Lissu Vs Zitto: Nani mkali wa kujenga hoja za kisiasa?

Cumudia

Senior Member
Sep 21, 2018
193
250
Hakuna mtu ananunuliwa. Sina shaka na uwezo wao Kama viongozi ila bado wanahitaji kutumia uwezo huo kuisaidia nchi badala ya kuiangamiza. Wanahitaji kuwa wazalendo zaidi
Wanaweza isaidiaje nchi kwa mfumo huu wa nchi hii pia wanaiangamizaje ebu nitoe gizani?
Istoshe wote ni wazalendo hakuna asiye mzalendo kati yao
 
JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
628
500
Waungwana hebu tuwe tu wakweli bila jazba wala chuki, Kati ya viongozi wa upinzani hawa wawili, Lissu na Zitto namuona Zitto kuwa yuko vizuri sana kwenye kujenga hoja za Kisiasa.

Lissu ni mzuri sana kwenye field yake ya sheria ila kiukweli nadhani hata CHADEMA wenyewe sasa hivi watakuwa wameona, Lissu sio mjengaji mzuri wa hoja za Kisiasa. Anapitwa kwa mbali mno na Zitto.

Lissu shida yake kubwa ni ile hali ya kutokuweza kuzuia hisia zake. Anaongea kwa ukali, jazba na hasira. Hii inamkosesha ule mvuto wa kisiasa.

Nashauri timu yake ya Kampeni imsaidie ili wananchi tuweze kumfuatilia vizuri na kufanya maamuzi sahihi.

Siasa sio mabishano ya kimahakama. Hapa tunataka hoja za msingi zinazowasilishwa kwa ufundi. Namna gani pale TAL?

Amani Msumari

Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)
Zitto mzuri lakini TL mzuri zaidi
 
dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,390
2,000
Zitto anauwezo mkubwa wakujenga hoja na watu wakamuelewa kwa urahisi Sana.
Nikimuangalia bungeni Zitto alikua na uwezo wa kujenga hoja akiwa na vielelezo ishu Kama Za Buzwagi n.k zililichachafya Sana bunge.
Hivyo Zito namuona ni mjengaji hoja Mzuri sana na anajenga hoja bila matusi wala jazba kiasi kwamba kila mtu anaona hoja yake bila kujali itikadi yake.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
shabiki

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
866
1,000
Waungwana hebu tuwe tu wakweli bila jazba wala chuki, Kati ya viongozi wa upinzani hawa wawili, Lissu na Zitto namuona Zitto kuwa yuko vizuri sana kwenye kujenga hoja za Kisiasa.

Lissu ni mzuri sana kwenye field yake ya sheria ila kiukweli nadhani hata CHADEMA wenyewe sasa hivi watakuwa wameona, Lissu sio mjengaji mzuri wa hoja za Kisiasa. Anapitwa kwa mbali mno na Zitto.

Lissu shida yake kubwa ni ile hali ya kutokuweza kuzuia hisia zake. Anaongea kwa ukali, jazba na hasira. Hii inamkosesha ule mvuto wa kisiasa.

Nashauri timu yake ya Kampeni imsaidie ili wananchi tuweze kumfuatilia vizuri na kufanya maamuzi sahihi.

Siasa sio mabishano ya kimahakama. Hapa tunataka hoja za msingi zinazowasilishwa kwa ufundi. Namna gani pale TAL?

Amani Msumari

Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)
Msukuma!
 
Larson

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
257
250
Shida yake tu ni ule "undumilakuwili"
Nani kwenye ile saccos yenu sio ndumilakuwili?. Huyo Zitto alikuwa mwana saccos mzuri tu, mkamtimua alipoanza kugusa maslahi yenu. Huko kwenye chama tu mnatusuana, ndio mnataka watanzania wawape nchi thubutu. Huyo Lissu mwenyewe hawezi kuwa mwenyekiti hapo saccos, je ataweza tanzania kweli?.
 
Larson

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
257
250
zito mwana aminifu wa ccm na msaliti wa harakati za cdm anawezaje kulinganishwa na lisu? ni dhambi kubwa nani asiyejua alivyolipwa na ccm kuiangusha akashindwa akaishia kuanzisha chama chake ?
Huijui saccos wewe. Kilichomtoa Zitto hapo, ni uenyekiti. Hiyo nafasi hata Lissu akiikodolea macho, anaondoka mchana kweupe.Zitto yuko smart kuliko Lissu, hoja zake hazina matusi wala jazba. Ni aina ya viongozi kama kina Dr. Slaa na Eng Mbatia.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,723
2,000
..Zitto ni mjenga hoja mzuri, lakini wakati mwingine anachosha kumsikiliza. He is kind of robotic.

..Tundu Lissu akianza kuzungumza huwezi kuchoka kumsikiliza, hatabiriki ktk uzungumzaji wake.

..Lissu anaweza kuzungumza mambo serious jukwaani, lakini pia anaweza kuzungumza vichekesho vya kuwavunja mbavu wasikilizaji wake.

..Zitto ni mzuri zaidi ktk masuala ya uchumi na fedha. Tundu Lissu ni mzuri ktk masuala ya sheria, katiba,haki za binadamu, na utawala bora.
 
Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,832
2,000
Binafsi zito kabwe naona kuwa ni mzuri zaidi wa hoja.anauwezo wa kutoa hoja na kujenga hoja katika kila idara ama sehemu na ikawa nzito kweli.

Yaani anafiti kotekote.

Na lissu nae naona yuko vizuri hasa kwenye mambo ya sheria,mbali na sheria naona kama kwenye mambo mengine hafiti kiivyo
Huo ndio ukweli ndugu Safuher. Tatizo was hawako "objective" mahaba yamewazidi.

Mfano huu ni mdogo sana lakini wenye maana kubwa sana. Mada hii nimeileta kwa makusudi kabisa kutaka kuwafundisha ndugu zangu kuangalia ukweli with objective lens. Hii inawasaidia sana kufanya maamuzi sahihi.

Ni wachache watasema Zitto ni mzuri wa hoja za Kisiasa lakini mimi nitamchagua Lissu kwasababu hizi na hizi .........
 
Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,832
2,000
Wote wawili ni matapeli wa kisiasa tu hawana hoja hata.
Ila sifa ya utapeli hauwaondolei uwezo wa kuweza kujenga hoja. "Matapeli wazuri pia ni wajengaji hoja wazuri ili waweze kukutapeli vizuri". So, hebu tuwapime hawa kwenye ulingo wa kisiasa
 
Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,832
2,000
Wanaweza isaidiaje nchi kwa mfumo huu wa nchi hii pia wanaiangamizaje ebu nitoe gizani?
Istoshe wote ni wazalendo hakuna asiye mzalendo kati yao
Chama kikishashinda uchaguzi, basi wengine wote mnatakiwa kuungana kutekeleza ilani ya chama hicho. Hii ni kwasababu ilani inatekelezwa kwa watanzania wote bila kujali chama, dini au kabila.

Kuzuia au kutokutoa ushirikiano katika utekelezaji wa chama tawala ni kuihujumu nchi. Vyama vya upinzani vinatakiwa kuzunguka mikoani kipindi cha kampeni kunadi sera zake mbadala ili wachaguliwe
 
Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,832
2,000
kwhiyo tukika ndani tunaweza kurekebisha tume ya uchaguzi? just be honest
Kwani wakati Rais Kikwete anakaribia kuondoka alilazimishwa na nani kuunda ile time ya Mzee Warioba?

Tujenge ushawishi wa ndani kwa njia stahiki, "everything in due time"
 
Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,832
2,000
Nani kwenye ile saccos yenu sio ndumilakuwili?. Huyo Zitto alikuwa mwana saccos mzuri tu, mkamtimua alipoanza kugusa maslahi yenu. Huko kwenye chama tu mnatusuana, ndio mnataka watanzania wawape nchi thubutu. Huyo Lissu mwenyewe hawezi kuwa mwenyekiti hapo saccos, je ataweza tanzania kweli?.
Nimekusoma ndugu Larson kuwa bwana Lissu kwa nafasi ya urais wa Tanzania bado hafiti. Kazi kwa mashabiki wake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom