea wabunge wamepata kura nyingi kuliko alizopata rais wao. CUF watakuwa wamepata kura za wabunge ambazo zinakaribiana sana na kura alizopata profesa.

CHADEMA watatoka kuwa na viti 6 mpaka 23+ wakati CCM watatoka viti 58 mpaka 67+. CUF ndio watabaki pale pale walipokuwa 2005.

Kumbuka mwaka huu viti vimeongezeka maana ni 40% wakati 2005 ilikuwa 30%
 
Mtanzania, naona mahesabu yako yana utata.

Kwa mpangilio wako na mahesabu, unaonyesha kuwa CCM watakuwa (kwa uwiano wa asilimia za kura za wabunge vs Rais) wamepata ZAIDI kuliko CHADEMA, hapo hapo unaweka idadi ambayo inakinzana na logic yako.

CHADEMA kutoka 6 hadi 23+ ni ongezeko la 17+ (ongezeko sawa na takribani 283%).

CCM kutoka 58 hadi 67+ ni ongezeko la 9+ (ongezeko sawa na takribani 16%).

Sasa hapo kwa logic na mpangilio wako, sijui unaona nani ana ongezeko kubwa.

Ukiangalia kura za Urais (CCM Kikwete 2005 - 82%, 2010 - 61%), CHADEMA (Mbowe 2005 - 11%, Slaa 2010 - 26%), hapo pia utaona kuna ongezeko kubwa kwa mmoja wao kulikoni mwingine.

Na hii ni kwa mpangilio wako kwenye nyekundu hapo juu.

Kumbuka, kuongezeka kwa viti maalumu kutoka 30% hadi 40%, havibadilishi rate ya ongezeko (gari la uwezo wa tani 10, litabeba tani 10 tu hata kama litaenda safari 2 au 20)
 
Mkuu Mtanzania unaweza Usiwe sahihi kwa Sababu Jumla ya kura za Uraisi siyo Lazima ziwe sawasawa na Jumla ya Kura za Ubunge
 
Kiungani,

Hapo juu hesabu zako zimenichanganya na nimeshindwa kukuelewa.

Nilichoandika ni kwamba inaelekea kwenye ubunge CHADEMA wamepata kura chache kuliko za urais. Kitu ambacho nilitegemea maana Slaa alikuwa maarufu kuliko wabunge wake. Kama wana viti 23 katika 102 ina maana wana around 23% ya kura za ubunge. Lakini kwasababu unatoa kura za vyama vidogo (kwasababu havishiriki mgao wa viti maalum kwa sababu ya kukosa at least 5% ya kura) basi hiyo asilimia 23 inashuka na kuwa chini ya asilimia 23. Ndio maana nika conclude kwamba wabunge wamepata kura chache kuliko rais wao maana Slaa alipata zaidi ya 26%

Upande wa CCM, kama wana viti at least 67 ina maana wamepata kura around asilimia 67 za wabunge wakati rais wao alipata kura asilimia 61. Hivyo conclusion yangu ya kwamba wabunge wamepata kura nyingi kuliko rais wao.

Hiyo ya wabunge kuongezeka kutoka 6 kwenda 23 ilikuwa haina uhusiano na analysis ya hapo juu. Ilikuwa ni information ya ziada tu.

Na hiyo ya CCM kutoka 58 kwenda 67 pia ilikuwa information ya ziada. Ndio maana nikaonyesha effect ya 40% maana mtu mwingine angeshangaa iweje CCM wamepata kura chache lakini viti viongezeke?

Nafikiri umenielewa!
 
Mkuu Mtanzania unaweza Usiwe sahihi kwa Sababu Jumla ya kura za Uraisi siyo Lazima ziwe sawasawa na Jumla ya Kura za Ubunge
Ndege ya Uchumi,

Unaweza kuwa right. Assumption yangu ilikuwa kwamba waliopiga kura za ubunge pia walipiga kura za urais.

Hiyo haikuwa detailed analysis ila nilitaka kuangalia uhusiano wa kura za wabunge na marais wao. Inaelekea kila kitu kimekuja kama ilivyotegemewa upande wa CHADEMA. Slaa alikuwa maalufu kuliko wabunge wake.

Upande wa CCM, tuliambiwa JK alikuwa maarufu kuliko wabunge wake lakini matokeo haya yanaonyesha huenda haikuwa kweli.
 
Idadi ya viti maalumu bungeni inatokana na uwiano wa kura za wabunge majimboni na si kura za raisi wala idadi ya wabunge walichaguliwa.
 
Jamani mwenye taarifa kamili nasikia Kibonde naye yumo kwenye viti maalum.
 
mkuu ccm walikuwa na viti maalumu 80 bunge lilokwisha,angalia mtandao wa bunge.chadema 6, cuf 14
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom