Lissu: Sheria na kanuni za uchaguzi zinataka akibaki mgombea mmoja anatangazwa kupita bila kupingwa, sasa CCM wanadai kufanya kampeni ya nini sasa?

SIO MIMI, NIMEIKUTA KWA MISS ZOMBOKO. Hii ndio michezo ya sheria isiyofahamika hata na nguli wa sheria.

WIZARA ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI imewataka wagombea wa vyama vya upinzani, vilivyojitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kuandika barua za kujitoa katika uchaguzi huo, kabla ya saa 10:00 jioni ya leo tarehe 16 Novemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Sharti hilo amelitoa Mwita Waitara, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wakati akizungumza na mtandao wa MwanaHALISI ONLINE, kwa njia ya simu.

Waitara amefafanua kuwa, wagombea wanaotakiwa kuandika barua za kujitoa, ni wale walioteuliwa kugombea katika uchaguzi huo, unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019.

Waitara amesisitiza kuwa, muda huo ukifika pasipo wagombea husika kuandika barua ya kujitoa, wizara yake itaendelea kuwatambua, na kuwa watapigiwa kura, hata kama vyama vyao vimetangaza kujitoa.

“Sisi hatupokei barua ya chama ya kujitoa, tunapokea barua kutoka kwa mgombea mwenyewe. Hata kama chama kimejiondoa lakini mgombea akaendelea kushiriki, atashiriki sababu kanuni zinaruhusu.

Kila mgombea anayetaka kujitoa mwisho wa kuandika barua, ni leo saa kumi ikizidi hapo, kama kuna mgombea aliyeteuliwa na msimamizi wa uchaguzi, ataendelea kwenye mchakato na atapigiwa kura,” amesema Waitara.

Aidha, Waitara amesema kuna baadhi ya wagombea wa vyama vilivyojitoa hasa kwenye maeneo ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na Tarime mkoani Mara, wamegoma kujitoa katika uchaguzi huo.

“Kuna baadhi ya maeneo wagombea wao wamegoma kujitoa, na uchaguzi siyo chama, uchaguzi ni mgombea. Anayejitoa sio chama, mwanachama ndiyo anajitoa, mambo ya chama ni ya kwao, sisi tutaendelea kuwatambua,” amesema Waitara.

Hadi sasa vyama takribani nane, ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi na Chama cha Ukombozi wa Umma, vimetangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo, baada ya wagombea wake wengi kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi.
 
Kwanza hakuna mwendawazimu wa kuhudhuria hiyo mikutano. Waendelee na maigizo, watanzania wenye akili watakuja na uhalisia.
 
Mtajiongelesha sana, lakini mwisho wa siku CCM itanyakua viti vingi kama sio vyote.

Kama hawashindani na yoyote unategemea wachukue viti vichache? Yaani unachezesha timu yako bila timu pinzani kisha unasema timu yako itapata mshindi mkubwa, kumbe ulitegemea ipate magoli machache wakati haishindani na yoyote?
 
Pole pole anatumia matope kufikiri. Na matope haya kayarithi kutoka kwa mwenyekiti wake
Hakika usemalo ni kweli, mbona kabla ya 2017 alikuwa na akili timamu? Amekuwepo kwenye Tume ya Warioba na alionekana kuwa ni mmoja wa vijana wanaotumia akili na wenye misimamo yenye weledi.
Lakini ghafla ukatokea uteuzi kuja kufanya kazi na mwenyekiti wa hicho chama.
Hapo ndio akili ikapiga about turn na kuwa hivyo alivyo. Hakika ksirithi toka kwa huyo bosi wake, maana huko nyuma hakuwa hivyo!
 
Mbona kwenye taarifa ya habari walitangaza uchaguzi utafanyika tu sehemu ambazo kuna wagombea zaidi ya mmoja?

Sehemu yenye mgombea mmoja hakutafanyika kampeni wala uchaguzi. Hiyo imetangazwa zaidi ya siku 3 zilizopita.

Kama mgombea hajajitoa kwenye uchaguzi, na mwisho ilikuwa jana tarehe 16 kupeleka barua ya kujitoa. Kama hujapeleka bado unahesabiwa unagombea, kampeni na uchaguzi utafanyika.

Inamaana nyie wote including Lissu hamkusikia hayo matangazo au mnajifanya hamkuelewa??
 
Kama hawashindani na yoyote unategemea wachukue viti vichache? Yaani unachezesha timu yako bila timu pinzani kisha unasema timu yako itapata mshindi mkubwa, kumbe ulitegemea ipate magoli machache wakati haishindani na yoyote?
Leo tunazindua lampeni mtaani kwetu. Karibu sana!
 
Leo tunazindua lampeni mtaani kwetu. Karibu sana!

Mnazindua kampeni au mnaendeleza kampeni? Muda wote wa miaka minne mlikuwa kwenye kampeni wala hamna jipya wananchi watasikia zaidi ya marudio ya hii kampeni ya miaka minne.
 
Kwenye demokrasia geresha ndio kuna mambo ya mapingamizi na kuengua wagombea ili kuondoa ushindani.

Sheria na kanuni zote zinazoipa tume mamlaka ya kupokea mapingamizi na kuengeua wagombea zinapaswa kufutwa kwa sababu zinakiuka msingi mzima wa demokrasia ya vyama vingi na ushindani.

Sheria inapaswa kuwa kwamba wagombea waenguliwe kama sio raia au ni whalifu tena kupitia mahakama na sio tume au kamati.
 
Back
Top Bottom