Lissu: Shujaa mwenye sura 1,000

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Mwandishi Joseph Campbell aliwahi kuandika kitabu 'The Hero with a Thousand Faces' ambapo aliongelea jinsi hadithi nyingi za mashujaa, toka enzi na enzi zinafanana sana kwa sababu kawaida wanapitia njia ile ile ya mashujaa, au kama alivyoiita 'The hero's journey'. Kuanzia Musa, Buddha, Yesu na mashujaa uliowahi kuwasoma katika vitabu, kuhadithiwa habari zao au kuwaangalia katika filamu, wote wamepitia njia inayoshabihiana kwa kiasi kikubwa.

Sihitaji kuwakumbusha masaibu aliyopitia na anayoendelea kupitia Bw. Tundu Lissu, naamini wote mtakuwa mmeshayajua mpaka sasa kwa kiasi fulani. Lakini nimeona ni muhimu kuiweka hadithi yake 'in perspective', au katika mtazamo mpana utakaokufanya uelewe nafasi yake katika historia pamoja na kwamba historia yake bado inaandikwa na kwamba bado tunaishi katika nyakati zake.

Mwandishi Campbell aligawa hatua mbalimbali na matukio muhimu ambayo mashujaa huwa wanapitia. Kimsingi kuna hatua nne ambazo nazo zimegawanywa zaidi. Nimeambatanisha picha kadhaa zinazoonyesha hatua hizo.

Hatua hizo kuu ni:
  • Initiation (Mwanzo)
  • Separation/Departure (Anaanza Safari)
  • Reign and Death (Mapambano Makali)
  • Return (Anarudi Nyumbani akiwa amebadilika)

1280px-Heroesjourney.png
Myth_quest_model.gif



Ili kufupisha mada hii kwa leo, nimeonelea nigusie tu kwa hatua alizofikia Lissu na kwamba hata maadui zake ni muhimu watambue wanapambana na nani, kama bado hawajajua mpaka sasa. Lissu yupo katika hatua za mwisho katika mzunguko huu wa mashujaa. Yupo katika 'Return Phase' ambapo, kama Campbell alivyosema 'anakuwa Master of Two Worlds'. Ameuona uovu jicho kwa jicho na akaushinda na ameuona wema wakati ambapo yupo chini kabisa ambao ulimpa nguvu.

Juzi juzi nilileta uzi humu unaoelezea ni jinsi gani uchaguzi wa 2020 unaenda kui define Tanzania ya miaka 100 ijayo. Ni uchaguzi unaogusa nafsi ya kila Mtanzania. Ni uchaguzi unaomuuliza Mtanzania, wewe ni nani? Ni swali linaloonekana jepesi lakini lina maana kubwa sana. Ninachojua kwa uhakika ni kuwa Lissu tayari anawabadilisha Watanzania wawe majasiri, waujue ukweli na wawe tayari kuusimamia, wasisite kutetea haki zao. Baadhi, labda kwa sababu ya itikadi zao, maslahi, woga au sababu zingine tunaweza tusione thamani yake leo ila kuna siku tutaijua. Vizazi vyetu vitamuangalia Lissu tofauti na baadhi yetu tunavyomuangalia.

Ninaamini wakati akiugulia majeraha ya risasi, Lissu alikuwa na nyakati za kutafakari mengi. Kuna nyakati woga ulimuingia. Kuna nyakati simanzi ilitaka kujipenyeza ndani ya nafsi yake. Kuna nyakati kujilaumu pia inawezekana kulitaka kuchukua nafasi katika nafsi yake. Inawezekana baadhi ya ndugu na marafiki walijitokeza wakamwambia, 'achana na Tanzania, siyo salama kwako, tunakushauri uendelee tu na maisha yako'. Inaonyesha amezishinda hizi sauti zote. Hizi zote ni changamoto ambazo mashujaa wanapitia.

Hotuba ya Lissu kule Njombe inaonyesha ni wazi kuwa hatarudi nyuma, dhamiri yake iko imara na yuko tayari kukutana na kitu mwandishi Campbell alichokiita 'The Meeting with the goddess', ambayo ni hatua ya mwisho katika safari ya shujaa. Kwa Lissu hii inaweza kutokea kwa njia zaidi ya moja ambazo nikipata nafasi siku chache zijazo nitazielezea zaidi.

Mungu akitujaalia uzima nitarudi tena.
 
Back
Top Bottom