Lissu: Wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote kwa mauaji Morogoro

sheria zifuate ili kuondoa viongozi pandikizi wa ccm wanaofanya kazi kwa remote wakitegemea kulinda masilahi ya walio wateua au kuwapa kazi
 
Inasikitisha sana nikiangalia jinsi hii picha inadevelop, chunga sana tusije fika walikofika wenzetu huko libya, syria nk maanake watu wanahasira sana aisee.
 
Kuna mijitu humu inakituhumu CDM kuhusika na mauaji ya morogoro ,ivi na yale mabomu na hao polisi nao ni CDM?
 
images
images


Tundu Lisu (kushoto)VS Kamanda Shilogile (Kulia)
LISSU AAHIDI KUMFUATA SHILOGILE

Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Haki na Sheria Chadema, alisema suala la kuandamana halijawahi kuwa kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifo, kama ilivyotokea kwa kijana aliyeuawa na polisi.

Alisema hakuna damu ya Mtanzania aliyeuliwa bure kuwa itasahaulika, hata kama hao wanaowaamuru polisi kwa kudhani wataishi milele.

Alieleza kuwa
wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote alipo iwe amevaa sare au amevua kwa ajili ya kuulezea umma wa Watanzania kwa nini alimuuwa Ally Nzona.

"Tunawaambia tutawafuata popote walipo watuambie kwa nini wameamua kumwaga damu ya Watanzania, vilio vyetu havitapita hivi hivi leo na hata kesho," alisema Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

Tundu Lisu Asisitiza:
Lissu aliongeza kuwa ni wakati wa wakazi wa Morogoro kuwaanda viongozi wao watakaosimama mwaka 2015, kwa kuwa na vitendea kazi vya uhakika, kwa kile alichoeleza kazi ya ukombozi inahitaji kujitolea kwa hali na mali.


Wana JF,

Hawa viongozi wa Police wakubwa hawa wana philosophy gani kuhusu maandamano semina ganai wanapewa kuhusu maandamano?

Haiwezekani kiongozi mkubwa wa police anashindwa kujenga hoja ya kuwashauli viongozi wakubwa hawa wa vyama au wanasiasa kuwa mkakati wenu wa kuandamana tungependelea uwe hivi matokeo yake wao ni kukataaaa kila mara na kuvuruga maandamano.

Wana Inteligensia gani yao ya kuweza kutabili kesho kuhusu maandamano? Hawa Police wana kitengo cha siasa au diplomasia ndani ya jeshi la police na kama kipo kazi yake ni nini?

Kuna tatizo kubwa la Jeshi letu la Police kukataaa katu kuwa ustaarabu wa watanzania umebadilika na umekuwa wanajua lipi jema na lipi si jema leo mwataka kuifanya nchi iwe kipindi cha ubaguzi, Si tulidai UHURU sasa kwanini tusielimishane jinsi ya kutumia uhuru wetu kwa pammoja na si kwamabavu, Vyombo husika ndio muna wajibu wa kuwaelimisha hawa wakubwa wanao toa order jinsi gani ya kuweka amani ndani ya nchi na kuitunza matokeo yake mwataka wananchi wawe waoga kwa kudai haki zao kwa kulazimishwa kukubali AMANI isiyo na HAKI.


My Take;


Viongozi hawa wakubwa wa Police wanashusha hadhi ya Jeshi hili la Police kwa kupenda kufwata Order kutoka Juu hivi huyo juu ndio nani IKULU,SERIKALI,WIZARA YA MAMBO YA NDANI?

Kwa umakini tuu ukiangalia kwanini kila maandamano hutokea fujo ni kwa ajili ya kigeugeo cha kauli za Police watakubali maandamano then masaa sita kabla ya maandamano wanakupa sababu na hakuna maandamano kwa kutumia vigezo vya sheria. na ndipo hapo chanzo cha machafuko kuanza baina ya Police na waandamanaji na link of information toka jeshi la police zinakuwa nyingi, Yet hawa wakubwa wa police hawajifunzi kuwa hata ndani ya jeshi lao la police kuna baadhi yao wahafurahishi na mwenendo mzima wa maamuzi yanavyo chukuliwa na wakubwa wao.

"Umaskini wa mawazo /Kufikili ni umaskini mbaya kuliko umaskini wowote duniani" by Mwl.JK Nyerere-1995 MAY MOSI - MBEYA
 
Mikutano yenu ni kila siku,mbona kwingine hakupigwa risasi mtu?

majebere,

Usiwe kama juha wewe. Chama hakiwezi kujijenga na kujiimarisha bila mikutano ya kueleza sera na mikakati yake ya kuendesha nchi au kushika dola. Hata hao CCM wanafanya mikutano kila siku,tatizo lao kwa sasa hawana mvuto hata wakifanya mikutano yao hakuna anayehudhuria labda wamkokote kwa lazima kwa kuwabeba kwa mijifuso.

Nina uhakika baada ya CDM kuondoka Morogoro hawa Magamba nao watapeleka mikutano yao kule walikopita CDM eti kufuta nyayo za CDM.Kitu cha kushangaza ni pale unapoona hakuna polisi atakayezuia mikutano yao maana kila mtu anajua kuwa CCM na POLISI wanaunda kitu kimoja kinaitwa POLICCM!

Akili ya kawaida tu itahoji ni kwanini mikutano ya CDM tu ndiyo inayozuiwa ilhali ya CCM inaachwa iendelee kwa amani?Je,ni mkutano mingapi ya CCM watu wamewahi kupigwa mabomu na risasi za moto kama inavyofanyika kwa mikutano ya CDM???

Swali kwa Rais Kiwete: Hivi kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015 mtawaambia nini Watanzania ili kuwashawishi wawape ridhaa ya kuwaongoza?? Maana inavyoelekea kwa mtindo huu mpaka 2015 sijui wewe na Polisi wako mtakuwa mmeua Watanzania wangapi? Kama Rais Kiwete una busara basi lazima ukomesha huu udhalimu na ushenzi wa Jeshi lenu la Polisi. Usipofanya hivi basi ujue kabisa kushinda kwa CCM hata kwa aslimia ndogo tu itakuwa ni ndoto!Rejea matokeo ya Chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru Mashariki. That is just a trail,the true movie is coming the year 2015!
 
Lissu anatafuta sifa tu,hawa wanafurahia raia akiuawa ndio wanapo patia nafasi ya kujijenga kisiasa. Alikua wapi wakati yule kijana wa CCM alieuawa singida kwenye mkutano wa CDM
Wapi na wapi, kwenye starehe tingatinga limefikaje?
 
Rafiki yangu wameunda tume kutafuna allowances kwa sababu ni yao wenyewe kwa manufaa yao wenyewe. God help us. Unaua halafu unaunda tume, hizi pesa ziko wapi Tanzania??? Tusijenge madarasa kwa ajili ya watoto wetu jamani????
 
Back
Top Bottom