Lissu Vs Zitto: Nani mkali wa kujenga hoja za kisiasa?

Cumudia

Senior Member
Sep 21, 2018
193
250
Chama kikishashinda uchaguzi, basi wengine wote mnatakiwa kuungana kutekeleza ilani ya chama hicho. Hii ni kwasababu ilani inatekelezwa kwa watanzania wote bila kujali chama, dini au kabila.

Kuzuia au kutokutoa ushirikiano katika utekelezaji wa chama tawala ni kuihujumu nchi. Vyama vya upinzani vinatakiwa kuzunguka mikoani kipindi cha kampeni kunadi sera zake mbadala ili wachaguliwe
Hayo ni ya kwako kimaoni! ,lakini pia maoni hayo yamejaa uoga wa ushindani wa kisiasa,uoga wa mabadiliko,uoga wa kuona fulani hana haki tena as long as huyu kashinda, that's shame mkuu.
1. nini maana ya demokrasia ya vyama vingi pia pana haja gani kukubali demokrasia ya vyama vingi ikiwa unabinya wengine kwa kutumia taasisi zilizochini yako?
2. Je utawala wa nchi unaruhusu hiyo demokrasia?
Kuhusu chama kushinda uchaguzi sio tatizo, waunge mkono kwani katiba zao zinafanana?
Vipi kuhusu ilani zao?

Mwisho:
What if aliyeshinda akabinya Uhuru wa wengine kuwakomoa katika tasnia ya uhuru na haki ili yeye aogopeke mawazo yako ni rahisi mno kuunga mkono utawala wa mkono wa chuma naamini,Uhuru wa kupata habari, Uhuru wa kuhoji nk.
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Wote ni wakali na wote wanajenga hoja zao kwa kuegemea uweledi wa taaluma zao.Ila kwenye uwadilishaji wa hoja jukwaani ZZK Yuko njema zaidi but kwenye kujuamini,msimamo usioyumba na kuaminika TL ni Bora kuliko ZZK maana Zito hakawii kuwauza .ZZK angekuwa Chadema ingekuwa combination nzuri Sana na TL lakini huko alikoenda atapotea Kama alikuwa na malengo ya kuja kuingia ikulu,nafasi iko kwa Chadema zaidi
Unfortunately kwa mgombea wa chama Cha mbogamboga yaani kwenye kujenga na kutetea hoja ni hamna kitu pale
 

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
4,389
2,000
Waungwana hebu tuwe tu wakweli bila jazba wala chuki, Kati ya viongozi wa upinzani hawa wawili, Lissu na Zitto namuona Zitto kuwa yuko vizuri sana kwenye kujenga hoja za Kisiasa.

Lissu ni mzuri sana kwenye field yake ya sheria ila kiukweli nadhani hata CHADEMA wenyewe sasa hivi watakuwa wameona, Lissu sio mjengaji mzuri wa hoja za Kisiasa. Anapitwa kwa mbali mno na Zitto.

Lissu shida yake kubwa ni ile hali ya kutokuweza kuzuia hisia zake. Anaongea kwa ukali, jazba na hasira. Hii inamkosesha ule mvuto wa kisiasa.

Nashauri timu yake ya Kampeni imsaidie ili wananchi tuweze kumfuatilia vizuri na kufanya maamuzi sahihi.

Siasa sio mabishano ya kimahakama. Hapa tunataka hoja za msingi zinazowasilishwa kwa ufundi. Namna gani pale TAL?

Amani Msumari

Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)
naona mmetumwa kuja kumfundisha lissu cha kuongea kisa kawashika pabaya. MATAGA bana...na bado hadi mtokwe na damu. utamu wa lissu kwenye ujengaji wa hoja ni kama unaangalia prison break vile au money heist! hachoshi.

lile lingine kule limedanganya kuwa kwa kukataa kupiga lockdown wakati wa corona ndio kete ya kisiasa kumbe ni upuuzi mtupu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom