Lissu Vs Zitto: Nani mkali wa kujenga hoja za kisiasa?

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Waungwana hebu tuwe tu wakweli bila jazba wala chuki, Kati ya viongozi wa upinzani hawa wawili, Lissu na Zitto namuona Zitto kuwa yuko vizuri sana kwenye kujenga hoja za Kisiasa.

Lissu ni mzuri sana kwenye field yake ya sheria ila kiukweli nadhani hata CHADEMA wenyewe sasa hivi watakuwa wameona, Lissu sio mjengaji mzuri wa hoja za Kisiasa. Anapitwa kwa mbali mno na Zitto.

Lissu shida yake kubwa ni ile hali ya kutokuweza kuzuia hisia zake. Anaongea kwa ukali, jazba na hasira. Hii inamkosesha ule mvuto wa kisiasa.

Nashauri timu yake ya Kampeni imsaidie ili wananchi tuweze kumfuatilia vizuri na kufanya maamuzi sahihi.

Siasa sio mabishano ya kimahakama. Hapa tunataka hoja za msingi zinazowasilishwa kwa ufundi. Namna gani pale TAL?

Amani Msumari

Tanga (kwasasa Arusha kwa kazi maalumu)
 
Hao wote ni vichwa ndio maana nyinyi maccm mmeshindwa kuwanunua.
Hakuna mtu ananunuliwa. Sina shaka na uwezo wao Kama viongozi ila bado wanahitaji kutumia uwezo huo kuisaidia nchi badala ya kuiangamiza. Wanahitaji kuwa wazalendo zaidi
 
Hakuna chochote kikamilifu ila tunakikamilisha kwa kuwa kinakuwa kimechukua sifa za ukamilifu kamili
 
Hakuna chochote kikamilifu ila tunakikamilisha kwa kuwa kinakuwa kimechukua sifa za ukamilifu kamili
Kumbe umeona eeeh. Ndio maana nashauri asaidiwe labda 2025 anaweza kuongea vizuri zaidi hapo Watanzania watampima vizuri. Kwa mwendo huu ataigharimu CHADEMA, yaani 25% ya kura haipo
 
We tulia...tunataka mdahalo na mgombea wa CCM...asijaribu kutoka nduki aje ili watanzania wajionee wenyewe kwa macho na maskio yao kwamba zipi ni mbivu na zipi ni mbichi.
 
Ukiacha makandokando mengine, Zitto kwenye hoja ni heavy weight! Anavutia, anajua kuchambua complex issues hasa za kiuchumi!

Lissu ni wakili mzuri Sana na he can make the best mwanasheria wa serikali!

Ukiwaweka jukwaa la siasa, Zitto is far better than Tundu!
 
We tulia...tunataka mdahalo na mgombea wa CCM...asijaribu kutoka nduki aje ili watanzania wajionee wenyewe kwa macho na maskio yao kwamba zipi ni mbivu na zipi ni mbichi.
Mgombea wetu kazi zake zinamuuza
 
zito mwana aminifu wa ccm na msaliti wa harakati za cdm anawezaje kulinganishwa na lisu? ni dhambi kubwa nani asiyejua alivyolipwa na ccm kuiangusha akashindwa akaishia kuanzisha chama chake ?
 
Back
Top Bottom