Lissu: Wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote kwa mauaji Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu: Wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote kwa mauaji Morogoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Tundu Lisu (kushoto)VS Kamanda Shilogile (Kulia)

  LISSU AAHIDI KUMFUATA SHILOGILE

  Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Haki na Sheria Chadema, alisema suala la kuandamana halijawahi kuwa kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifo, kama ilivyotokea kwa kijana aliyeuawa na polisi.

  Alisema hakuna damu ya Mtanzania aliyeuliwa bure kuwa itasahaulika, hata kama hao wanaowaamuru polisi kwa kudhani wataishi milele.

  Alieleza kuwa
  wanasheria watamfuata Kamanda Shilogile popote alipo iwe amevaa sare au amevua kwa ajili ya kuulezea umma wa Watanzania kwa nini alimuuwa Ally Nzona.

  "Tunawaambia tutawafuata popote walipo watuambie kwa nini wameamua kumwaga damu ya Watanzania, vilio vyetu havitapita hivi hivi leo na hata kesho," alisema Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

  Tundu Lisu Asisitiza:
  Lissu aliongeza kuwa ni wakati wa wakazi wa Morogoro kuwaanda viongozi wao watakaosimama mwaka 2015, kwa kuwa na vitendea kazi vya uhakika, kwa kile alichoeleza kazi ya ukombozi inahitaji kujitolea kwa hali na mali.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Damu ya kijana Nzona itakuwa ikimlilia huyo Kamanda milele!!
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kila chenye mwanzo kina Mwisho, CCM na Policcm jua lina karibia kuzama.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  What goes around comes around!!!!!
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Shilogile amefanya kazi aliyotumwa na Boss wake
   
 6. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Wadai mlioko Morogoro Tunaomba ratiba ya mazishi ya Ally Zonna.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uamuzi wa Tundu Lisu kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makamanda wa polisi wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kupindisha sheria ni wa muhimu na busara sana, kwani kilichofanyika ni uvunjaji wa sheria uliofanywa na polisi kuua na kujeruhi watu ambao hawakuwa na silaha wala dalili zo zote wa kuwadhuru. Badala ya kuwalinda na kuyaongoza maandamano wao wanasababisha mitafaruku, kujeruhi na kuua kinyume cha maadili ya kazi zao.

  Tunahitaji wanasheria mashuhuri kukingia kifua shauri hili ili liwe funzo kwa wengine, kwani watanzania sasa hivi tumechoshwa na idara ya polisi kuzidi kuhalalisha unyanyasaji, uuaji na kukandamizaji wa sheria kwa visingizio visivyo na hoja za msingi kwa malengo ya kulinda nafasi zao, CCM na viongozi wa serikali. Mahakama ndio chombo pekee chenye kuwashikisha adabu hawa na kulinda haki za wananchi.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka watu wa Sodom na Gomora walipozidi kutenda dhambi MUNGU alisema; Kamwe sitashindana na mwanadamu, nitashuka nikauone uovu wao!!!
   
 9. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  huyu kamanda mbona ameghafilika kama nyoka vile?
   
 10. m

  majebere JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Lissu anatafuta sifa tu,hawa wanafurahia raia akiuawa ndio wanapo patia nafasi ya kujijenga kisiasa. Alikua wapi wakati yule kijana wa CCM alieuawa singida kwenye mkutano wa CDM
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Pamoja na vitisho vyote hivyo na mauaji ya polisi lakini bado mkutano ulifana na kujaza watu nyomi dalili ya njaa ya uongozi bora waliyo nayo wananchi wa Tanzania.
   
 12. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mtajuzwa tuje tuage pamoja
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni jana Mkuu,nakumbuka iliwapa watu simanzi kubwa pale kiwanjani wakati Lissu anatoa kauli hii,wengi walio na machozi ya karibu walishndwa kuzuia hisia zao!too sad kwa watawala walipofikia,yote kwa yote wameshndwa kujifunza kwa watawala na wakuu wa polisi wengine duniani kwa kujijaza u.j.i.n.g.a kua magamba watatawala milele,muda wao unahesabika,tena umebaki mchache sana!
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jaribu kutofautisha matukio, kwani mimi binafsi nahuzunishwa na kila damu inayopotea. Yaliyotokea Singida yalichukuliwa hatua mara moja na viongozi wa Chadema ambao hata hawakujua nini kimetokea waliitwa na vyombo vya dola, lakini hili la Morogoro hakuna hata hatua zo zote zinazochukuliwa, we unaona tofauti hiyo kama una uchungu wa kweli na kupima haki sawa kwa wote?
   
 15. m

  majebere JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Hii ndio single mpya ya CDM.
   
 16. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya niko safarina na natumia cellphone mkuu,ila naigongea like
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama malalamiko hayasaidii na wala kusikilizwa, kwa vile wanasheria mashuhuri wako, bora hatua hii ya kufikisha wahusika mahakamani, kwani mahakama ni mhimuli huru ambao hauangalii nafasi au sura ya mtu bali sheria.
   
 18. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Dah .... morogoro imekuwa shujaa wakubwa sana .... sijui ccm imebakia eneo gani?
   
 19. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii nayo ni hoja au viroja?
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Too sad, Waziri na serikali imekaa kimya kana kwamba hakukutokea kitu, ni aibu ilioje jamani nchi hii?
   
Loading...