Lissu: Serikali ya Magufuli wanahusika na jaribio la mauaji dhidi yangu. Sooner or later, ukweli utajulikana

CCTV ziko api kwanza,maana hizo ndo zilirekodi kila kitu.Ila bora dereva amefichwa maana angejikuta pasipojulikana.

Dereva ana ushahidi mkubwa sana wa tukio zima, ushahidi mkubwa kama CCTV ulishapotea kazi inabaki kwa Dereva tu? huyo dereva tayari kesha toa maelezo mahala pengine? kiuhalisia dereva hatobadili maelezo yake unless otherwise....ngoma inogile
 
we kilaza kabisa awataje mara ngapi?
Acha ungese wako hapo kamtaja nani kumbe na wewe ni wale wale kama huyo lisu wako..
Hapo mi nimeona analaumu magufuli magufuli akiulizwa aseme yeye hasemi anaishia tuu kulaumu...
Kumbuka alipopata fahamu aliulizwa je?aliweza kuwajua wahusika? Akajibu hajui hata mmoja leo hii eti anasema magufuli anahusika.. kwani huo magufuli ndo alienda kumfyatulia hizo risasi?usitetee /kukubali usichokijua kijana wee kaa kimya uchunguzi unaendelea
 
Kuna watu wanasema kwamba Tundu Lissu baada ya majeraha haya hataweza tena kuwa Tundu yule aliyeitetemesha Serikali ya JPM. Mimi nafikiri tofauti. Tundu Lissu wa sasa ni hatari zaidi. Tayari amepita kwenye ngazi ya ICONIC FIGURE na sasa anaelekea kwenye CULTIC FIGURE. Ameshaingia kwenye vitabu vya Historia, na anacheza kwenye uwanja, siyo Afrika mashariki, Siyo Afrika, bali Dunia nzima. Mungu akujalie Neema Tele na Baraka Tele. Ulijitoa kuwahudumia wanyonge walioonewa na makampuni ya madini kwa kushirikiana na serikali ya CCM. Leo CCM ili kujisafisha, wanataka kufuta historia hii na kukuweka pamoja na wanyonyaji. hata aibu hawana!
Sasa hivi utamuweka Tundu Lissu kwenye kundi moja na akina Mzee Mandela
 
Acha ungese wako hapo kamtaja nani kumbe na wewe ni wale wale kama huyo lisu wako..
Hapo mi nimeona analaumu magufuli magufuli akiulizwa aseme yeye hasemi anaishia tuu kulaumu...
Kumbuka alipopata fahamu aliulizwa je?aliweza kuwajua wahusika? Akajibu hajui hata mmoja leo hii eti anasema magufuli anahusika.. kwani huo magufuli ndo alienda kumfyatulia hizo risasi?usitetee /kukubali usichokijua kijana wee kaa kimya uchunguzi unaendelea
hivi mimi nikikutuma kwenda kumuua mtu kisha ukafanikisha hapo wahusika ni kina nani?
 
Nimetembea nchi nyingi sana...Ulaya niliwahi kukutana na vijana wa Kilibya(wanatoka Benghazi).Nikawauliza kuhusu Ghadafi walikuwa wanamuogopa ohh analindwa na majini Mara wale mabodyguard wake wanawake sio binadamu nk..kumbe walikuwa wamejazwa hofu na uoga..baada ya miaka mitatu Ghadafi aliuliwa na sharobaro wa miaka 21...jipeni moyo siku akija kutokea MTU wa kuwaondoa hofu na uoga hawa vijana mnaowaita "watanzania wa kawaida" mtafute kwa kukimbilia..salaam
 
Umeandika kifupi lakini umemaliza mkuu
 
ANAANDIKA TUNDU LISSU.......

Nimemsikia Mwita Mwikabe Waitara na alichokisema juu ya jaribio la mauaji dhidi yangu la September 7 mwaka jana.

Sijashangazwa hata kidogo na maneno yake. Amerudi kwenye madhehebu yake ya zamani, lazima ajionyeshe ana msimamo mkali wa kiimani kuliko wale aliowakimbia mwanzoni na ambao sasa amewarudia.

Nilishambuliwa nikiwa na dereva wangu. Niliwaona walionishambulia kwa macho yangu mwenyewe.

Niliona alichofanya dereva wangu kuanzia risasi zinarushwa mpaka aliporuka nje ya gari na kujificha.

Niliona jinsi yeye na mfanyakazi wangu wa nyumbani wakisaidiana na mfanyakazi wa Naibu Spika Tulia walivyonitoa kwenye gari yangu na kunikimbiza hospitalini kwenye gari ya mfanyakazi wa Naibu Spika Tulia.

Mimi ndiye niliyemwagiza ampigie simu Mwenyekiti Mbowe na wabunge wengine wa CHADEMA wakati wananikimbiza hospitali. Nilikuwa na fahamu na nilikuwa nazungumza mpaka nilipoingizwa theatre Dodoma General Hospital.

Nimekaa na dereva wangu miezi minne Nairobi Hospital. Polisi walileta ujumbe kwamba wanataka kuja kunihoji mimi na dereva wangu.

Tuliwaambia waje. Hawakuonekana mpaka tumeondoka Kenya na kuja Ubelgiji. Leo hii ni miezi saba tangu tuje Ubelgiji. Hawajaonekana.

Tuna uhusiano wa kibalozi na Ubelgiji wa miaka mingi. Wana Ubalozi kwetu na tuna Ubalozi hapa kwao. Serikali ya Magufuli haijaomba msaada wa Serikali ya Ubelgiji ili utaratibu wa kumhoji huyu dereva au mimi mwenyewe ufanyike.

Tuna sheria iliyotungwa na Bunge letu inayoitwa Mutual Assistance in Criminal Matters Act, ambayo imeweka utaratibu wa nini kifanyike mtuhumiwa wa jinai au shahidi anapokuwa kwenye nchi nyingine. Hakuna mwenye habari nayo.

Jeshi la Polisi la Tanzania ni mwanachama wa Interpol (International Police Organization) ambayo inaweza kusaidia upelelezi wa jambo hili. Interpol nayo imesahaulika.

Dereva wangu amesafiri mchana kweupe kutoka Dodoma hadi Nairobi. Ametumia hati ya muda ya kusafiria iliyotolewa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji ya Tanzania mpakani Namanga.

Amekuja Ubelgiji kwa hati ya muda ya kusafiria iliyotolewa na Ubalozi wa Ubelgiji Nairobi kwa sababu hati ya muda ya Tanzania ilikwisha muda wake.

Anaishi Ubelgiji mchana kweupe. Niko naye muda mwingi. Aliyekuwa Balozi wetu hapa na maafisa Ubalozi wa kwetu wamenikuta naye hospitali. Nimemtambulisha kwao.

IGP Sirro alishasema hadharani kwamba Jeshi la Polisi limefunga faili la upelelezi juu ya kushambuliwa kwangu. Polisi wanajua kilichofanyika, ndio maana hawajawahi kuhangaika na taratibu hizi za kufahamu ukweli.

CHADEMA na familia yangu tulidai uchunguzi huru wa shambulio dhidi yangu. Tulisema Serikali ya Magufuli na watu wake wanahusika na jaribio la mauaji dhidi yangu. Hawawezi na hawataweza kujichunguza.

'Watu wasiojulikana' walitumwa na Magufuli na watu wake kuja kuniua. Ndio maana ulinzi wote Area D ninapokaa uliondolewa siku hiyo.

Ndio maana CCTV ya kwa Waziri wa Nishati Medard Kalemani iliondolewa baada ya tukio.

Ndio maana Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilizuiliwa kuwasilisha taarifa yake bungeni.

Ndio maana Magufuli aliwakataza Wabunge wa CCM na viongozi wa serikali kuja kuniona hospitalini Nairobi.

Ndio maana amekataza Bunge la Spika Ndugai kunitibu kama inavyotakiwa na Sheria ya Uendeshaji wa Bunge.

Ndio maana sasa tunasikia kwamba mara baada ya kushambuliwa, Magufuli aliwaelekeza Mawaziri Mwigulu Nchemba na Augustine Mahiga kukanusha hadharani kwamba Serikali yake haikuhusika na jaribio hilo la mauaji.

Ndio maana tunasikia Magufuli alitoa maagizo, mara baada ya kushambuliwa kwangu, kwamba nikifariki dunia mwili wangu ukimbizwe haraka kwetu Ikungi, Singida, kwa maziko; kusiwe na shughuli yoyote rasmi bungeni Dodoma, na kwa vyovyote vile nisipelekwe Dar yaliko makazi yangu.

Ndio maana mpaka sasa Magufuli, huyu anayependa kuonekana mcha Mungu na mwenye huruma, hajawahi kuonekana akisema chochote juu ya shambulio hilo.

Anawajua fika aliowatuma kuja kuniua. Jeshi la Polisi linawajua. Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi inawajua. Wanawaita 'watu wasiojulikana' lakini wanawajua fika.

Haya ya akina Waitara ni majaribio tu ya kupotezea kuhusika kwa Magufuli na Serikali yake. Lakini kama nilivyosema majuzi, sooner or later, ukweli utajulikana tu.

Habari zaidi, soma => DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali
Lissu sitoacha kutoa machozi kwa unyama uliotendewa, hukusthahili hata kidogo ur a man of the people and he is an enemy of the people.
 
Na kwa maelezo hayo juu ni kwamba hawezi rudi Tanzania na lzm aungane na akina chahali,Ngurumo kujifanya wakimbizi wa kisiasa. Haiingii akilini risasi 38 mtu bado uwe na uwezo wa kujitambua hadi utoe maagizo na wakati huohuo tunaambiwa kuna risasi ilikua kwenye uti wa mgongo.Waliosoma biology wanajua kaz ya uti wa mgongo.
Ukipata jeraha la uti wa mgongo kwani lazima uwe unconscious?
 
Ni watanzania wachache tena wenye sababu zao wasioamini alichoandika Lissu. Lakini hata hao wasioamini nafsi zao zinathibitisha ukweli ila kwa nje wanajifanya wanapinga. Mungu awatie hofu kwa uovu huo.
 
Mliojaribu kutoa uhai wa Lissu ndio mpo humu mnaweweseka mara awataje mara muongo etc amewataja na atawataja nyie kaeni mkao wa kuitwa hukumuni. Evidence zipo nyingiii tuu mtashangazwa yatakayokuja mbeleni. Hahahhh mtatajana tu mlifikiri mlikuwa mnapiga mbuzi??!!
Karibu nyumbani TL
 
Acha ungese wako hapo kamtaja nani kumbe na wewe ni wale wale kama huyo lisu wako..
Hapo mi nimeona analaumu magufuli magufuli akiulizwa aseme yeye hasemi anaishia tuu kulaumu...
Kumbuka alipopata fahamu aliulizwa je?aliweza kuwajua wahusika? Akajibu hajui hata mmoja leo hii eti anasema magufuli anahusika.. kwani huo magufuli ndo alienda kumfyatulia hizo risasi?usitetee /kukubali usichokijua kijana wee kaa kimya uchunguzi unaendelea
Tema cheche mkuu!asikubabaishe.
 
Wolf cry! Ulimboka alipong'olewa kucha, Kubenea alipomwagiwa tindikali, Mwangozi alipopigwa bomu, Mauaji ya kibiti, n.k. Ulishawalilia watu hawa? Laana yako ilimpata nani? Ulipata nafuu kwa kusambaza laana? Any toilet paper coupon?
Sijamlaani mtu. Mwenye akili aelewe.
 
TUSHACHOKA NA MANENO YAKE YA KUTAFUTA HEADLINES.

1. Mwanasheria gwiji
2. Amewaona waliompiga risasi
3. Bado ana backup ya watu kama akina Kibatala, Fatma Karume na wengineo
Sasa mbona haendi kushitaki mahakamani au nchi yetu hairuhusu mwananchi kuishitaki serikali au taasisi mojawapo ya serikali????
 
hivi mimi nikikutuma kwenda kumuua mtu kisha ukafanikisha hapo wahusika ni kina nani?
Hawezi kukuelewa hao akili zao walishakodisha na kuazimisha ndiyo maana kila mtu hutoa taarifa yake ktk jambo moja. Unayeongea naye hata memkwa alifeli sasa hujui kuwa unajichosha.
 
Duh!Jamaa kaamua kumlipua mtu bila kumungunya maneno!!

Lissu,kama mwanasheria,bila shaka atakuwa ana taarifa nyeti ndio maana leo kaamua kulipuka.

Nina wasiwasi "fagio la chuma" litapita baada ya hii habari kutoka.

Huyu bwana angekuwa askari,vitani angekuwa askari jasiri sana kuwahi kutokea.

Kupona kwa Lissu ulikuwa ni mpango wa Mungu ili mapenzi yake yatimie.

Yajayo yatanoga!
.......
......Kabisa Mkuu
 
Hawezi kukuelewa hao akili zao walishakodisha na kuazimisha ndiyo maana kila mtu hutoa taarifa yake ktk jambo moja. Unayeongea naye hata memkwa alifeli sasa hujui kuwa unajichosha.
cha ajabu hata CCM wanaelewa kinachoendelea hata mwenyekiti wao wa taifa
 
Back
Top Bottom