List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mwanakijiji nilijua utataka kusikia data za Lowassa..
Lakini naona itakuwa muhimu Dr. Slaa akizungumzia mambo ya Mkapa pia...
 
Mwanakijiji,

Naomba umuulize ushiriki wa Patrick Rutabanzima aliekuwa waziri wa Nishati na Madini kwa kadiri nijuavyo alikuwa ni kiongozi safi na lijitahidi (bila mafanikio) kuzuia dili la IPTL.

Natanguliza shukrani.
 
Tumetajiwa Watu hawa na Mh. Slaa kuwa ndio Vigogo wa Ubadhirifu Tanzania,na kwa maelezo yake ni watu ambao wanapaswa kutoa majibu kwa Tuhuma zinazowakabili.Majina ni mazito na Mh.Slaa anaendelea kutoa somo Dhidi yao!!Naweka majina yao hapa Waungwana!

1. Dr. Daud Balali.
2. Andrew Chenge.
3. Basil Mramba.
4. Gray Mgonja.
5. Patrick Lutabanzibwa.
6. Nimrod Mkono.
7. Edward Lowassa.
8. Rostam Aziz.
9. Nazir Karamagi.
10. Benjamin Mkapa.
11. Jakaya M. Kikwete.

Sababu haijulikani,lakini list ipo kwenye mlolongo huo,naona Waheshimiwa marais wamewekwa mwisho!
 
It is about high time, wa-Tanzania tukaanza kuongea siasa ya kweli, kwa kuwasema wazi hao mafisadi na waliyoyafanya,

ndio maana mimi siku hizi situmii majina ya el na en sijui, nimeamua liwalo na liwe, ni kuwataja kwa majina yao ya kweli tu, maana either we are with them mafisadi, au we are not!

na kama we are not basi dawa ni Kumkoma Nyani Giladi Let Chip Fall Where They May! Liwalo na liwe enough!

mkjj,
napena kuuliza hivi,
kumekuwa na tuhuma nying dhidi ya serikali pamoja na taasisi zake lakini serikali imeendelea kuzipuuza au kutoa ahadi zisizo kuwa na ufanisi,na pale ambapo zimejibiwa majibu yake yamekuwa sio ya kuridhisha.
Je ni hatua gani viongozi wa upinzani pamoja na wanasheria wanaweza kuzichukua ili kurekebisha hali hiliyopo.

Mwanakijiji nilijua utataka kusikia data za Lowassa..
Lakini naona itakuwa muhimu Dr. Slaa akizungumzia mambo ya Mkapa pia...

Mazee hiyo itakuwa bab kubwa...
Sasa leo itabidi nianze mapema na hapa Alize naona imeisha so ngoja nikimbie liqor store...si unajua tena ndo mambo ya wikendi hayo

nikumbushe ile namba yetu

Kama majina yametajwa na Dr. Slaa kwa nini tusubiri hiyo live yenu... publish name... story zingine baadaye!

HIVI NYIE MBONA MNATIA AIBU?

MAJINA MWANZAO TULIAMBIWA YAMETAJWA THEN IKABADILIKA TUKAMBIWA YATAZUNGUMZIWA NOW TUNAAMBIWA TUSIKILIZE LIVE

HIVI 2007 KUNA MTU KWELI ANAWEZA AKAKAA CHINI KA KUMSIKILIZA MREMA ?


KAMA MAJINA YALIKWEPO THEN YANGETAJWA KWENYE POST YA KWANZA THEN TUANZE KUUULIZA MASWALI KUWA KUNA USHAHIDI GANI WA KUTHIBITISHA HAYO HALAFU SIE WENGINE TUTAWAPIGIA SIMU MARAFIKI ZETU MA LAWYER WACHANGAMKIE TENDA HIYO
 
Tumetajiwa Watu hawa na Mh. Slaa kuwa ndio Vigogo wa Ubadhirifu Tanzania,na kwa maelezo yake ni watu ambao wanapaswa kutoa majibu kwa Tuhuma zinazowakabili.Majina ni mazito na Mh.Slaa anaendelea kutoa somo Dhidi yao!!Naweka majina yao hapa Waungwana!

1;Dr. Daud Balali.
2;Andrew Chenge.
3;Basil Mramba.
4;Gray Mgonja.
5;Patrick Lutabanzibwa.
6;Nimrod Mkono.
7;Edward Lowassa.
8;Rostam Aziz.
9;Nazir Karamagi.
10;Benjamin Mkapa.
11;Jakaya M. Kikwete.

Sababu haijulikani,lakini list ipo kwenye mlolongo huo,naona Waheshimiwa marais wamewekwa mwisho!


MAJINA KAYATAJA NANI? NAAMINI WAPO AMBAO MMEREKODI HII INTERVIW SASA KILICHOBAKI TUNATAKA USHAHIDI THEN TUITE MA LAWYERS
 
Mheshimiwa Mkjj ukizungumza na Tundu Lissu muulize swala la Mkataba wa Madini wa Kahama Minning uliotiwa saini na Muungwana mwaka 1996 ambao uliwaacha wananchi wa Bulyankulu kufukiwa kwenye migodi na karibu watu 1000 kuharibiwa makazi yao na kutopewa fidia mpaka leo!!
 
MAJINA KAYATAJA NANI? NAAMINI WAPO AMBAO MMEREKODI HII INTERVIW SASA KILICHOBAKI TUNATAKA USHAHIDI THEN TUITE MA LAWYERS
Sikiliza LIVE kwenye Bongo Radio utamsikia mwenyewe Dr Slaa akiongelea kuhusu hii ishu.
 
Swali kwa Lissu,je tunaweza kuwashitaki hawaviongozi wote,je wakishitakiwa wanaweza kukaa pembeni mpaka mahamuzi ya mahakama yatakapo tolewa.
 
Sikiliza LIVE kwenye Bongo Radio utamsikia mwenyewe Dr Slaa akiongelea kuhusu hii ishu.

Kumbe wewe unasubiri ushahidi hapa? Hii ni lugha ya akina Mkapa kwa kuwa wanajua jinsi ilivyovigumu kuwapa ushahidi kabla hawajafa. Hata hivyo, ni rahisi kugundua kuwa wameiba na vielelezoi vipo. Kumbuka kuwa vielelezo hivyo, kisheria, siyolazima viwe ushahidi. Hapo ndipo wanapoponea. Ukweli unabaki pale pale...ni mafisadi.
 
unasema Majina Kayataja Nini!? Naamini Wapo Ambao Mmerekodi Hii Interviw Sasa Kilichobaki Tunataka Ushahidi Then Tuite Ma Lawyers

Kweli Washahili Hatukosi La Kukosoa.suppose Slaa Asingetaja Majina,je Usinge-demand Awataje Wahusika?au Ungependa Iwe Ule Mtindo Wa Uhuru Na Mzalendo Wa Kusema "kigogo Flani" Wa "wizara Flani" (majina Tunayo)?
 
Swali zuri katibu Tarafa,lakini kwani katiba yetu inasemaje kama tunakosa Imani na Viongozi wakuu wa serikali waliopo Madarakani?Sina ufahamu mzuri na mambo ya katiba,lakini naona serikali kwa kupitia Viongozi wake wakuu Rais na Waziri Mkuu wanatuhumiwa kwa ubadhirifu,Je! ni kweli kwamba serikali inabidi ijiuzulu!!Kwa yeyote mwenye Uelewa naomba ufafanuzi kwa hilo.
 
Makubwa haya, hata muungwana yupo?

Nchi za Afrika tukate tamaa ya kuendelea kama watu ambao wana mishahara na marupurupu makubwa kiasi hicho nbado wanaongoza kwa ufisadi?

Afadhali niendelee na kibarua changu ASDA, angalau ni pesa nazipata kwa nguvu zangu.

"Mtaji wa maskini ni nguvu zako mwenyewe"
 
Hata sielewi implication yake...backlash, backfire, hatua madhubuti zaidi; au itaishia kuwa soga tu.
 
Naona wala rushwa wanaingilia kati matangazo,hawataki tujue kinachoendelea
 
Spoila acha masihara.Kwenye digital age hii tulonayo bado unataka kitu cha jana ukisikie keshokutwa?You must be kidding!!!

Ahhh mimi tatizo langu ni kuwa MWANAKIJIJI sasa hivi anajulikana DUNIA NZIMA na redio yake ya DETRIOUT sasa kulikuwa na umuhimu gani kufanya Interview kuhutumia vifaa vya hawa mabitoz wa CHICAGO?

Kwani inaonekana kuwa tunayeyushana na pili interview INAPOTEA POTEA na tatu kama kweli MWANA KIJIJI YUKO SERIOUS NA MAMBO HAYA KWA NINI ASICHUNE CREDIT CARD ANUNUE MITAMBO YA KISASA ZAIDI BADALA YA KUTULETEA INTERVIEW ZA AJABU AJABU

I AM SORRY IN A DIGITAL AGE HIZI MISHAP HAZINA MPANGO

MIMI MWANAKIJIJI HUWA SIKUBALIANI NAYE LAKINI AKIPITISHA HARAMBEE YA KUNUNUA MTAMBO MPYA NIKO TAYARI KUMSUPPORT KWA HALI NA MALI.
 
Back
Top Bottom