Lissu: TUCTA ndiye adui wa kwanza wa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mbunge wa Jimbo la Singida ambaye pia Raisi wa Chama cha Wanasheria TLS Mhe Tundu Lissu asema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ndiye adui wa kwanza wa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyakazi kama inavyotarajiwa

=========

Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, amesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) ndiye adui wa kwanza kwa wafanyakazi.

Lissu ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Nishati na Madini nchini (NUMET) katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani .

Alisema Shirikisho hilo ni mwiba kwa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyafakazi kama inavyotarajiwa, badala yake linashirikiana na Serikali kuwanyanyasa.

Kutokana na hali hiyo, Lissu aliwataka wafanyakazi kubadilika katika mitazamo yao ili waweze kudai haki zao na siyo kuziomba kama wanavyo fanya hivi sasa.

“Wafanyakazi badilikeni, haki haiombwi bali inatafutwa, inadaiwa hata ukiona nchi ambazo wafanyakazi wake wanapata raha leo hii walipambana hata kumwaga damu kwa ajili ya kupata haki zao za msingi, acheni kuwa ombaomba wa haki zenu,” alisema.

Alisema ni vigumu kwa wafanyakazi kuomba haki zao kwa watu ambao wamewatesa kwa zaidi ya miaka 50 kwa kuwalipa mishara midogo ambayo pia imekuwa ikikatwa kodi kubwa.

“Wafanyakazo wadogo leo hii wanahangaika na wanahitaji unafuu maana wanakatwa kodi ambayo hupunguza mishahara yao wakati wengine hawatoi hata senti tano katika kodi hali hii inafanya ubaguzi wa hali ya juu,” alisema Lissu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NUMET, Nicodemus Kajungu, alisema kuna haja ya kuundwa wa shirikisho lingine la vyama vya wafanyakazi nchini kutokana na kuonekana kuwa Tucta inawatenga.

“Leo hii sisi vyama ambavyo sio wanachama wa Tucta tumenyimwa nafasi ya kushiriki kule Moshi, hivyo basi ipo haja ya kuwa na shirikisho letu ambalo litasimamia kwa nguvu zote haki zetu na kuboresha maslahi ya wafanyakazi na Tucta iendelee na wanachama wake 12 ilionao sasa,” alisema Kajungu.

Chanzo: Mpekuzi

 
Mbunge wa Jimbo la Singida ambaye pia Raisi wa Chama cha Wanasheria TLS Mhe Tundu Lissu asema TUCTA ndiye adui wa kwanza wa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyakazi kama inavyotarajiwa

Anategemea TAWI la CCM limtetee Mfanyakazi??Wakose Chakula??TL aanze kuwaelimisha wafanyakazi waache kujikomba kwa wanachama wa CCM na kuchagua MAKADA
 
Mimi kila siku nasema Nchi haiendeshwi kwa bla bla..

Sijui ajira 52,000.. sijui umri feki.. aache bla bla..

Jana Uhuru Kenyatta sio mtu wa bla bla.. kapandisha mshahara 18% na kuna kodi zimeondolewa kwa wafanyakazi wa Kenya.

Hicho ndio wafanyakazi wa Tanzania wanataka kusikia..

Huyu amekalia bla bla tu halafu mwisho wa hotuba MNIOMBEE..!!
Nonsense.
 
Mbunge wa Jimbo la Singida ambaye pia Raisi wa Chama cha Wanasheria TLS Mhe Tundu Lissu asema TUCTA ndiye adui wa kwanza wa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyakazi kama inavyotarajiwa
LISSU alitaka TUCTA waandae mgomo nchi nzima ndio ionekane wanafanya kazi
 
Mimi kila siku nasema Nchi haiendeshwi kwa bla bla..

Sijui ajira 52,000.. sijui umri feki.. aache bla bla..

Jana Uhuru Kenyatta sio mtu wa bla bla.. kapandisha mshahara 18% na kuna kodi zimeondolewa kwa wafanyakazi wa Kenya.

Hicho ndio wafanyakazi wa Tanzania wanataka kusikia..

Huyu amekalia bla bla tu halafu mwisho wa hotuba MNIOMBEE..!!
Nonsense.
Wewe Mange kumbuka uchaguzi wa kenya ni August unategemea nini? Kama unaona kenya kuna kufaa nenda kahamie....
 
LISSU chizi alitaka TUCTA waandae mgomo nchi nzima ndio ionekane wanafanya kazi
TCTA imeshakuwa kama chama siasa
tmp_24465-IMG_20170502_0817201871348366.jpg
 
chadema wanatutukania shirikisho letu, tutafanya maazimio yetu kimyakimya wasubirie waone multiplying effects
 
Nyie mnaomsema kenyata eti kapandisha kwa ajili ya uchaguzi..ata kama lakini si ndo kapandisha wafanyakazi wameneemeka..kwa iyo na nyie ccm mnasubiri mwaka wa uchaguzi sio ndo mpandishe
 
Back
Top Bottom