Lissu wako wapi wale watu uliosema utawaingiza barabarani?

Habari wanajf, poleni na pilikapilika za sikukuu hizi za mwisho wa mwaka.

Moja kwa moja niende kwenye jambo ambalo limenisukuma nije kuandika uzi humu.

Wote tunakumbuka kipindi cha kampeni mwaka huu kilivyopamba moto.

Kulikua na kila aina ya ngebe na majigambo kwa kila upande unaoshiriki kwenye uchaguzi.
JF kama ilivyo kawaida zikaibuka id's nyingi sana mpya.

Kubwa ni lile la Lissu kusema atawaingiza barabarani watu. Moja kwa moja wenye akili ndani ya chadema walisubiri huo muda ufike ili tuone kama ataweza.

Lissu kwa jeuri na mihemko ya hali ya juu alisema atawaingiza watu barabarani, na hili amekuwa akilisema mara kwa mara kwenye mikutano yake.

Wenye akili tulikuwa tunaendela kujiuliza pengine Lissu kuna watu anawafuga kama mifugo, hivyo akikohoa tu nao wanafata.

Siku ikafika, akaamuru watu waingie barabarani, ila bahati nzuri wabongo huwa ni wanafki(na mimi nikiwemo), huwa tunakusupport kwa kila aina ya maneno, linapokuja suala la vitendo huwa tunaanza kukusengenya.

Humu JF kabla ya kutangazwa watu kuingia barabarani, watu wengi walionekana kuhamasika na kupost kila aina ya ngebe wanazozijua, ila ilipofika siku ya tukio, wote waligeuka na kuanza kusema polisi wametumia nguvu sana ndio maana hatujatokea.

Unafki unakupa pale ambapo haohao wanaosema hawajaandamana sababu ya polisi ndio haohao waliosema polisi hawataweza kuzuia nguvu ya umma.

Na ni hawahawa waliosema Lowassa ana busara kwa kutotoa amri ya watu kuandamana kwa kuwa ingeleta maafa, na wakaenda mbali zaidi na kusema walikuwa wanasubiri Lowassa atoe tu tamko waingie barabarani.

Mungu si athumani, mwaka huu Lissu akatoa tamko, wote tunajua kilichotokea. Hawa ndio Wabongo.

Ni kweli, polisi wala jeshi hawawezi kuzuia nguvu ya umma, mifano ipo mingi sana. Hivyo ni dhahiri wale watu aliosema lissu kuwa atawaingiza barabarani HAWAPO.

Lissu ulishindwa vipi kujua kuwa huna nguvu ya kuamrisha watu kuingia barabarani?

Pole Lissu, umejifunza jambo. Ila kama bado hujajifunza ningependa kujua wale watu uliokuwa unaringia kuwaingiza barabarani WAPO WAPI??
Hivyo vilikuwa vituko vya Lodi Lofa
 
Binafsi kuhusu Lisu hakuna kitakachonitenganisha naye zaidi ya kifo. Atabaki kuwa Lissu tu. Juzi nimesimamia Mtoto anabatizwa Antipas kwa heshima yake. Heri kwake.
Huyo jamaa anaitwa Tundu. Hilo Antipas ni baba Yake. Huyo mtoto aitwe Tundu.
 
Hapana, mimi ni mmoja wa watu ambao tunahoji walipo watu ambao lissu alisema na kuturingishia kuwa atawaingiza barabarani
Kwa hiyo ahadi za jamaa yenu za mamilioni na laptop unazikana/hazikuhusu? Au wewe si mtanzania????
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom