Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua Kiingereza? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka Kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu. We want to make Tanzania great nation, Kiswahili ni ajenda kuu.
Kwanza wewe umetawaliwa na chuki binafsi dhidi ya Lissu, possibly due to political ideology au misimamo yake. Hivyo badala ya kuiangalia na kuipima hoja yake wewe inapambana na chuki dhidi yake. Assume for the moment, hiyo hoja kaizungumza JPM au Kikwete halafu ipime...
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani Muingereza anaongea Kiswahili kama Mtanzania?
Hajakwambia anataka ,anakwambia tuwe na lugha moja ,ka kuswshili iwe kiswahili au ka kizungu iwe kizungu,India chuki inakufanya usielewe vizuri
 
Tundu Lissu amesema haya kuhusu lugha ya kufundishia:

Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything.

Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha.

Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia.

Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Lieu hajajiandaa kuwa rais
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?
Na wewe ni mzazi wa familia hapo mtaani ?

Mbona majibu ya swali lako yapo wazii sana kwa mtu mwenye kushughulisha ubongo wake.
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?
Kingereza siyo Yes and no let mdahako live na usisahau kulet na pain killer K Vant na Adam energy
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?
Hajajiona kasema wengi hawajui na siyo mbaya maana siyo lugha yetu,tujitahidi ni sawa MTU anaposema Tanzania hapa mpira hakuna na wakati yeye ni mtanzania pia,kiingereza ni juhudi ya MTU binafsi mkuu.
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?

Kama nilisoma sawasawa uzi ule, alisema kuna BAADHI ya majaji na mawakili.... kitu ambacho ni kweli.
 
Sina jibu la kitalaamu katika hili lakini hakuna ajabu yoyote ikiwa Lissu yupo more fluent in English kulinganisha na hao wengine hata kama wote wamesoma shule zile zile na kukulia mazingira yale yale!

Nina kila sababu ya kuamini watu tunatofautiana uwezo wetu wa ku-master lugha ya kigeni/ second language.

Mama yangu kwa mfano... huyu hakupata bahati ya elimu, lakini anakupigia broken ya Malkia!

Anachonishangaza zaidi ni uwezo wake wa kuongea lugha za makabila matatu wakati maisha yake karibu yote yupo Dar es salaam, na wala hajawahi kuishi kwenye mikoa ya hayo makabila mengine mawili!

Kutokana na makuzi yake, ananishangaza hata ambavyo bado anaiweza lugha ya kabila lake wakati hajaishi sana kule! And on top of that, hata Bush kwetu ni very rare ukute watu wanaongea kilugha... labda majumbani kwao kwa baadhi; but still my mom anaongea kilugha!

Nililazimika siku moja kumuuliza ni namna ana-manage kuongea hizo lugha wakati hajaishi hayo mazingira... hata mwenyewe nikaona kama anajishangaa!

I bet angekuwa ameenda shule yule, basi angekuwa na uwezo wa ku-master lugha za mataifa kadhaa endapo angeamua kujifunza!

But also REMEMBER, according to Howard Gardner na theory yake ya Multiple Intelligences, out of 8 intelligences in Multiple Intelligence Theory, moja wapo ni Linguistic Intelligence!

So, if Gardner is true, na TL kasema kweli kuhusu hao majaji, then tunaweza ku-conclude kwamba Tundu Lissu has HIGHER Linguistic Intelligence kulinganisha na hao majaji!
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?
Exactly, ndiyo maana tunasema Lisu is extraordinary intelligent! University of Warwick Law Professors walisema wamepita wanafunzi wengi hapa, lkn huyu ni exceptionally intelligent!
 
Amesema Majaji na Mawakili wa Tanzania hawajui Kiingereza na kwamba wakiongea anaweza kuingia chini ya uvungu kwa aibu, ina maana yeye anakijua hicho kiingereza, sasa kakijulia wapi?

Kazaliwa, kakulia, kasomea hapa hapa Bongo kuanzia msingi mpaka Chuo kikuu, kama hao wengine, sasa iweje ajione anajua kuliko wengine?
Sio majaji tu hata huyu bwana hapa akiongea utajificha mbali kabisa inasikitisha.
Sikiliza kidogo uone kwanini Lissu ana point ya msingi. Aibu kishenzi.
 
Attachments

  • IMG_5105.MP4
    690.2 KB
Mpaka sasa list yangu ya wenye PhD wasiojua kingreza inasoma 2 na naendelea kufanya utafiti kuwabaini PhD holders wengine lugha gongana.
 
Ushajiuliza pia na anayepata sifuri kwenye mtihani na anayepata 100 darasa hilo hilo na mazingira hayo hayo?
 
Back
Top Bottom