Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,791
Awali, Lissu alieleza kuwa kabla ya Mbowe kwenda Mwanza walizungumza naye na kusema tabia ya Polisi kuwakama, kukaa nao kwa muda na kisha kuwaachia kwa masharti ya kurudi kuripoti Kituo cha Polisi kila mara wamechoka na sasa hawatakubali.Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa katika mtandao wa Kijamii wa “Club House” katika chumba kilichofunguliwa na CHADEMA cha “Mashtaka ya Ugaidi ya Mbowe na Katiba Mpya” amesema CHADEMA haitashiriki katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe
Amesema “Hatutaandika barua ya kuomba dhamana, wala yeye hataomba. Mwenyekiti hatatoa ushirikiano wa aina yoyote, sio Polisi sio Mahakamani. Waamue wao wanataka kumfanya nini”
Ameongeza, “Wakikaa naye wajue hii kelele itakuwa kubwa. Wamuachie menyewe, wakimuachia kwa masharti ya kurudi Polisi siku nyingine hatarudi. Na wakimuachia atarudi Mwanza kwenye Kongamano”
Amesisitiza, “Kama wanamuachia waamue wenyewe, na wamuachie bila masharti yoyote. Sisi hatutashiriki kwa lolote katika kesi hii tunayojua ni ya kijinga”
Awali, Lissu alieleza kuwa kabla ya Mbowe kwenda Mwanza walizungumza naye na kusema tabia ya Polisi kuwakama, kukaa nao kwa muda na kisha kuwaachia kwa masharti ya kurudi kuripoti Kituo cha Polisi kila mara wamechoka na sasa hawatakubali.