Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima

Ni msimamo wa chadema, hatuko tayari kumuunga mtu mkono ambae anafikili kuwa yeye ndiye mzalendo wa kweli na kufikili yoyote yule mwenye mawazo mbadala si mzalendo.

Hatuko tayari mtu aliyekaa kwenye cabinet miaka 20 na kupitisha mikataba hii iliyotufikisha hapa Leo halafu anajitoa ufahamu nakujifanya kuwa sasa yeye ni mzalendo namba one na wale wote wanaomshauri vinginevyo si wazalendo

Mtu anaefikili kuwa anakili kuliko wote na wengine wote ni mazezeta wasio takiwa kuhoji ila kusema tu ndioooo kama ccm walivyozoea
 
Ukiwa na uwezo wa akili mdogo huwezi kumuelewa Lisu hata kidogo.
Na nina uhakika ulishangilia mkapa wakati anauza nchi na hukumwelewa pia Lisu
Ukamshangilia kikwete wakati wanapitisha sheria sa5 usiku na hukumwelewa Lisu
So sidhani kama utamwelewa now maana utakuwa ni Kilaza paseee
 
For the Record: What Goes Around Comes Around!!!

Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.

Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.

Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.

1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.

2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.

Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.

Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99 nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.

Kwa miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.

Watu hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.

Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.

Wachache tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.

Kwa mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'

Baadhi yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi '08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.

Kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.

Tunaambiwa ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama tunaona amekosea???

Hebu naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni hivyo, fikiria yafuatayo:

1) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba, kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara Tarime.

Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!

2) Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini) inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.

3) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.

4) Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi, uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic changes excepted.

Aidha, licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.

5) Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.

6) Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu miaka ya mwanzo ya '90.

Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.

Lakini je, hii ni mara ya kwanza tunaahidiwa hayo???

Mwaka '08 Jemedari Mkuu wa kabla yake alituahidi hivyo hivyo. Tuwe na subira kabla ya kuanza kushangilia prematurely.

7) Nimemsikia Magufuli akielekeza wahusika wote wa uchafu huu washughulikiwe. Kweli???

(a) Je, Jakaya Kikwete aliyesaini leseni za Bulyanhulu na Nzega mwaka '94 anaponaje???

(b) Je, Ben Mkapa aliyekuwa Rais na Mwenyekiti wa Cabinet wakati haya yanafanyika anaachwaje???

(c) Je, waliokuwa mawaziri na manaibu wao wote wakati haya yanatokea wanasalimikaje???

(d) Je, wale washangiliaji na wapiga meza wa bungeni, ambao waliunga mkono kila walicholetewa bungeni na kukipitisha kilivyo wanakosaje lawama???

8) Nimesikia Acacia Mining hawana hata leseni/usajili wa kuendeshea shughuli zao hapa nchini. Labda. Hata hivyo, jiulize yafuatayo:

(a) Hivi wamekuwa wanalipa kodi kama PAYE, SDL, income tax, withholding tax, mrahaba, n.k., kwa kutumia jina gani miaka yote hii???

(b) Je, wana akaunti yoyote katika benki za Tanzania??? Kama ndio, wamezifungua kwa jina gani???

Kama hapana, wanalipaje mishahara ya wafanyakazi wao wa Kitanzania au watoa huduma mbali mbali wa Kitanzania???

(c) Je, wanalipa bili za umeme kwa TANESCO au za simu kwa Vodacom, Tigo, Airtel, n.k. kwa kutumia jina gani???

(d) Je, wamesajiliwaje katika Soko la Hisa la Dar kama Acacia kama wanaendesha shughuli zao kihuni hivi???

(e) Kuna kitu kinaitwa 'estoppel' katika Sheria yetu ya Mikataba (the Law of Contract Act, Cap. 345) na katika Sheria yetu ya Ushahidi (the Law of Evidence, Cap. 6).

Je, estoppel haituhusu kwenye suala hili la leseni au usajili ya Acacia???

Kama estoppel inahusika, je, hoja hii ya ukosefu wa usajili ina uzito gani, kama upo, kisheria???

9) Nimesikia Sheria za Madini zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Sawa kabisa.

Lakini je, kwanini Rais Magufuli hajasema chochote juu ya Sheria za Gesi Asilia na Mafuta ambazo zilipitishwa haraka haraka kwa Hati ya Dharura baada ya sisi 'waropokaji' kutimuliwa bungeni na Spika Anna Makinda mwaka '15???

Au Rais wetu anaamini kwamba Sheria za Gesi Asilia na Mafuta hazina matatizo licha ya kupitishwa kwa utaratibu ule ule uliotumika kwa Sheria za Madini???

10) Wakati tunaingojea kwa hamu mikataba ya madini iletwe bungeni, hebu na tujiulize yafuatayo:

(a) Mikataba ya uchimbaji gesi asilia na mafuta nayo iko wapi???

(b) Mikataba ya manunuzi ya Bombardier na Dreamliner za Magufuli nayo italetwa bungeni au itabidi tusubiri aondoke madarakani kwanza kama ilivyokuwa kwa JK na BM???

(c) Mikataba ya ujenzi wa airport Chato na Reli ya Standard Geji ya Waturuki au Wachina na mabarabara kibao nayo italetwa bungeni au ndio basi tena tusubiri Bwana mkubwa atakapoondoka madarakani???

Wakati tukisubiri kufukuzwa bungeni na Spika Ndugai kwa maelekezo ya bosi wake, na wakati tukisubiri dhahama ya Bwana Mkubwa nje ya Bunge, hebu na tujiulize hivi nani hasa ndiye mzalendo wa kweli wa nchi hii???

Hebu na atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli.

Sijazungumzia bado plagiarism ya taarifa mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali katika Taarifa ya Kamati ya Prof. Osoro. Hili ni la baadae.
Tatizo kubwa ni kufanya maamuzi pasipo kuwa na sababu za kujiridhisha....all in all tujenge taifa letu pamoja.
 
MUNDENDE: Umeona ee, Lissu ni hazina ya Taifa. Hoja zake ni za kufikirisha kweli kweli. Kama ningekuwa mshauri wa Mzee ningemwambia asimchokoze Lissu kwa sababu ukweli ni kwamba kiakili na kiweledi Lissu yuko juu mno! Huyu mzee hana ubavu wa kumshinda Lissu kwa hoja. Amuulize mama Anna Makinda. Alifika mahali akamwacha Lissu kama alivyo. Huyu tunasikia kwa waliosoma nao kwamba hata maprofessa waliomfundisha walipaswa kujipanga kuja kumfundisha darasani. Alikuwa anazisoma kwa undani mada zote hata kabla hajaja professa kufundisha. Akiwa chuoni pale University of Dar es Salaam alikuwa moto wa kuotea mbali kwenye masuala ya sheria. Huyu mtu ni GENEOUS (JINIASI), ana akili nyingi mno. Nio wale wa vipaji maalumu. Ili kulinda heshima yake aliyonayo namwomba Mzee wa nchi aache kulumbana na Lissu kwenye hoja. Ni kweli yeye ana vyombo vya dola ila mwenzake ana ubongo unaofanya kazi. ana maarifa makubwa mno! Mara nyingi anaitwa nchi za nje kwa mambo mengi ya kitaalamu. Wenzetu wa nje wanamtumia vizuri sisi tunamtishia kumshuighulikia. Narudia tena, Mzee wetu aache kulumbana kwa hoja na Lissu, vinginevyo ataendelea kuumbuka. Sisi wananchi hatupendi hilo litokee maana ni mzee wetu na ni nembo ya nchi yetu, wito umetolewa tumuunge mkono, sawa, ila kwa hili la kila kukicha kulumbana na Lissu mimi simuungi mkono. Hivi kulikuwa na sababu gani za kumwingiza Lissu kwenye ripoti ya pili ya makinikia? Yaani kwa kuhamishia hasira kwa Lissu badala ya kuhamishia hasira kwa viongozi wa serikali na chama chake kwa kutuuza mchana kweupe anaonekana hamtafuti adui halisi wa wizi huu. Tunashindwa kumwelewa mzee wetu, ni nini wamekosana na Lissu? Wana ugomvi gani? Lissu ndio aliingia hiyo mikataba?
 
watamkamataje na wao pia ni mafisadi?

unajua akili zako ni zile zile za kijinga, hawa mafisadi walioko ccm wana akili na ajenda sawa na mafisadi walioko chadema

kukamatwa kwa mtu sio justification kuwa sio fisadi; hama na ondoka kwenye akili hizo
Kwahiyo Magufuli nae Fisadi kwa kauli yako hapo juu?
 
Dah hiki kichwa huwa sikiewi kabisa sijui in short si cha dunia hii kiko misplaced hapa Bongoland, more than gifted.
Hapa hata kiziwa anaelewa kwa kweli, Magu amuite jamaa wakae kwa meza moja washauriane juu ya kuondokana na hii mikataba kandamizi vile vile Magu avae ile sura ya mbusi katiba ifumuliwe then kusiwe na kinga wala ukoo wa kijani kwa waliohisika bila kujali jina wala cheo alichokuwa nacho wapelekwe kwenye mahakama ya mafisadi, wahujumu uchumi na walioliingiza taifa hili kwenye hasara kubwa kiasi cha kutokuelezeka.
 
Dah hiki kichwa huwa sikiewi kabisa sijui in short si cha dunia hii kiko misplaced hapa Bongoland, more than gifted.
Hapa hata kiziwa anaelewa kwa kweli, Magu amuite jamaa wakae kwa meza moja washauriane juu ya kuondokana na hii mikataba kandamizi vile vile Magu avae ile sura ya mbusi katiba ifumuliwe then kusiwe na kinga wala ukoo wa kijani kwa waliohisika bila kujali jina wala cheo alichokuwa nacho wapelekwe kwenye mahakama ya mafisadi, wahujumu uchumi na walioliingiza taifa hili kwenye hasara kubwa kiasi cha kutokuelezeka.
 
Umetoka na akili wewe lisu kaongea kipi kibovu yeye kasimamia sheria. Sema matatizo yenu ni vigeugeu sasa mnashangalia wakati lisu anawafundisha cha kufanya mlimzomea, kipindi anaomba miktaba iletwe ninyi mlikataa wakati anauliza miktaba kufungiwa hotelini ninyi mlimwambia hana jipya WAKATI MNAPITISHA MIKTABA MIBOVU MLIPIGA MAKOFI YEYE HAKUPIGA MAKOFI. Sasa najua unafiki wenu mtapiga makofi tena miktaba itakapo letwa bungeni hamueleweki
Kama nyinyi ¡!mlivyopiga makofi pale Mwembeyanga kwenye list of shame halafu baadae 2015 mkapiga makofi tena pale Bahari beach hotel mkimtangaza mgombea urais wa Chadema
 
Muheshimiwa Raisi, embu mpe huyu LISSU huo uwaziri wa madini kwa faida ya watanzania.
 
Ni msimamo wa chadema, hatuko tayari kumuunga mtu mkono ambae anafikili kuwa yeye ndiye mzalendo wa kweli na kufikili yoyote yule mwenye mawazo mbadala si mzalendo.
Hatuko tayari mtu aliyekaa kwenye cabinet miaka 20 na kupitisha mikataba hii iliyotufikisha hapa Leo halafu anajitoa ufahamu nakujifanya kuwa sasa yeye ni mzalendo namba one na wale wote wanaomshauri vinginevyo si wazalendo
Mtu anaefikili kuwa anakili kuliko wote na wengine wote ni mazezeta wasio takiwa kuhoji ila kusema tu ndioooo kama ccm walivyozoea
Kwani Lissu hana akili kuliko wote halo Chadema?
 
Kwahiyo unataka Lisu asiongee kwa sababu siyo msemaji wa chama? "Za kuambiwa changanya na zako"
 
Jana nimemsikiliza Rais wetu wa jamhuri ya Tanzania amesema dhahiri tena kwa ujasiri Sana,"kuwa vita ya kiuchumi huwa ningumu Sana maana huwa haimuachi mtu salaam, sasa emu tujiulize hapa ndugu zangu,ninani Adui yetu Kati ya wawekezaji ambao wameletwa na kupewa kila walichoitaji, na makada na viongozi wa serikal ya Chama la thithiemu au ni Thithiemu?
Tumjue Adui yetu ili tumtangaze hadharani
 
Mm nimeshangaa tu pale kelele za wezi..wezi...wezi zilivyopigwa na Mwenyekiti wa kamati...mpaka na kwenye mapendekezo nikasikia Acacia wachukuliwe hatua za kisheria kwa kituibia.

Mwenye kamati naye aliposimama akaimba wezi...wezi....wezi na akakubaliana na mapendekezo yote ya kamati ila alipohitimisha akasema tukae tena na wezi kwenye majadiliano tuone ni jinsi gani wanatulipa hela yetu waliyotuibia...hapo ndipo nilichoka na kuchoka Kabisa.

Tutaomba mrejesho wa mazungumzo kati ya wezi na maafisa wa serikalini kama hayo mazungumzo yatafanyika lakini isije ikawa ni danganya toto tu ya kutafuta sifa mbele ya viongozi wa dini.
Mkuu,inakera sana sana. Kwa binadamu kamili ( hapa nazungumzia binadamu na si mauchafu ambayo wamama wengine wametoa) huwezi kuelewa maana ya hili la kukaa meza moja na mwizi. Kama ulivyosema,mtu kakuibia,umeita mwizi mwizi mwizi,watu wakaanza kumfukuza na kumkamata na hivyo vitu vya wizi,then unawaambia wale waliokusaidia kumkamata kuwa wewe utakaa na mwizi wako ili mzungumze!! Mzungumze kuhusu nini? Au ushahidi haupo ni kiini macho?
 
Chesty: Tatizo watu hawajajua adui halisi wa nchi hii ni nani. Mimi nakuunga mkono kabisa! Kama CCM wataendelea kupewa nchi kila uchaguzi tutaendelea kuibiwa tu. CCM wanaishi kwa ujanja ujanja, mtaji wao ni ujinga wetu. Hao wawekezaji ndio hugaramia fedha za kuendesha kampeni kwa chama chao. Leo wanajifanya hawawajui wezi hawa wa mali zetu, kweli? Nakumbuka Rais mmoja kupitia CCM alipewa bonge la dhahabu alipotembelea mgodi fulani. Wadanganyifu sana hawa CCM. Ila kwa ujinga wetu tutwendelea kudanganywa kwamba hawakujua kuwa tunaibiwa na tutawapa kura tena. Leo tunaaminishwa kisiasa eti akina Lissu ndio wabaya wetu. haya watanzania tuendelee kudanganywa.
 
Acha kuwa kama wale waliodekishwa barabara. Huyu mpka sasa hajatuambia nini kilimfukuzisha Uwaziri mkuu.
Kina Lissu walifanya makosa makubwa sana kuwapokea hawa wezi waliokimbia genge lao kule CCM. Magufuli na Lowasa ni tofauti maana amejitolea kukiaibisha chama chake kwa maslahi ya Nchi kuliko huyo unayemtetea aliyeshindwa kutuambia kabla ya kujiuzuru kuwa nini kilitokea na ndiye aliyefanya Upinzani ukose uchaguzi mwaka 2015.
Naamini huko alipo Lowasa sasa hivi amebadilika, but huko alipo Mjomba yuko na mafisadi wengi sana. Na ili tufanikiwe kama taifa inampasa afanye vitu kama kuweka system nzuri ambayo hata akitoka madarakani mambo yataenda vzur.

Ila kwa design hii ya uongozi wake wa kibabe, vitisho na utumbuaji akiondoka madarakani tunarudi kulekule. Ni muhimu tuweke katiba sawa.
 
Back
Top Bottom