Lissu: Polisi hawana uwezo wa kukaa na Mbowe muda mrefu gerezani. Mbowe na CHADEMA hatutatoa ushirikiano

Lissu atulie hapo hapo ushahidi usio na chembe ya shaka unawekwa wazi, tena miongoni mwa mashahidi ni wanachadema wenyewe....! Mdude chadema aliwashwa hadi akaropoka ila yeye hata sio shahidi kati ya mashahidi lukuki! Hongera TISS hongera Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri.
 
Anamtelekeza Mbowe yeye akiwa ulaya, na yeye akirudi akishikwa atakosa utetezi maana sasa hakuna namna kumtelekeza Mwenyekiti wa Chama Taifa.
 
Soma alama.

Mbowe kawanyima ushirikiano polisi ndio maana haruhusiwi kuonana na ndugu zake wala mwanasheria wake.

Siyo ajabu hata chakula hali.
Huyo gaidi atakufa,mwambieni ale chakula,kifo hakina masihara sheikh
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa katika mtandao wa Kijamii wa “Club House” katika chumba kilichofunguliwa na CHADEMA cha “Mashtaka ya Ugaidi ya Mbowe na Katiba Mpya” amesema CHADEMA haitashiriki katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe

Amesema “Hatutaandika barua ya kuomba dhamana, wala yeye hataomba. Mwenyekiti hatatoa ushirikiano wa aina yoyote, sio Polisi sio Mahakamani. Waamue wao wanataka kumfanya nini”

Ameongeza, “Wakikaa naye wajue hii kelele itakuwa kubwa. Wamuachie menyewe, wakimuachia kwa masharti ya kurudi Polisi siku nyingine hatarudi. Na wakimuachia atarudi Mwanza kwenye Kongamano”

Amesisitiza, “Kama wanamuachia waamue wenyewe, na wamuachie bila masharti yoyote. Sisi hatutashiriki kwa lolote katika kesi hii tunayojua ni ya kijinga”

Awali, Lissu alieleza kuwa kabla ya Mbowe kwenda Mwanza walizungumza naye na kusema tabia ya Polisi kuwakama, kukaa nao kwa muda na kisha kuwaachia kwa masharti ya kurudi kuripoti Kituo cha Polisi kila mara wamechoka na sasa hawatakubali.
Good
 
Back
Top Bottom