List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Hatimaye leo wapinzani wamefanya kile ambacho wamekuwa wakikitishia mara kwa mara kuwa wanawajua kwa majina vigogo wa ufisadi.Wamewataja kwa majina.

Habari zitafuatia...


Top Level embezzlement claims:

Marmo fault opposition stance

Daily News; Tuesday,September 18, 2007 @00:02

THE government has expressed surprise that the opposition had information about officials involved in serious crime but did not report the matter to law enforcement organs.

The Minister of State in the President's Office (Good Governance), Mr Philip Marmo, said yesterday that conventional wisdom would not allow a person to use such allegations for political gains during a public rally.

"Judging people in a public rally without even having heard the other party's side of the story is not prudent. We have state organs that have the mandate to work on such matters, they should have reported the matter to the same", he said.

Mr Marmo said that the allegations by the opposition were very serious and naturally would have serious consequences and that it was not prudent for them to air them in public without giving the accused the opportunity of defending themselves.

"We have laws that allow people to lodge reports or allegations against any other citizen, we would have expected that that would have been the case instead of a public rally", he said. Mr Marmo also said that the government has its mechanism of working on allegations of malpractices, citing the ongoing audit of the Bank of Tanzania External Payment Account (BoT-EPA) that had been ordered by the government following allegations of abuse.

The opposition had on Saturday during a rally in Temeke district in Dar es Salaam alleged that five Cabinet ministers, two permanent secretaries, a former president and some top BoT officials were behind the embezzlement of some 1.3tr/- of taxpayers' money.

The allegations by the opposition further said that the money was embezzled in the past seven years through five different projects and that two prominent businessmen were used as agents or conduits to stash away public funds for the said projects.

LIST OF SHAME:-


ORODHA YA MAFISADI
(LIST OF SHAME)

KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.

MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI

A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali' kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
(a) Kwamba "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi….";

(b) Kwamba "lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi"; na

(c) Kwamba "Serikali itawajibika kwa wananchi…."
(d) …."

Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, "… Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(a) …
(b) Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(d) Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) …
(f) …
(g) …
(h) Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

(j) Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k) …."

Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa "… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …" ya Katiba. Katiba pia imewapa viongozi wa umma "… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano." Aidha, viongozi wa umma wamepewa "… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…." Vile vile viongozi wote wa umma "watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao."

Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:

(a) Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;
(b) …

(c) Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;

(d) Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
(a) kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;

(b) kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;

(c) kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;

(d) kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;

(e) kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;

(f) kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;

(g) kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
(h) …
(i) Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;

(j) Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KAMA IFUATAVYO:

A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI

Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;

(ii) Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba makampuni mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. – nayo yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50 tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd. badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine haujulikani;

(iii) Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba "… mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja." Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba "Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni." Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha "majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa." Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea "Jamhuri ya Mauritius" na anwani yake iko Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;

(iv) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30 Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. "Katika mazingira haya", inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, "hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani 5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza kulipika." Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA, Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba 2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J. Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd. na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T) Ltd;

(v) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. "Katika mazingira haya", inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, "hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9 zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006…." Kwa mantiki hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni 2007 imetamka kwamba "Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika." Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

2. ANDREW J. CHENGE

Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa "mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria…." Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
(ii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
(iii) Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

(i) Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa "hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06"! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani."

(ii) Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ‘Bwana Basil' anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil' ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo.

(iii) Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma.

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.

Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates' Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.

Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme' iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: "Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)

Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: "Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP."

7. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

8. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

C. SHERIA YA UDHIBITI WA MAKOSA YA KUHUJUMU UCHUMI, 1984
D. SHERIA YA KUZUIA RUSHWA, 1971 na/au SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, 2007

Tangu tutangaze orodha ya mafisadi pale viwanja vya MwembeYanga, mjadala mkali sana umetokea katika taifa. Mara baada ya kutangaza orodha hiyo siku ya jumamosi tarehe 15 Septemba, waliotajwa wengi walikaa kimya bila kujibu chochote wakiamini kuwa vyombo vya habari havitataja majina yao. Ni kweli takribani vyombo vyote vya habari havikutaja majina yao.

Wiki iliyopita ikabadili kabisa mjadala huu ambao ulikua umeanza kulala. Gazeti la MwanaHalisi lilitaja Mafisadi wote kwa majina na kwa vipi wamehusika. Hapo ndipo waliotajwa walipoanza kujibu mmoja baada ya mmoja.

Najua kuwa Mkuu wa Kaya aliagiza kupitia Waziri Marmo kuwa kila mtu ajibu tuhuma zake. Waziri Mkuu alikuwa ni mmoja wa watu waliogomea agizo hilo la mkuu wa kaya ya kwamba kila mtu ajibu tuhuma zake mwenyewe. Aakamtuma Mzee Kingunge ajibu. Haikutosha na pia mwungwana akahimiza kupitia kwa Waziri anaepata nguvu za ajabu hivi sasa ndugu Marmo. Karamagi akaanza!

Majibu ya Karamagi na yale ya Mgonja, ambae alifuatia yanafanana sana. Mtindo wao wa kujibu ulikua ule ule.

Hata hivyo, majibu ya Patrick Rutabanzibwa, mmoja wa wasomi wazuri sana katika Taifa hili yamenifanya nitake tujadili, tumjadili kwa kina yeye na ufisadi wake na ikibidi humu humu totoe 'verdict'. Wale walio karibu nae wamwombe aje humu katika mjadala huu. Kwa nini yeye?
Angalau yeye amejibu baadhi ya tuhuma zake katika mkutano wake na waandishi wa habari. Wakati Karamagi na Mgonja wametishia tu kwenda mahakamani, Rutabanzibwa yeye kasema ni masuala gani hahusiki nayo na yepi anahusika nayo. Kasema kwa kina ni vipi hahusiki na IPTL lakini kakubali kuwa katika bodi ya TANGOLD na pia kuwa na hisa za kampuni hii. Wengine wote isipokuwa Chenge wamechenga kusema chochote. (Chenge kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD).

Nilikutana na Ruta kwa mara ya kwanza mwaka 2003 nikiwa pale Chuo Kikuu cha Dar. Nilikua kiongozi wa DARUSO na tuliandaa mjadala kuhusu Netgroup Solution, kwanini nchi iingie katik mkataba huu (NETGROUP ulikuwa ni mkataba mbovu pia). Tulifanya mjadala pale Council Chamber, alijenga hoja na kutuacha wote hoi licha ya kujindaa kweli kweli.

Tunaambiwa Ruta ni mmoja wa Bureaucrats wenye uzalendo wa hali ya juu na alie tayari kulinda maslahi ya nchi kwa gharama yeyote. Tunaweza kukubali kuwa Ruta alipinga IPTL, lakini IPTL bado ipo na nchi inafujwa.

Kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD, kwa niaba ya serikali. Uchunguzi unaonesha kuwa TANGOLD ni monster. Kampuni hii imehusika moja kwa moja na wizi wa fedha za umma katika Benki Kuu. Mzalendo Ruta anakaa katika bodi ya kampuni hii. Anasemaje juu ya hili.

Rafiki yangu mmoja aliniambia, jamani mmekosea kumtaja Ruta. Ni mwadilifu! Dkt. Slaa, hana tatizo lolote binafsi na watu waliotajwa. Ametimiza wajibu wake na alitoa mwezi mzima kwa serikali kuact, wakadharau. Orodha iliyotolewa ni orodha iliyofanyiwa kazi vya kutosha na wala haikuwa na lengo la kumwonea mtu. Rutabanzibwa, ambae anaonekana kutetewa na watu wnegi sana hapa nchini, ni vema aseme ni vipi ahusishwe na uporaji wa nchini.

Ikumbukwe kuwa katika orodha hii kuna mafisadi wa moja kwa moja na wale waliotumia mamlaka yao ya umma.

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.


Patrick Rutabanzibwa atajwa kama ntu aliyetumia madaraka yake vibaya kuingia mikataba mibovu na kushindwa kuizuia. Ruta aweza kuwa safi, lakini analo la kujibu kwa Watanzania.

Tumjadili Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa zamani (1997-2006) wizara ya nishati na madini na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Maji.



Vielelezo vya Madai ya Ufisadi vya Dk. Slaa vyapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Friday,September 21, 2007 @00:06

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amewasilisha vielelezo vya madai ya ufisadi vilivyotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema), kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua zaidi za sheria zichukuliwe.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ameamua kuzipeleka nyaraka hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile ndiye mshauri mkuu wa mambo yote ya sheria ndani ya serikali.

"Tumeamua kuzirejesha serikalini. Wao watajua watazifanyia nini hizo nyaraka," alisema Sitta.

Awali, Spika alisema angevipeleka vielelezo hivyo Polisi kwa hatua zaidi kutokana na utata wake.

Hata hivyo, baada ya kupokea ushauri wa kisheria kutoka kwa maofisa wa Bunge, ameamua kuvipeleka vielelezo hivyo serikalini vikafanyiwe kazi zaidi.

Ofisa mmoja wa Bunge aliliambia gazeti hili kuwa waliamua kumshauri spika wasipeleke vielelezo hivyo Polisi kwa kuhofia kujiingiza kufanya kazi zinazopaswa kufanywa na maofisa wa upelelezi wa polisi.

"Tulikuwa makini tusigeuke kufanya kazi za CID (wapelelezi wa polisi)," alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa vile si msemaji wa ofisi hiyo.

Naye ofisa mwingine katika ofisi hiyo alisema kwa kuwa hoja ya Dk. Slaa haikuwasilishwa bungeni, ndiyo maana wameshauri nyaraka hizo zipelekwe serikalini.

"Sisi huwa tunafanyia kazi vitu ambavyo vimewasilishwa bungeni, lakini hoja hiyo haikuwasilishwa ndiyo maana tumeshauri viende kwa mwanasheria mkuu wa serikali," alisema ofisa huyo ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Kwa upande wake, Spika alisema nyaraka za Dk. Slaa zina utata na mchanganyiko wa vitu vingi, hivyo kwa kuvipeleka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu anaamini kuwa watajua cha kufanya.

"Mwanasheria anaweza kufanya lolote kwani ndiye mshauri wa mambo yote ya sheria ya serikali, kwa hiyo usiniulize kwa nini sikuvipeleka Polisi kama nilivyoahidi," alisema Sitta.

Alisema kuna sheria za nchi zinazoelekeza namna ya kufanya iwapo kuna nyaraka za namna zinapofikishwa serikalini. "Hivyo sisi hatunazo tena hizo nyaraka," alisema.

Juhudi za kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika hazikufanikiwa na ilielezwa na katibu wake muhtasi kuwa alikuwa anahudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Dk. Slaa alipanga kutoa hoja binafsi juu ya ubadhirifu ndani ya Benki Kuu (BoT) bungeni, lakini baadaye akaondoa hoja hiyo kwa madai kwamba ilikuwa inapigwa danadana.

Baada ya kuondoa hoja hiyo, aliahidi kwenda kwa wananchi kuwashitaki wale aliodai ni mafisadi wanaoitafuna nchi.

Alifanya hivyo kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita na kuwataja vigogo 10 wakiwamo viongozi wa kitaifa wa serikali, mawaziri, wanasheria na makatibu wakuu wa serikali na watendaji ndani ya BoT yenyewe na kiongozi wa CCM.

Jumanne wiki hii, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru alisema serikali inasubiri kupata nyaraka za tuhuma zilizotolewa na mbunge huyo ili iweze kuzijibu.

Waziri alisema tuhuma hizo zilikuwa na lengo la kuwachafua viongozi wa serikali na CCM.

Ngombale-Mwiru aliwaambia wanahabari kuwa serikali ilikuwa haijapata nyaraka hizo.

Tangu kutolewa kwa kwa orodha hiyo na wapinzani, Ofisi ya Rais kwa kuwatumia mawaziri wake wawili, Philip Marmo (Utawala Bora) na Ngombale-Mwiru (Siasa) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Aggrey Mwanri, wameshatoa matamko mbalimbali ikipinga madai hayo ya ufisadi kwa viongozi waliotajwa.

Mwanri amewataka wananchi kuwapuuza wapinzani kwa kauli hizo, kwani zina lengo la kuwachonganisha viongozi na wananchi.

Ngombale-Mwiru alisema kauli hizo za wapinzani zina lengo la kudhoofisha utendaji wa serikali na ni wivu kutokana na serikali kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM.

Marmo kwa upande wake, alimtaka Dk. Slaa kuwasilisha ushahidi wake kwa mamlaka zinazohusika na uchunguzi wa ufisadi yaani Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), ambayo Dk. Slaa anadai hana imani nayo.


Chanzo: HabariLEO



MKONO AJIBU TUHUMA ZA UFISADI.

-Slaa muongo
-Adai ushahidi alioutoa ni feki
-Afichua mawakili wanaoidai BOT kesi ya mdai mfu
-Asema shughuli zake BOT sio kwa kesi moja tu

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono amejibu mapigo ya Dk. Willbrod Slaa kuhusu tuhuma dhidi yake na kusema kiongozi huyo wa CHADEMA ni muongo.

"Slaa hana silaha...huyu alikuwa kanisani enzi zake inashangaza anasema uongo. Huyo (Slaa) ni muongo, kama mimi amenitungia yote hayo, naamini na wengine kafanya hivyo," alisema jana Mkono alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake.

Mkono ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma alisema tuhuma zote zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake hazina ukweli na kuwa lengo la kiongozi huyo wa upinzani lilikuwa kuwadanganya wananchi.

Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Mkono alisema madai ya Dk. Slaa kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia, siyo sahihi.

Alisema katika kesi hiyo ambayo aliipokea mwaka 2003, amefanikisha mambo mengi ikiwemo kuokoa fedha za serikali zilizokuwa zichukuliwe na wadai na ambazo zina walakini ndani yake na kuwa hatua hiyo imemzushia chuki miongoni mwa mawakili.

Mkono alisema kuna kampuni ya mawakili (majina tunayahifadhi) ambayo katika madai yake ya awali ya Aprili 3, 2003 iliomba kulipwa dola 9,917,850 (sawa na sh. bilioni 11) kama gharama za kuendesha kesi hiyo.

Aliongeza kuwa: "Kampuni hiyo hiyo ilipofika Juni 6, mwaka huu, iliomba kulipwa dola 19,835,701 (sawa na sh. bilioni 25.4) kuhusiana na kesi hiyo ambayo muhusika alifariki dunia muda mrefu uliopita."

"Sasa hapo nani ni mfisadi. Waandaishi mtapima wenyewe, mimi naendelea kutetea BOT ili fedha za walipa kodi ambao ni wananchi isiende bure," alisema Mkono na kuwa anafanya shughuli nyingi mbalimbaliza BOT mbali ya kesi hiyo.

Kuhusu kuhusika kwake na kampuni kama vile Azania Agricultural Enterprises, Liberty Leather Shoe Ltd, Azania Eximco na mengineyo, Mkono alisema hausiki nayo kwa maana ya kuwa na hisa au kuwa mkurugenzi wake.

Katika kuthibitisha hilo, alitoa taarifa kuhusu ukaguzi wa kampuni hizo kwa maana ya wana hisa na wakurugenzi wake kama ilivyotolewa na BRELA wiki hii.

Kuhusu kampuni za Oxford Services Ltd na Marcus Ltd, mbunge huyo alikanusha kuwa mkurugenzi au mwenye hisa na kufafanua kuwa alikuwa wakili wa kampuni hizo.

"Haya ni mambo ya ajabu sana. Hivi mtu kuwa wakili wa kampuni au wa mtu ni dhambi au ndiyo unakuwa mfisadi," alihoji Mkono na kuwa katika biashara za kampuni hiyo miongoni mwa waliochukua fedha na kupata matatizo ni Chavda.

Alisema kutokana na matatizo aliyopata Chavda, alitakiwa kufukuzwa nchini mara moja, lakini kutokana na taaluma yake alimtetea kwa mujibu wa sheria na kuhoji iweje wakili ahusishwe na dhambi ya mtuhumiwa.

"Kila mtu ana haki ya kutetewa. Wapo wauaji wamefanya makosa, lakini wana haki ya kutetewa...hata hivyo wakili anayemtetea mtu wa aina hiyo hawezi naye kuitwa muuaji," alisema Mkono na kuwa baadhi ya mambo hawezi kuyazungumza hadharani kwa undani kwa kuwa kama wakili kuna miiko ya kazi.

Mkono alitumia fursa hiyo kueleza ukweli kuhusu suala la kampuni ya City Water na kuwa katika kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa nchini Uholanzi ambayo inashughulikia usuluhishi wa migogoro, kamwe hakupata kumuona.

"Huyu mwingine anayeitwa Tundu Lissu, sikumuona na wala simfahamu kwa kuwa kule mimi nilikuwa naongoza jopo la mawakili wa serikali," alisema Mkono.

Katika tuhuma mbalimbali walizozitoa kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam ambapo Dk. Slaa na Lissu walikuwa wasemaji wakuu, Lissu alitajwa kama mmoja wa mawakili wa serikali katika shauri la City Water.

Akihitimisha kwa ujumla tuhuma dhidi yake, Mkono alisema waliotoa madai hayo anahisi wanamuonea wivu kutoka na mafanikio katika kazi yake na jinsi anavyojitahidi kupeleka maendeleo jimboni mwake Musoma Vijijini.

"Nimemuita Slaa, lakini amegwaya na kwa jinsi anavyosema uongo huenda ningemchapa makonde,"alisema huku akionyesha kusikitishwa na tuhuma hizo.


Imetolewa kwenye Gazeti la Uhuru 21/10/07.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kikwete Aonya kuhusu Ufisadi

Rais Jakaya Kikwete ameonya tabia inayotaka kujengeka miongoni mwa wananchi na hususani wanasiasa ya kugeuka kuwa wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu, na tena wakizitoa huku hizo bila ya watuhumiwa kuwapo.

Amesema tabia hiyo ikiachwa kuendelea siyo tu itaipeleka nchi pabaya, lakini itawatisha wananchi, itawatia hofu na kujenga chuki kati ya mtu na mtu hali ambayo amesema haiendani na taratibu za kuendesha nchi kwa misingi ya kufuata kanuni,taratibu, na sheria za nchi.

Amebainisha kwamba tabia hiyo ya wanasiasa kujigeuza kuwa wao ndio wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu kuwa haimtendei haki mtuhumiwa ambaye naye ana haki yake ya msingi ya kulindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Kikwete ameeleza kuwa kila taarifa inayohusu rushwa au tuhumu za mtu kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, zitachunguzwa kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi na vyombo vinavyohusika na si vinginevyo na kuongeza kwamba yeyote
atakayethibitishwa na mamlaka halali kwamba ama ametoa rushwa au kupokea rushwa atachukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali nafasi na madaraka aliyonayo.

Rais kikwete ameyasema hayo jana usiku (Jumanne) wakati alipokuwa akimshukuru Askofu Thomas Laiser wa Dayosisi Mkoani Arusha ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania, kwa kumpongeza (Kikwete) kwa ujasiri mkubwa wa kupambana na vitendo
vya rushwa na hasa rushwa katika uchaguzi.

Askofu Laiser alitoa pongezi hizo kwa Rais wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hosteli ya Dayosisi ya KKKT Arusha, hafla iliyofanyika katika hoteli ya Kibo Palace, ambapo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi. Jumla ya shilingi milioni 363.6
zilipatikana huku Rais akichangia shilingi milioni mbili. Lengo lilikuwa kukusanya shs. 350.0.

Rais Kikwete amebainisha kwamba nia na dhamira ya serikali ya Chama cha Mapinduzi ya kupambana na vitendo vya rushwa ni ya dhati, na utekelezaji wa vita hivyo umeanzia ndani ya Chama chenyewe.


"Kama sisi wenyewe ndani ya Chama cha Mapinduzi tumeanza kupambana wenyewe kwa wenyewe kwa nini tushindwe kwa watu wengine, tumedhamiria kwa dhati na wala hatutamuogopa na hatumuugopi mtu yoyote" akasema Rais.


Akasema Kikwete "Mhe. Baba Askofu, naomba nikushukuru kwa kunipongeza kwa juhudi zangu za kupambana na rushwa,nimefarijika sana na pongezi zako. Kwa sababu wapo watu wengine wanaoona hakuna lolote tunalofanya, wana macho lakini hawaoni, wana
masikio lakini hawasikii. Tumedhamiria kupambana na rushwa popote pale na tumeanza ndani ya Chama chetu, hiki ni kielelezo cha juu kabisa cha dhamira yetu ya kupamba na rushwa".

Akizungumzia zaidi juhudi hizo za serikali za kupambana na rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla, Rais ameeleza kwa kusema " Nilitoa ilani na tahadhari kabla ya uchaguzi kuanza katika ngazi za wilaya, maana huko ndiko pesa zinakotembea tembea. Niliwaambia wenzangu jamani taarifa hizi za kwamba viongozi wanapata uongozi kwa kununua hii si heshima nzuri, tuachane na tabia hii".

Akaendelea "Tuliviagiza vyombo vyetu kuifanya kazi hiyo. Lakini tunafanya hivyo kwa kuzingatia misingi ya kanuni, taratibu na sheria za nchi". Anasema Kikwete na kuongeza "Hata wale TAKUKURU wakisema huyu tumemkamata akitoa rushwa au katika mazingira ya kutoa rushwa wao hawana uamuzi wa mwisho wa kutoa hukumu, zipo mamlaka halali zinazohusika na kutoa hukumu baada ya kuridhika na upelelezi na uendeshaji wa kesi hiyo. Ni mahakamani ndiko kutakako thibitisha kama mtuhumiwa huyo ametoa au hakutoa rushwa".

Anaonya Rais kwa kusema. " Lakini tusifike mahali tukageuka sisi ndio wapelelezi,wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu. Wako wenzetu ambao wameamua kuwa wapelelezi wao, wakamataji wao, waendesha mashitaka wao na watoa hukumu wao, tena
wanatoa hukumu wakati mtuhumiwa hayupo.Tusijipeleke huko na tukifanya hivyo tunaipeleka nchi pabaya, nchi itayumba na hili si jambo nzuri na wala si sawa".

Anasisitiza kwa kusema " tabia hii ya watu kujifanya wao ndio wapelelezi, wakamataji na watoa hukumu ni tabia ambayo ikiendekezwa itawatisha wananchi, itawatia hofu, na itajenga chuki kati ya mtu na mtu, hii si haki na wala si sawa, hii si nchi isiyokuwa na utawala wa sheria (law of the jungle). Ni nchi yenye utawala halali na unaozingatia sheria za nchi na ina mamlaka ya kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya haki, nje ya hapo ni ukiukwaji wa misingi hiyo."

Akasema haiwezekani kauli ya mwanasiasa mmoja ya kumtuhumu fulani ndio mla rushwa ikawa ndiyo hukumu, au serikali ikalazimishwa kumchukulia hatua mtu yule kwa kutumia
kauli ya mwanasiasa tu, lazima taratibu za kisheria zifuatwe, lakini kubwa na la msingi hapa hata yule anayetuhumiwa naye anayo haki yake ya msingi ya kutendewa haki.

"Baba Askofu ninashukuru umeyasema haya na mimi nimeamua kuyaeleza haya niliyosema" akafafanua Rais.

Awali katika pongezi zake, Askofu Laiser alimweleza Rais kuwa, Dayosisi Mkoani Arusha ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kupitia kwake linampongeza Rais Kikwete kwa moyo wa dhati, kwa ujasiri mkubwa aliochukua hivi karibuni wa kupambana
na rushwa katika uchanguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Akasema Askofu Laiser "tunajua katika mapambano yoyote wataathirika waliomo na wasiokuwako katika jambo lenyewe, lakini afadhali waathirike wachache wasiokuwamo maana bila ya mapambano hayo wale wengi waliomo wataendelea kuendeleza uovu na dhambi hiyo"

Akasisitiza kwa kusema "Mhe. Rais tunajua mapambano hayo yana gharama zake kijamii na kisiasa, lakini gharama hizo ni ndogo ukilinganisha na athari zitakazolikumba taifa hili, rushwa za aina hii na aina nyingine zote zitakapoendelea kufumbiwa
macho. Neno la Mungu linasema ila wanawe hawakuenda njia zake bali waliziacha ili wapate faida wakapokea rushwa na kupotosha hukumu".

Dayosisi Mkoani Arusha ya Kanisa la Kiijili la Kilutheri Tanzania inajenga hoteli itakayoitwa Arusha Springs Hotel mkoani Arusha kama kitega uchumi kitakachosaidia uendelevu wa miradi ya Dayosisi hiyo.

Hoteli hiyo inayotarajiwa kukamilika mwezi Februari mwakani itagharimu Tshs. Bilioni 3.6 sawa na dola za Kimarekani milioni 3.5.

Askofu Laiser amemweleza mpango wa maendeleo wa Dayosisi hiyo ambayo inahusisha ujenzi wa shule za sekondari, hospitali ya rufaa ni juhudi za Dayosisi hiyo la upunguzwaji wa umaskini na kuisaidia serikali ya awamu ya nne iweze kufikia lengo
lake la maisha bora kwa kila Mtanzania.

Kabla ya kuongoza harambee hiyo, Rais Jakaya Kikwete alitembelea na kukagua miradi mikubwa ya shule ya sekondari ya watoto yatima Peace House Secondary School ambayo ujenzi wake utagharimu Tsh. Bil.8.7 sawa na dola za kimarekani milioni 8. mradi wa ujenzi Hospitali ya Rufaa, Arusha Lutheran Medical Centre ambayo ujenzi wake utagharimu dola za Kimarekani milioni 5.6 sawa na Tsh Bil 5.8
 
Ben

Ben usiseme pesa ya serikali, SEMA PESA ZA WANANCHI ,Serikali haina pesa,ingekuwa ina pesa nani angeihoji kwa matumizi yake?
 
Last edited by a moderator:
Mwanzo ilikuwa wametajwa sasa hivi wanazungumziwa

Mbona mazingaombwe yashaanza hata kabla watu hawaja kaa sawa?
 
Hakuna atakaye katwa mikono.
Kwa nini?
Kwa sababu Tanzania hatuna adhabu ya kukata mikono, Unless sentensi hiyo imebeba maana fasihi.

Haki na Sheria katika mahakama zetu zinatosha kuwabana.

Sivyo tuunde Mahakama Maalumu ya Wahujumu uchumi yenye Jopo la Majaji kutoka nchi mbali mbali zenye uzoefu wa kutia adabu Maharamia wa Kitaifa.
 
Kwenye GMT -5 Majina siyo yanazungumzwa zungumzwa... orodha itakuwa hewani.. pia tutaungana na Bw. Tundu Lissu ambaye atazungumzia mambo ya kisheria hususan suala la kuweza kumshtaki Rais aliyetoka madarakani kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani ambayo ni ya kiuhalifu....
 
Ben usiseme pesa ya serikali, SEMA PESA ZA WANANCHI ,Serikali haina pesa,ingekuwa ina pesa nani angeihoji kwa matumizi yake?

Basi hela zetu na babu zetu.Kwa vyovyote vile hakuna short kati kwa njia ya demokrasia na kwa utawala unaooongozwa under rule of law ndipo tutakapwerza kufanya kama walivyofanya wazambia kwa rais wao wa zamani Chiluba,au kama Ex-president wa Philipenes Joseph Estrada

Still we can do better,tuna imani sana kwani bado Mungu hajatutupa.We have a dream
 
Yeah,hapo ndipo tutakapofaidi matunda ya demokrasia ya kweli.Lakini kama wananchi wetu wataacha kuwa wasahaulifu tu
 
Kama majina yametajwa na Dr. Slaa kwanini tusubiri hiyo live yenu... publish name... story zingine baadaye!
 
Majina bado tu? Tunataka kuwajua hao mafisadi


It is about high time, wa-Tanzania tukaanza kuongea siasa ya kweli, kwa kuwasema wazi hao mafisadi na waliyoyafanya,

ndio maana mimi siku hizi situmii majina ya el na en sijui, nimeamua liwalo na liwe, ni kuwataja kwa majina yao ya kweli tu, maana either we are with them mafisadi, au we are not!

na kama we are not basi dawa ni Kumkoma Nyani Giladi Let Chip Fall Where They May! Liwalo na liwe enough!
 
mkjj,

Napena kuuliza hivi,

Kumekuwa na tuhuma nying dhidi ya serikali pamoja na taasisi zake lakini serikali imeendelea kuzipuuza au kutoa ahadi zisizo kuwa na ufanisi,na pale ambapo zimejibiwa majibu yake yamekuwa sio ya kuridhisha.

Je ni hatua gani viongozi wa upinzani pamoja na wanasheria wanaweza kuzichukua ili kurekebisha hali iliyopo.
 
Back
Top Bottom