Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Kiukweli sijuagi hata anaongea lugha gani yule mzee!

Mara nitawabomolesha, mara nitawafanyizia maendeleo....... fontifedi...kirometa...

Sielewagi hata anachoongea.
Umenifanya nicheke kwa nguvu wananishangaa!🤣🤣🤣
 
Mbona hamuelewi nyie MaCCM..wachina lugha yao ya kufundishia ni kichina...na sisi tuamue iwe kiswahili au English..mfano ukiwa Ulaya ni United Kingdom tu ndio wanaotumia kiingereza...nchi nyingine zote wanatumia lugha zao...
Acha uongo China kwenye elimu ya juu wanafundisha kwa kutumia Kiingereza ndiyo maana Watz na Waafrika wanasoma huko!! Jamani za kuambiwa changanga na zako!!
 
kiswahili kikue SADC itumie hii lugha, rubbish? lugha ya kingereza ni lugha ya kidunia,inatamkwa na nchi karibia zote duniani,kwa nini mjilimit na opportunities za SADC.. wakati mngeweza ku enjoy..dunia
Kuwa na heshima kwa Lugha yetu tafadhali.....
Usitumie hilo neno ni kulitusi taifa letu.
 
Ninamaanisha uwe na viwanda vingi vyenye ufanisi na bidhaa zake uandike kwa kiswahili na uuze kwa wingi nje
 
Mimi wangu wanasoma kwa Kiingereza la kwanza mpaka univ.Sasa tuachane na kiswahili.
Hapa tu huwezi hata kuandika sentensi moja ya kiingereza! Sisi tunataka tuendelee na kiswahili chetu ndiyo maana sasa tumeamua kitumike Afrika na baadae iwe lugha ya bara la Afrika sasa huyo msaliti anataka kuturudisha nyuma atawapata wajinga wenzake!! Chadema wekeni kwenye ilani yenu !
 
Hapa tu huwezi hata kuandika sentensi moja ya kiingereza! Sisi tunataka tuendelee na kiswahili chetu ndiyo maana sasa tumeamua kitumike Afrika na baadae iwe lugha ya bara la Afrika sasa huyo msaliti anataka kuturudisha nyuma atawapata wajinga wenzake!! Chadema wekeni kwenye ilani yenu !
Kinge nilipata Msonge form four ,halafu nishindwe kuandika sentensi ?SASA WHY WATOTO WENU MNAWAPELEKA FEZA ENGLISH ACADEMY ?
 
Kwenye lugha kuna ukakasi, watawala wetu wa mwisho walikuwa Waingereza sasa Kiswahili kilitokea wapi!!!
 
Mkuu hivi umeelewa anachosema Tundu lisu au umekurupuka kujibu tu.
Nadhani hajaelewa. Hii ndiyo shida ya kukurupuka kujibu kabla ya kutulia na kutafakari. Ni kama vile inavyokuwa katika mazungumzo.
Watu wengi si wasikilizaji wazuri kwa kuwa wakati wewe unazungumza yeye anafikiria jinsi atakavyokujibu, hivyo anakuwa hakusikilizi. Na wakati mwingine hangoji hadi umalize kuzungumza ndipo afuatie, yeye atakukatisha kabla hata hujamaliza.

Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri na watu na pia kujenga hoja zako vizuri unapokuwa kwenye mazungumzo na watu wengine, basi jifunze kutumia muda mwingi kusikiliza kuliko kuongea.
 
kiswahili kikue SADC itumie hii lugha, rubbish?
Cha ajabu mwenyekiti wa SADC hajui Kiswahili, achilia mbali kujua Kiswahili fasaha.

Halafu sijui kwanini wanaoking'ang'ania Kiswahili huwa hawajui Kuzungumza Kiswahili.

It is a very unfortunate coincidence!.

Anasema tukikuze Kiswahili lakini ghafla ukigeuka anakwambia "nitakufanyizia maendeleo".

Hmmmmmm!!!!
 
Kinge nilipata Msonge form four ,halafu nishindwe kuandika sentensi ?SASA WHY WATOTO WENU MNAWAPELEKA FEZA ENGLISH ACADEMY ?
Kwa sababu sera yetu TZ inaruhusu sasa huyu msaliti Lissu anataka tuwe na lugha moja ya mabwana zake ya Kiingereza!! Huyu atausikia tu Urais.
 
Kwa nini uwe bubu labda kama hujiamini? Wachina wanakuja hapa nchini hawajui kiingereza hata kiswahili lakini baada ya miezi michache tu wanaongea kiswahili. Wanafunzi kule Soweto walipambana kupinga kutumia Lugha ya Makaburu mashuleni ingekuwa ni nyinyi wanasaccos mngelikubali tu kwa sababu ya kutojitambua. Jua kuwa unapozungumza kuhusu utamaduni ni pamoja na lugha yako. Wanasema mdharau utamaduni wake ni mshenzi sasa ukipata mgombea urais anapigania lugha ya wengine huyo hafai kuwa kiongozi katika jamii hiyo!! Hakupashwa kabisa kuongelea hilo wakati huu!!
Hujui lolote wewe !!. Hata Mwl Nyerere alijilaumu kukitupa English . Aliyoiita mwenyewe kama "KISWAHILI CHA DUNIA".

Kinachowasumbua ninyi ni uzalendo uchwara.
 
Mbona hamuelewi nyie MaCCM..wachina lugha yao ya kufundishia ni kichina...na sisi tuamue iwe kiswahili au English..mfano ukiwa Ulaya ni United Kingdom tu ndio wanaotumia kiingereza...nchi nyingine zote wanatumia lugha zao...
Kama unajua hivyo basi huyo kibaraka wenu hasiwacheke wale wanaoongea kiingereza vibaya maana ata hao wazungu mnao wanyenyekea wakiongea kiswahili kibovu hakuna anaye wacheka. Sana sana mnajipongeza kuwa mzungu amejitahidi.
 
Unajua kuwa sheria zetu na hata hukumu zetu ni English tupu ?! Barua zetu za ki serikali na mawasiliano na dunia ni only in English !!
Ndugu hili nakukatalia kabisa, tena nakataa huku napiga kelele.
In primary courts official language ni swahili. Kuanzia Dc na kwenda mbele ni English

Kwa ufupi official Languages ni swahili na Emglish. Lakini je ni lazima mtanzania atamke English kama muingereza?
 
Hawa mataga ni wapumbavu Sana kazi yao ni kupinga kila Jambo
Bila jet lee ,jack chan, don yen kucheza muvi na kuongea kingereza kizuri ungewajulia wapi, asilimia 10 ya wachina wote wanaongea kingereza
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation, kiswahili ni ajenda kuu
Duh Mheshimiwa umeelewa Kamanda Lissu anasema nini!
 
Back
Top Bottom