LISSU ushauri wako naukataa kabisaa!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwanini tusikubali kua CCM wametushinda? Haya mambo ya kufarijiana mimi binafsi siyaafiki kabisa! Au nawe unacheza na hawa jamaa? Tumeshindwa, tumeshindwa bhaasi! na hili ndilo jibu tusing'ate midomo.

Inamaana tuendelee kuchekelea kwakua Lowassa hakupoteza kitu 2015 kwa vile urais ulikua CCM? Au kuze Zanzibar CUF nao waendelee kufurahia kwa vile hawakupoteza kitu kwa vile Urais tangu zamani alikua nao Dr Shein?LISSU my brother try to think big on this.I do respect you very much!

Kwa kawaida kazi ya mpinzani ni kumtoa madarakani aliyekalia kati au anayetetea nafasi yake, yaani inatakiwa kua na mawazo mbada ili kuwashawishi wananchi wamkatae na sio kusema tufurahi kwa sababu hatujapoteza kitu! Hatujapoteza kitu? Rasirimali pesa na muda hatukupoteza wakati wa kampeni? Tusifarijiane kwenye mambo ya msingi ni lazima tuwe wawazi ile tujipange vyema zaidi.

Kazi kubwa ya mpinzani ni kumyang'anya mtawala kiti chake ili wewe ukalie, ukishindwa kumnyanganya inamaana bado anakuzidi mbinu. Hatutakiwi kuchekelea kabisa juu ya hili. Kama tumeshindwa kumnyang'anya hasimu wetu kiti chake basi tusubiri arudi aje atunyanganye sisi.

Kama hatuna time huru ya Uchaguzi,basi hayo ndiyo majibu sahihi na siso kujifariji eti hatukupoteza kitu ilihali tumepoteza rasirimali muda na pesa.

Tutoke tuidai tume huru ya uchaguzi, wakurugenzi makada wa CCM wabaki kuendelea na shughuli zao na sio kuvishwa kofisa za usimamizi wa uchaguzi.Tume ya taifa ni taasisi kubwa iwezeshwe ipeleke wawakilishi kila jimbo.Hatutaki mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ateuliwe na Rais, tubadili katiba kabla ya 2020 hatuna namna.
 
Ni shida mkuu. Pamoja na kusema mkubwa wetu hakubaliki....matokeo yake ndio haya. Nafasi haitumiki vema inapopatikana. 2020 itakuwa majonzi zaidi.
 
Mimi binafsi Lissu nimemwelewa

Mara ya mwisho Ccm kushinda nikakubali na nchi ikawa na furaha ilikuwa mwaka 2005 toka hapo Ccm hawajawai kushinda ........
 
Wapinzani watumie muda wao kuwapa presha ccm ili wafanye mambo ya msingi lakini kwenye suala la kuingia ikulu sio leo wala kesho labda waungane na ccm.
Kabisa mkuu! Haya mambo ya kushukuru kwakua CCM wameshinda kutetea nafasi zao mimi inanitia shaka sana.
 
Wapinzani watumie muda wao kuwapa presha ccm ili wafanye mambo ya msingi lakini kwenye suala la kuingia ikulu sio leo wala kesho labda waungane na ccm.
Mkuu ni ngumu wapinzani kupasua kwa mazingira yasio rafiki.Tatizo kubwa ni kutegemea miujiza.Na Kaisari haamini katika miujiza.
 
Maendeleo mnayoyaona sasa yalipaswa kuwepo tangu miaka ya 1990 huko lakini nchi ilikosa viongozi wenye utu.
 
tume huru ndo suluhisho lkn ukawa hawana mpango nayo utaona 2020 wanaingiza kichwa afu kinaliwa tu na ccm toka 1995 mpk leo wameridhika na ruzuku tuu
 
Kukiwa na upinzani makini hata Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi awe mke wa rais au rais mwenyewe ushindi uko pale pale tu.

Angalia Ghana upinzani umeshinda ilhali Mwenyekiti na Deputies wake wawili pamoja na wajumbe wengine wanne wa tume ya uchaguzi ni wateule WA rais japokuwa anatakiwa kushauriana na coucil of state kwenye hizo teuzi lakini council nayo imejaa makada.

Nigeria nayo iko hivyo Chairman ni mteule wa rais anayethibitishwa na senate lakini upinzani umepenya.

Siasa ni watu(uungwaji mkono) kama upinzani una ushawishi,tume haiwezi kuzuia kitu.

Jammeh alikuwa na kila kitu lakini mbona kashindwa uchaguzi?
 
kwa tume hii wapinzani wakiendelea kushiriki uchaguzi mwaka 2020 watapigwa zaidi....wakurugenzi wote kwa sasa ni wale makada walioshindwa kwenye kura za maoni.
 
Mkuu ni ngumu wapinzani kupasua kwa mazingira yasio rafiki.Tatizo kubwa ni kutegemea miujiza.Na Kaisari haamini katika miujiza.
Ni ujinga kuingia ulingoni ukapoteza muda na rasilimali halafu unaleta hoja ni vigumu kutusua. Kama unajua hivyo kwa nini uingie ulingoni. Acheni hoja zisizo na mashiko Mheshimiwa kakosea eti Hanna tulichopoteza. Kwanza rasilimali fedha imepotea na muda pia. Hata hivyo psychological mood inawafanya watu wawe na imani na chama tawala. Msijidanganye eti hamna tulichopoteza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom