Lissu, Zitto, Polepole na Nderakindo kukutana kujadili Vipaumbele, Utendaji na Siasa za Tanzania

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Sauti za Wananchi kama ilivyo ada inakuletea matokeo mengine ya utafiti wake unahusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini. Utafiti huu utakuletea data kutoka kwa wananchi zinazowakilisha nchi nzima kuhusu Vipaumbele vyetu kama taifa, Utendaji na Siasa.

Ripoti hiyo ambayo itazinduliwa Siku ya Alhamisi wiki ijayo tarehe 15.06.2017 kuanzia saa 5 asubuhi hadi 7 mchana pale Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na chuo cha IFM), itabainisha maoni ya wananchi. Je wananchi wana maoni gani kuhusu vipaumbele vya Serikali, utendaji wake na siasa nchini?

Wazungumzaji waalikwa watakuwa ni

1. Nderakindo Keesy - NCCR
2. Zitto Kabwe - ACT
3. Tundu Lissu - CHADEMA
4. Humphrey Polepole - CCM

JamiiForums itakuletea uzinduzi huo live! Usikose.

DBtW47sWAAAIdi7.jpg
 
Hakuna haja ya kujisumbua
Niwazi kuwa tukio hilo litafutwa kwa amri ya Polisi na kabla ya hapo Humphrey Polepole atatoa tamko la kutohusika na hataweza kuhudhuria
 
Sauti za Wananchi kama ilivyo ada inakuletea matokeo mengine ya utafiti wake unahusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini. Utafiti huu utakuletea data kutoka kwa wananchi zinazowakilisha nchi nzima kuhusu Vipaumbele vyetu kama taifa, Utendaji na Siasa.

Ripoti hiyo ambayo itazinduliwa Siku ya Alhamisi wiki ijayo tarehe 15.06.2017 kuanzia saa 5 asubuhi hadi 7 mchana pale Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na chuo cha IFM), itabainisha maoni ya wananchi. Je wananchi wana maoni gani kuhusu vipaumbele vya Serikali, utendaji wake na siasa nchini?

Wazungumzaji waalikwa watakuwa ni

1. Nderakindo Keesy - NCCR
2. Zitto Kabwe - ACT
3. Tundu Lissu - CHADEMA
4. Humphrey Polepole - CCM

JamiiForums itakuletea uzinduzi huo live! Usikose.

View attachment 521682
Asante kwa taarifa, tutakaribia!.
Ila pia hizi ripoti za Twaweza na hao wanaohojiwa, leaves much to be desired.
UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila ...

Paskali
 
Natabiri suala hilo kusitishwa kwa kuwa Lissu na Zitto watakuwepo. Hawa hawatakiwi maana wanahoji kiundani. Anatakiwa mtu kama Dr. Bana ambaye nimemsikia leo akiunga mkono bajeti lakini analalamikia utekelezaji wake kisa eti anadsi miaka minne hajalipwa!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom