Uchaguzi 2020 Lissu umati usikudanganye, wengi hawajajiandikisha

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,066
2,214
Wafuasi wa CHADEMA na Lissu wamekuwa wakipagawa na kuota kwamba, uchaguzi wa October utawapatia ushindi na kwa mara ya kwanza toka tujipatie Uhuru nchi itaongozwa na upinzani.

Hii ni kutokana na Umati ambao umekuwa ukijitokeza kwenye kampeni za ugombea urais kwa mheshimiwa Tundu Lissu. Niwaambie wafuasi wa CHADEMA endeleeni kufurahia ngojera za mgombea wenu ila Urais mtaendelea kuusikia hadi 2925.

Sababu ya kwanza ni kwamba, watanzania wengi mnaowaona kwenye mikutano, hawajajiandikisha na hata hao waliojiandikisha, kwenye uchaguzi wa mwaka huu hawataamka kwenda kupiga hiyo kura kwa vile inajulikana wazi Mjomba Magu anarudi pale Chamwino na Magogoni.

Pili, vyama vya upinzani vyote vimeshapoteza mvuto kwa wananchi na kuikubali CCM na mgombea wake, kwa yale Serikali ya CCM iliyoyafanya na yanaonekana kwa macho na hata kuyagusa kwa mkono.

Tatu, Viongozi wa vyama vya upinzani wameshapoteza imani kwa wananchi na hasa Wasomi na waelewa wa mambo,ambao miaka michache iliyopita ndiyo tulikuwa tukiunga mkono mageuzi, kwa kuona CCM ni ya watu wasiojielewa. Kupotea kwa imani hii kumetokana na viongozi wenyewe wa vyama vya upinzani kufanya kama taasisi zao, na si za wananchi. Tazama Mbowe na Chadema, Zitto na ACT, hawana tofauti na Mzee Mrema wa TLP, au NCCR ya Mbatia.Ndiyo maana Dr Slaa aliyaona haya mapema akaamua kukaa pembeni.Chadema na wafuasi wenu msijidanganye.
 
Naona Misukule ya Lumumba mnaanza kuelewa na kukubali hatua kwa hatua!!

Juzi juzi tu hapa Jiwe na Misukule yake ilikuwa inadanganya umma kwamba CHADEMA ina-post picha fake kwenye social media na kwamba zingine ni zile za 2015!

Leo hii unakiri kwamba "Umati ambao umekuwa ukijitokeza"!!

Well done, inafahamika wanadamu wametofautiana kasi ya kuelewa jambo fulani!!

Wakati wengine ubongo wao unawafanya waelewe kwa haraka sana, wengine ubongo wao unawafanya waelewe pole pole na wengine kutoelewa kabisa!

Kwa mara nyingine, kwa roho nyeupe kabisa ningependa kukupongeza kwa kutokuwa na ubongo lala usiolewa kabisa!!
Kitendo cha magu kusema zile ni picha za 2015. Nilijiuliza tuna kiongozi wa aina gari? Mkapa ulale unapostahili
 
bro hao wasio jiandikisha ni watu hatari sana!

Umati anaopata Tundu ni kipimo chao cha ushindi!

Ndio sababu sasa Navunja goti Uchaguzi huu Uwe wa Haqi! na ningekuwa nina mamlaka ungekuwa uchaguzi wa wazi; mtu afoleni nyuma ya mgombea anae mpenda, kisha mshindi apatikane na kutangazwa!

Tuendelee na mishe mishe!
 
Back
Top Bottom