Lissu: Wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote kwa mauaji Morogoro

Mimi nashuri mfanyie fujo zenu nje ya miji, mnatesa watu bure. Kila maadamano yenu lazima yafanyike sehemu watu wana shughuli zao.

images


Jaribu kutoa kauli yenye kuwa na mizani, kwani waliosababisha mateso ya mtoto huyu ni viongozi wa Chadema au Polisi? Polisi wangekuwa watulivu hayo yangetokea? Mbona mkutano ulianza na kuisha kwa amani?
 
images
images


Tundu Lisu (kushoto)VS Kamanda Shilogile (Kulia)

LISSU AAHIDI KUMFUATA SHILOGILE

Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Haki na Sheria Chadema, alisema suala la kuandamana halijawahi kuwa kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifo, kama ilivyotokea kwa kijana aliyeuawa na polisi.

Alisema hakuna damu ya Mtanzania aliyeuliwa bure kuwa itasahaulika, hata kama hao wanaowaamuru polisi kwa kudhani wataishi milele.

Alieleza kuwa
wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote alipo iwe amevaa sare au amevua kwa ajili ya kuulezea umma wa Watanzania kwa nini alimuuwa Ally Nzona.

“Tunawaambia tutawafuata popote walipo watuambie kwa nini wameamua kumwaga damu ya Watanzania, vilio vyetu havitapita hivi hivi leo na hata kesho,” alisema Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

Sisi tuna habari za kiitelijensia kuwa huyo kauliwa na nyinyi wenyewe, msitake kuzuga watu.
 
images


Jaribu kutoa kauli yenye kuwa na mizani, kwani waliosababisha mateso ya mtoto huyu ni viongozi wa Chadema au Polisi? Polisi wangekuwa watulivu hayo yangetokea? Mbona mkutano ulianza na kuisha kwa amani?
Mikutano yenu ni kila siku,mbona kwingine hakupigwa risasi mtu?
 
Mikutano yenu ni kila siku,mbona kwingine hakupigwa risasi mtu?

We mahindi sijui mabichi au makavu, mikutano haikuhusu wewe inawahusu wakereketwa wanaohudhuria kutokana na uhuru wa kila raia kuamua upande anaoona unamfaa ndo demokrasia, unachofanya wewe ni kufikiria demokrasia lazima mtu awe upande wako. Ipo siku utageukia unakofikiria si kwako kwa kuwa ni kawaida binadamu kujigeuza kama kinyonga kutegemeana na mazingira kwa malengo ya kujilinda.
 
Sisi tuna habari za kiitelijensia kuwa huyo kauliwa na nyinyi wenyewe, msitake kuzuga watu.


moro%20mabomu.jpg

Dalili za gari kuwa na usukani mbovu ni kuyumba huku na kule, ukishaona hivyo kwa usalama bora dandia gari jingine, kwani huwezi kujua gari hilo lenye usukani mbovu hatima yake litakufikisha wapi.

Wasio na upeo wa kutosha katika kutambua usukani mbovu wa gari walilodandia watabaki kushabikia gari linapoyumba huku na kule kwa wimbo ufuatao;
Dereva chechema chechema na gariX2 tupate kuona ufundi wa gari X2. Hatimaye majuto ni mjukuu.
 
Nchi ina mambo ya ajabu sana hii,eti Emmanuel Nchimbi ni waziri wa wizara nyeti kama ya mambo ya ndani!no wonder Mwalimu katika miaka ile ya 199's alisingizia kigezo cha umri kumbe alishajionea mbali

Kweli kabisa hii wizara ni nyeti sana, angekuwa wazir mwenye akili na hekima asingezungumza maneno mepesi namna ile na kufanya Conclusion za kitoto then anasema anaunda tume kuchunguza, wakachunguze nini na wakati ameshaconclude..??? Nyerere alijua hayo, em niambie asingemkataa JK 1995 ingekuwaje kama angetawala time ile??
 
Too sad, Waziri na serikali imekaa kimya kana kwamba hakukutokea kitu, ni aibu ilioje jamani nchi hii?
Umemsikia waziri wa CCM alivyozungumza? Aibu tupu, full of prejudiced information with poor intelligence report. Eti askari walikuwa mita 300 kutoka eneo la tukio. Wakati watu wameona yote yaliyotokea. Wasije wakamkamata msomali mmoja kanisani wakamtuhumu.
 
Kama Morogoro watu wanapigwa na SMG, Sometimes huwa najiuliza hivi siku watanzania wakiandamano kwenda magogoni, watatumia silaha gani kuwadhibiti?
 
......mungu akamuuliza kaini, "kaini kaini... Ndugu yako habili yuko wapi? ... Kaini akajibu kwani mimi ni mlinzi wake.... Mungu akasema " tazama damu ya ndugu yako habili yanililia toka udongoni..
Na mungu anakueleza: Shilogile shilogile shilogile, tazama damu ya ndugu yako ally nzona yanililia toka udongoni,,,,.... Mungu anakuuliza tena kwa nini haujamlinda ndugu yako habili nawe umemuua? Shlogile ndugu yako amepumzika udongoni akiacha majonzi kwa wazazi na wote waliotegemea mkate toka kwake. Hakika roho yako na itaabike milele usipate amani ya kula na kunywa hadi roho kuu ya ukatili iweze kukutoka na kukufanya mwana wa mungu tena. Bwana alipokuumba alikupulizia pumzi ya uhai ndani yako, kwani nawe kuruhusu ndugu yako afe? Shilogile ndugu yangu wajibika kwa kujiuzulu cheo chako ili damu hii isikumwagikie wewe na uzao wako. Na usipowajibika damu ya ndugu yako all nzona na iwe juu yako na uzao wako wote.
Kumbuka tena neno hili:mungu akamuuliza kaini: Ndugu yako yuko wapi? Tazama damu ya ndugu yako inanililia toka udongoni.
 
Umemsikia waziri wa CCM alivyozungumza? Aibu tupu, full of prejudiced information with poor intelligence report. Eti askari walikuwa mita 300 kutoka eneo la tukio. Wakati watu wameona yote yaliyotokea. Wasije wakamkamata msomali mmoja kanisani wakamtuhumu.

Hata kama wangekuwa mita zaidi ya 500 ni kosa kwa polisi kutumia silaha za moto kwa raia wasiokuwa na silaha au kuwa hatari kwa usalama wao. Ingawa kauli hiyo ya Waziri inakinzana na emerge ambazo zimesambaa kila kona ya vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, na kwa vyo vyote anajenga utetezi unaokinzana na ukweli.

Waziri mwenyewe ni yupi? Ni yule aliyekimbia na sanduku la kura katika uchaguzi wa Meya Songea?
Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura wakati madiwani wakigombana

Nimeonyesha mara kadhaa hapa askari polisi tanzania kutumia silaha kazi za kivita katika matukio kama haya hata katika kuongoza misafara ambayo haina hatari kwa usalama wao na wawanachi. Polisi kwa sheria na taratibu za kimataifa hutumia silaha za kiwango cha masafa mafupi sana silaha ambazo ni
pistol ambazo trigger yake hurusha risasi umbali mfupi sana, ni mita kadhaa tu kwa tahadhari ya kujilinda tu si kujeruhi raia.
 
Cdm waliwafanya nini makamanda Arusha, Tarime, Mbeya na Songea?
avatar118_8.gif

Maisha ya wapigania uhuru na haki si kama kuvaa sare zake, bali ni kila siku kuwa na ubunifu wa kitu kipya ambacho kwa kupima utaona kinaweza kukutengenezea mazingira ya kupata haki yako. Pale unapoona hata unayemtegemea kuwa ndiye mlinda haki yako anazidi kukunyang'anya hata kidogo kilichobakia na zaidi kuhatarisha uhai ambao ni zawadi pekee toka kila mmoja wetu toka kwa Muumba wetu, basi hakuna shaka unapata msukumo wa kuchemsha bongo na kutafuta njia nyingine mbadala ambayo itakupa haki unayoitaka.

Kesi ya Igunga ya kutengua matokeo ya ubunge wa mteule wa CCM Bwana Kafumu, hukumu ile ya hakimu wa Kanda ya Tabora imefunua jambo jipya ambalo linawapa moyo sasa Chadema kutumia haki za kisheria kupitia mhimili wa Mahakama kujenga utetezi wa kudai haki zinazokandamizwa daima.

Kila kitu na wakati wake, Mzee Mwanakijiji hata unapolima shamba ukiona aina fulani ya mbegu haikupi matunda unayotegemea itakubidi ufanye utafiti wa kupata mbegu nyingie itakayo kuletea mavuno unayotazamia.
avatar118_8.gif
 
Me nafurahi manake watu wakisikia , wanazidisha kuingiwa hofu na cdm , wameanza kujuwa malengo yao.
 
images
483695089.jpg


pamoja na vitisho vyote hivyo na mauaji ya polisi lakini bado mkutano ulifana na kujaza watu nyomi dalili ya njaa ya uongozi bora waliyo nayo wananchi wa tanzania.

naona rangi nyekundu nyingi,ni mashabiki wa simba au nyekundu inamaanishanini?
 
Kinacho nishangaza ccm wamesha sambaza propaganda kuwa chadema ni chama cha wakristo lakini polisiccm haohao kila siku wanaua wanachama wa chadema walioko kwenye maandamano ambao ambao niwa islamu!

Angalizo; sijasema wauwawe na wakristo! Hapana najaribu kuona jinsi ccm na polisi wanavyoua raia halafu baadae wanasingizia kuwa chama fulani nicha kidini! Silly leadership!


Kaka nimekubali kumbe ndugu zetu mnawaelewa hawa mabwepande vizuri. Wito wangu kwa wakristo,waislam na wasio na madhehebu tusikubali hawa Magamba watugawe kwa misingi ya imani zetu eti kwa sababu ya uzembe wao wa kutuletea mazingira bora ya maisha. tutamueleza ukweli kiongozi mkuu wa nchi yetu kuhusu madhaifu yake km ilivyokwa kwa JK bila kujali imani yake . Awe mkiristo ,mwislam au asiye na dini kama Kingunge lakini kamwe tusionyoosheane vidole kwa dini zetu nawaomba ndugu zanguni wana jamvi. sis sote ni watanzania na desturi zetu utengano ni sumu kwa ustawi wetu na vizazi vyetu. Tunacheka pamoja,tumeoleana,tunasaidia ktk shida na raha sasa iweje tutenganishwe na hawa mabwepande. Walianza na CUF wakafanikiwa lakini safari hii tumeshawaelewa hira zao tusikubali kamwe
 
Back
Top Bottom