Lissu usimjibu Albert Msando, mimi Namjibu

Kwa mabli nakubaliana na wewe mkuu maana choko choko hazitaisha iwapo atabaki chadema... kila siku atataka awe kwenye headlines za magazeti ... kama noma na iwe noma ... afukuzwe moja kwa moja na hao wafuasi wake wote ... mimi naamin approach waliyotumia akina mkumbo ya kuandaa waraka ule bado ni ya kisaliti na ki uwoga ... kama kweli wana hoja wameshindwa nini kuwasilisha chamani? hata kama wana hoja lakini wameonesha udhaifu wa hali ya juu wa kutofuata taratibu rasmi za chama ... i am utterly disappointed by them ... sharti la kusamehewa ni waombe msamaha hadharani kwa viongozi na wana chadema wote waliodhurika na kashi kashi hizi


Mkuu kwa heshima, uhai na uthabiti wa chadema, njia ni moja tu kufukuza hawa jamaa, kinyume na hapo chadema lazima

ife, narudia bila kuwafukuza hao jamaa ni suala la muda tu na chama kitasambaratika kama NCCR ya akina Mrema.
 
Ndugu,

Ameweka kifungu cha 'KAZI' za Kamati Kuu. Hajasema ni wapi nimesema Kamati Kuu haina mamlaka.

Swali langu ni rahisi sana, JE UTARATIBU wa kumvua mtu nafasi za uongozi unasemaje? Katiba ya Chama ina vipengele vinavyotoa utaratibu gani ufuatwe pale Kamati Kuu inapotekeleza wajibu wake.

Hayo mengine ya ujanja, sifa, utoto nk sio yangu kujibu. Sitajishughulisha nayo.

Albert.
 
Yassin, umenishangaza sana. Ila kipimo cha urafiki wa kweli unakijua. Au labda umeamua kujisahaulisha.

Moja ya kauli zako....

Kama ulivyoona hapo juu alitajwa ndugu yetu Albert Msando, sasa leo kamanda Albert Msando amevunja ukimya na kuweka haya kwenywe wall yake ya FB kama Salamu kwa Godbless J Lema na Zitto.

Ndugu yenu! Kamanda! Leo amegeuka mtu mjanja mjanja anaependa sifa!! Kisa kuhoji utaratibu na kusema ukweli?

Nitasimama hapo hapo mpaka pale utakapoweza kuleta hoja kwamba utaratibu uliotumika ni sahihi.
 
If you can't beat them join them!! - Albert, Boss wako alitakiwa alijue hili mapema, sasa haya ya vipengele yatafuata wakati boss wako hupo uraiani.
 
Ndugu,

Ameweka kifungu cha 'KAZI' za Kamati Kuu. Hajasema ni wapi nimesema Kamati Kuu haina mamlaka.

Swali langu ni rahisi sana, JE UTARATIBU wa kumvua mtu nafasi za uongozi unasemaje? Katiba ya Chama ina vipengele vinavyotoa utaratibu gani ufuatwe pale Kamati Kuu inapotekeleza wajibu wake.

Hayo mengine ya ujanja, sifa, utoto nk sio yangu kujibu. Sitajishughulisha nayo.

Albert.

Ndugu Albert,
Wewe kama mwanachama na kiongozi tena mwenye elimu na uelewa ni kwanini shortcomings kama hizi hamzileti au kuomba vikao ili viwe revised au introduced ili chama kiendelee kuimarika? Pia kama huna uwezo wa kuomba kikao hilo nalo linatakiwa liwe discussed ili mwanachama awe ana uwezo wa kuomba kikao. Hiyo ndio namna pekee ya kujenga chama. Huwezi kujenga chama mitandaoni.

Sijawahi kusikia software engineer wa Microsoft au Apple anaenda online kusaga product ya kampuni yake. Atakachofanya nikuwaeleza wakuu wake tatizo liko wapi na nini ufumbuzi wake.
 
Ndugu,

Ameweka kifungu cha 'KAZI' za Kamati Kuu. Hajasema ni wapi nimesema Kamati Kuu haina mamlaka.

Swali langu ni rahisi sana, JE UTARATIBU wa kumvua mtu nafasi za uongozi unasemaje? Katiba ya Chama ina vipengele vinavyotoa utaratibu gani ufuatwe pale Kamati Kuu inapotekeleza wajibu wake.

Hayo mengine ya ujanja, sifa, utoto nk sio yangu kujibu. Sitajishughulisha nayo.

Albert.

kamanda , KWENYE KATIBA YA CHADEMA HAKUNA KIFUNGU KINACHORUHUSU KUKATA RUFAA ? NA JE KAMA WAHUSIKA WALIKUWA VIONGOZI WA JUU, TENA WASOMI ( BILA SHAKA WANAIJUA KATIBA ) NA WAMERIDHIKA NA MAAMUZI YALIYOTOLEWA , JE KUNA HAJA YA WATU WENGINE KUPIGA KELELE ?
 
Tatu,

Unayosema ni kweli. Katika hali ya kawaida hayo yangejadiliwa kwenye vikao na kurekebishwa. Tatizo limeshajitokeza na lazima tukubali kwanza halafu tutatue.

Sioni kwa nini tuogope kukiri tatizo na kulitatua. Katika hili tumekosea. Na ni jambo la kawaida kabisa kukosea. Utaratibu haujafuatwa. Kama ukifuatwa wahusika watahukumiwa na kuadhibiwa kwa haki.

Ni matumaini yangu busara itatamalaki na wote tutajifunza.
 
Albert Msando hana waledi wa kusimama kama wakili wa Zitto na Dr. Kitilla mkumbo (japo wanamakosa). Huyu ni mtu anayefanya mambo kiujanja ujanja siku zote. Kama uliangalia ile Press ni kwamba Albert alienda kukaa pale kujitafutia umaarufu kwa kuvaa viatu visivyo mtosha.

Kuna mahala alijichanganya akasema kwa mihemko ya hali ya juu, nanukuu ''Zitto na Dr. Kitila hawajapokea barua rasmi ya kusimamishwa nyazifa zao'' mwisho wa kunukuu. Kabala hajaendelea Zitto na Kitila wakasawazisha fasta ,wakasema japo hawajapata barua ila wanayatambua na kuyaheshimu maamuzi ya Kamati kuu. Albert hawezi kushindana na Tindu Lissu hata siku moja ni mpenda sifa zisizo na tija.
Kumpatia Tundu Lissu ashindane na Albert ni kumkweza huyu kijana mjanjamnjanja. Na ndicho kitu anachokitaka.

Huyu Kibatala au Mbogoro, mmojawapo anamtosha.
 
Hawa maCDM hata jina la diwani wake halijuwi anakurupuka na kujibu hoja ati Albert Kisando? Huyu ni Msando ex speaker pale UDSM!

Nyie vijana wa CDM mbona mbembwe nyingi sana lakini umakini mnakosa? Kukosea jina la mtu ni mbaya sana kisheria! We umesoma wapi? Kile chuo cha mapadri cha mwanza? Maana nao wanafunzi wao wanatupa shida sana hapa maofisini!

Next time proof read kazi yako before you post ndio uungwana! No hurry in academia!

fungueni chenu cha masheikh we mbulula halafu ujue ni cha mapadri ila wanasoma watanzania wakiwemo waislamu acha dharau wewe mrembo habariyamujini.
 
Last edited by a moderator:
Utaratibu wa kukata Rufaa upo na ndio sababu jana tumeeleza kwamba taratibu zote zitafuatwa kwa mujibu wa Katiba na kanuni. Ni watu wachache wanataka jambo hili likuzwe na kuonekana ni mpasuko.
 
Kumbe hata wewe huijui Chadema kabisa.nani kakwambia Kitila alikuwa mjumbe wa kuteuliwa?Kitila alikuwa mjumbe wa kuchaguliwa kwa kura yeye pamoja na Pro Baregu na walishinda kwa kura nyingi akiongoza Baregu.Kina Mbowe na Katibu ndio wanaingia kwa nafassi za vyeo vyao then kuna zuile nafasi 5 za wabunge ambazo ndio za kuteuliwa kama Mbatia,humo unamkuta Lema na wenzake.
Acha kuropoka jkama hujui ukweli na hukuwemo kwenye uchaguzi.

leo katika vyombo vya habari, wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini (cdm) ametoa kasoro za kisheria kwa Mwanasheria Mkuu wa cdm juu ya hukumu ya kitila mkumbo na zitto kabwe. Msando alisema katiba ya cdm inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewanafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi, mwisho wa kunukuu.

napenda kumwambia Msando akasome katiba ya cdm vizuri hicho kifungu anachosema ni kwa viongozi yeyote wale wa kuchaguliwa, wa mabaraza, wenyeviti wastaafu, wawakilishi wa madiwani na wabunge ndio inawapaswa kufanya ivyo na sio wajumbe wa kuteuliwa kama wakina Kitila MKUMBO. kifungu ambacho kinawapa mamlaka ya kuwavua nyazifa ni hiki hapa.


7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisharipoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

(b) Kuteua Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu

(c) Kuteua Makatibu wa Wilaya na Mikoa

(d) Kuthibitisha uteuzi wa Sekretarieti za Wilaya.

(e) Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu.

(f) Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuliza Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano.

(g) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa baraza Kuu , Mikakati ya kupata mahitaji yaraslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali.

(h) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza kuu ratiba na maelekezo ya uchaguzi wakichama.

(i) Kupitia na kutoa kwa Baraza Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebishoau maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama.

(j) Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwautekelezaji.

(k) Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu

(l) Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu kwakuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu.

(m) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza Kuu na MkutanoMkuu.

(n) Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vyasiasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.

(o) Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.

(p) Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa mudamaalumu.

(q) Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka

(r) Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la wawakilishi
Zanzibar

(s) Kuandaa agenda za Baraza Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu.

(t) Kufanya uamuzi juu ya mpendekezo ya kufukuza Mwanachama.

(u) Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama

(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume nakatiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

(w) Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.

(x) Kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.

(y) Kuteua wajumbe maalum wawili kuingia Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya.


kwa kuwa mkumbo ni mjumbe wa kuteuliwa anaangukia kwy kifungu hicho hapo juu (v).





nawasilisha:


 
Back
Top Bottom