Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,850
Akihojiwa na gazeti la Mwananchi Mh Tundu Lissu amesema, tunataka Rais Magufuli atuambie, waliokaepa kodi bandarini ni kina nani na kwanini hatuwaoni Mahakamani.
Hatutakubali atuambie tu ameongeza makusanyo ya kodi. Atuambie waliokwepa wako wapi maana kukwepa kodi ni kosa kubwa kisheria"alisema Lissu"
================
Chanzo: Mwananchi
Hatutakubali atuambie tu ameongeza makusanyo ya kodi. Atuambie waliokwepa wako wapi maana kukwepa kodi ni kosa kubwa kisheria"alisema Lissu"
================
Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema upinzani utaendeleza mapambano dhidi ya ufisadi kwa kuwa ajenda za Taifa ni nyingi na Rais John Magufuli hataweza kuzitekeleza zote.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Lissu alisema tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akiwabana watendaji wa Serikali wanaoonekana kutowajibika na hivyo kuiingizia Serikali hasara ya mabilioni, akianzia bandarini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambako amewafukuza kazi vigogo kadhaa.
Lissu ambaye pia Mbunge wa Singida Mashariki, alisema ufisadi ndani ya Serikali ya CCM ni mfumo ambao Rais Magufuli hataweza kuufumua wote katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake.
Akijibu swali lililotaka aeleze ajenda mpya ya upinzani, baada ya Rais kuonekana kuichukua ya ufisadi na kuifanyia kazi alisema: “Magufuli hawezi kuua upinzani kama baadhi ya watu wanavyodhani kwa sababu ili afanikiwe hilo, inabidi kwanza afanye kazi ya ziada; aache tabia za CCM na akubali kuimaliza CCM Zanzibar kwa kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) amtangaze mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana ambaye sisi tunaamini ni Maalim Seif (Sharif Hamad) na akubali kuimaliza CCM Dar es Salaam kwa kusimamia uchaguzi wa meya,” alisema Lissu.
Lissu alisema kitendo cha Rais Magufuli kumteua Profesa Sospeter Muhongo kuwa waziri kimerudisha ajenda ya ufisadi wa Escrow bungeni. Alisema sasa wabunge hawahoji utekelezaji wa maazimio yake kuhusu suala hilo pekee, bali pia kina nani walichukua Sh73 bilioni zilizowekwa kwenye Benki ya Stanbic.
“Magufuli pia akitaka kuua upinzani nchini, atuambie waliokwepa kodi bandarini ni akina nani na kwa nini hatuwaoni mahakamani. Hatutakubali atuambie tu kwamba ameongeza makusanyo ya kodi, aseme waliokwepa wako wapi kwa sababu kukwepa kodi ni kosa kubwa kisheria,” alisema.
Alifafanua Katiba imezungumzia kosa la kukwepa kodi kwa msisitizo mkubwa, ikiwazuia wote watakaobainika kugombea ubunge: “Sasa hawa waliokwepa lazima tuwajue ili tuje kuwazuia kama wataamua kukwepa kugombea ubunge au kama ni wabunge tuwapinge mahakamani,” alisema.
Amsikitikia Magufuli
Lissu alisema anamwonea huruma Rais Magufuli kwa kuwa ana wakati mgumu zaidi kuliko watangulizi wake, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
“Tena hilo niliweke wazi kwamba kati ya marais wa CCM Mkapa ndiye aliyefanikiwa kuutesa upinzani. Aliingia madarakani kwa asilimia 61 ya kura na uchaguzi uliofuata asilimia ya ushindi wake ikaongezeka hadi asilimia 81 na katika kipindi chote cha utawala wake, nguvu ya upinzani ilipungua,” alisema. “Baada ya hapo upinzani ukakua kwa kasi. Kumbuka Kikwete alishinda kwa asilimia kubwa lakini uchaguzi uliofuata alishuka kwa kasi kubwa na upinzani ukakua. Faida aliyokuwa nayo Kikwete ni kuendeleza mazuri aliyoanzisha Mkapa.”
Lissu alisema tofauti na watangulizi wake hao, Rais Magufuli ameshinda kwa asilimia ndogo, lakini pia amechaguliwa kurithi matatizo lukuki ya CCM katika mazingira ambayo upinzani una nguvu kubwa.
Chanzo: Mwananchi