Lissu: Polisi hawana uwezo wa kukaa na Mbowe muda mrefu gerezani. Mbowe na CHADEMA hatutatoa ushirikiano

Hivi vitivii vya udaku udaku online TV vinaharibu sana uwezo wa vijana wetu kufikiri. Wanaona kudai katiba na haki havina maana wanataka mbowe na lisu wakimbizane na mademu wa bongomuvi!! Wanachojua ni umbea mitandaoni tukiendelea hivi tutakuwa na vijana machawa na wambea wenzetu nchi zilizo na Dira zinasaidia vijana wao kuwa conscious na ahead na teknology na important details za dunia. Hii sio utani kumbuka mtoto umleavyo... Lazima hizi TV zipewe mwelekeo wa taifa letu nazipite humo ama zifungwe shwain!!
Vijana hawawezi Ku- argue vitu vya msingi kitaifa wanabishania gari la mtu mwezii mzima? STUPID NONSENSE!!!
 
Hapana si kwamba sijali na si kwamba kwasababu niko kwenye mfumo, nadhan kinachotusumbua ni hisia binafsi, huyu mama ana miezi 4 tu tangu awe rais wa hili taifa na, kama unafuatilia vizuri sana huyu mama suala la katiba hakukataa bali aliomba apewe muda.... ghafla anaibuka mtu kama yule Mdude tena ameachiwa nadhan kwa huruma ya mama japo kesi yake haikuwa na kichwa wala miguu....anatoa kashfa kwa mtu aliyechagiza kuachiwa kwake...huyu kijana alikosa uungwana kabisa... Nadhani wapinzani wametaka kupima kina cha maji kwanza....hata siku moja sikuwahi kufurahia uminyifu wa haki za binadamu mwenzangu.......
Kwa hiyo ili Rais aonekane mwerevu ni lazima atumie mamlaka yake kiharamia kupambana na wapinzani wake kisiasa bila sheria yoyote inayompa mamlaka hayo? Swala la Katiba ni utashi tu wa rais peke yake? Unasema mdude aliachiwa kwa msamaha wa rais,Je hukumu iliyotolewa na Judge iliingiliwa na utashi wa rais? Rubbish
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa katika mtandao wa Kijamii wa “Club House” katika chumba kilichofunguliwa na CHADEMA cha “Mashtaka ya Ugaidi ya Mbowe na Katiba Mpya” amesema CHADEMA haitashiriki katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe

Amesema “Hatutaandika barua ya kuomba dhamana, wala yeye hataomba. Mwenyekiti hatatoa ushirikiano wa aina yoyote, sio Polisi sio Mahakamani. Waamue wao wanataka kumfanya nini”

Ameongeza, “Wakikaa naye wajue hii kelele itakuwa kubwa. Wamuachie menyewe, wakimuachia kwa masharti ya kurudi Polisi siku nyingine hatarudi. Na wakimuachia atarudi Mwanza kwenye Kongamano”

Amesisitiza, “Kama wanamuachia waamue wenyewe, na wamuachie bila masharti yoyote. Sisi hatutashiriki kwa lolote katika kesi hii tunayojua ni ya kijinga”

Awali, Lissu alieleza kuwa kabla ya Mbowe kwenda Mwanza walizungumza naye na kusema tabia ya Polisi kuwakama, kukaa nao kwa muda na kisha kuwaachia kwa masharti ya kurudi kuripoti Kituo cha Polisi kila mara wamechoka na sasa hawatakubali.

Huu ni mkakati wa ajabu sana kupata kutolewa na mwanasheria. Huu ukaidi ni recipe ya jamaa yenu kufungwa kibudu, kama Serikali ina kesi ya kuwasilisha mahakamani. Katu mahakama haihitaji ushirikiano wa criminal defendant kuendesha shauri la jinai.

Katika criminal justice system, criminal defendant ana haki ya kusikilizwa (akipenda kuitumia hiyo haki), lakini hana wajibu wa kufanya chochote kuthibitisha kwamba yeye ni innocent. Hivyo, kunyamaza ni moja ya options alizonazo criminal defendant. Serikali, kwa upande wake, ni lazima ithibitishe (beyond reasonable doubt) tuhuma ilizonazo dhidi ya criminal defendant. Vinginevyo, mahakama haitamtia hatiani huyo criminal defendant.

Wapo criminal defendants kadhaa waliopata kufanya ukaidi wa aina hiyo, lakini mashauri yao ya jinai yaliendelea kama kawaida na mahakama ziliwakuta na hatia. Wafuatao ni high-profile examples ya criminal defendants waliofanya ukaidi kama huo na wakaambulia kutiwa hatiani kibudu:

1. Saddam Hussein
2. Hastings Kamuzu Banda
3. Nicolae Ceaușescu

Kuacha kutumia haki yako ya kusikilizwa ni kujinyima fursa ya kupandikiza doubts juu ya ushahidi na hoja zilizowasilishwa na Serikali. Kama ushahidi wa Serikali uko vizuri, kaidi wa aina hiyo lazima akanyee debe!
 
Ingalikuwa wewe usingaliandika ujinga wako hapa.
Kwa vile uko huru we endelea na upuuzi wako huo
 
Wewe umewahi kusikia hata mlio wa risasi achilia mbali kuguswa nayo moja mwilini??
Unajiropokea tu.
Lissu hana uwezo huo kama anakabiliwa na hali kama hiyo wakati ambao sio wa uchaguzi.
Kama naongopa kauli yangu basi Lissu asingekimbilia ughaibuni baada ya uchaguzi angebaki kupambana na kufanya ukaidi kama anao shauri.

Kwa sasa mwanaume mpambanaji kweli kweli ni Mbowe ambaye hajakimbia anawapeleka mchakamchaka wahasimu wake akiwa battlefield na siyo Lissu au Lema waliokimbia mapambano live.

Mbowe ni mwanaume hasa..
 
Nchi za wenzenu zipi?
Marekani Republicans wanapambana usiku na mchana kuzuia watu weusi wasipige kura.Kuna maandamano mengi dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi.Trump alikiwa impeached kwa sababu gani kama sio siasa kama hizi tu.
..hoja yako imenifikirisha sana.

..kinachonitatiza ni siasa za UHASAMA za nchi yetu.

..kwenye nchi za wenzetu wanasiasa hawafanyiani hila kama hizi tunazozishuhudia hapa kwetu.
 
Baada ya kuona wamebanwa na ushahidi upo CHADEMA wameamua kujificha kwenye hatutatoa ushirikiano

Lema mwenyewe kilichomkimbiza ni kujua kuna kesi ya ugaidi itarindima baada ya dereva wa Meya wa CHADEMA kumwaga mboga HADHARANI

Ingalikuwa wewe usingaliandika ujinga wako hapa.
Kwa vile uko huru we endelea na upuuzi wako huo

Ujinga ni kutokujua mahakama inaendeshaje mashauri ya jinai. Ukichagua kutokujitetea haina maana kwamba shauri lako la jinai litakwama kusikilizwa. Serikali, kama kawaida, itabeba mzigo wake wa kuthibitisha (beyond reasonable doubt) tuhuma zinazokukabili. Whether ni mimi, wewe, Mbowe au mtu mwingine yeyote, taratibu ni zilezile!

Kama kuchagua kunyamaza ingekuwa solution, hakuna criminal defendant angefungwa jela.
 
Ndugu zangu,

Ama kweli "kikulachi ki nguoni mwako" japo wanazungumza kama wanesusa lakini wana ajenda kubwa dhidi ya Mbowe.

Ukitafakari kwa makini kauli yao "Chadema haotomdhamini Mbowe" kuna kitu utagundua naam wamemchoka, hawataki atoke korokoroni, wanatamani Lissu ashike usukani.

Kuna vita kubwa "ndani ya Chadema" muda si muda watanyukana hadharani.
 
Uadui wako na Mbo

we utakufa siku si zako. Utamfuata Jiwe, I mtelling you! Mungu hawezi kuwavumilia watu kama nyinyi, Mungu atatenda juu yako.
 
Back
Top Bottom